Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,

      

Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
1. Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,
Ondoka andama ndiya, nondosheya uso wako,
Ondoka wanisikiya, ziwate jeuri zako,
Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani?

2. Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri,
Haistahamilikii, uovu umekithiri,
Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri,
Sikati yako shari, enda zako wasiwasi.

3. Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha,
Viumbe na zao nyoyo, vitina kuwagotanisha,
Hiino ndio kaziyo, yenye kukufurahisha,
Ni kazi isiyokuchosha, mno umeizoeya.

4. Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani,
Ati mambo si mazuri, mambo yote tatashani,
Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini,
Nisononeke moyoni, upate kufurahika.

5. Au mara hunijiya, na kingine kisahani,
Kuhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani,
Huwa husishi nambiya, hali zao taabani,
Zingawa wakati gani? Ni zako au ni zao?

6. Na mara kuja mambiya, nitakapotoka humu,
Na kwamba yaningojea, nde maisha magumu,
Uliloni kusudiya, ni kunitiya wazimu,
Kama ndiyo yako hamu, basi unshatahayari.

(a) Eleza ujumbe uliojitokeza katika shairi hili.
(b) Fafanua muundo wa ubeti wa tatu.
(c) Eleza aina ya shairi hili.
(d) Fafanua arudhi za utunzi alizozingatia mshairi.
(e) Eleza toni ya mshairi.
(f) Andika ubeti wa tano katika lugha ya kinathari.
(g) Eleza mifano mitatu ya uhuru wa mshairi.
(h) Eleza maana ya misamiati ifuatayokama ilivyotumika katika shairi.
(i) ndiya
(ii) kisahani
(iii) nde

  

Answers


sharon
(a) Ujumbe wa mshairi.
(i) Anazungumzia kuhusu watu wapendao kusuta wengine.
(ii) Anazungumzia pia, watu ambao hupenda kusema ya wengine.
(b) Muundo wa ubeti wa tatu.
(i) Mishororo minne.
(ii) Vina vya kati (yo) na mwisho (sha) isipokuwa mshororo wa kipokeo; kina cha kati (sha) na mwisho (ya)
(iii) Mizani ni 16 kila mshororo.
(iv) Kila mshororo umegawika katika pande mbili.
(c) Aina ya ushairi;
Tarbia / unne - kila ubeti una mishororo minne.
(d) Arudhi za utunzi;
(i) Kila ubeti una mishororo minne.
(ii) Kila mshororo umegawanyika katika vipande viwili; ukwapi na utao.
(iii) Mizani 16 kila mshororo ; 8 kila kipande.
(iv) Kibwagizo cha aina ya kiishio / kimalizio.
(e) Toni ya mshairi;
(i) Malalamishi.
(ii) Ya onyo.
(iii) Kushtumu / kusuta.
(f) Lugha nathari;
(i) Mshairi anazungumzia yampatayo anapowazia mambo ya nyumbani. Huelezwa hali za kiafya za watu wake ambazo huonekana kuwa taabani. Hataki kuelezewa porojo kwani hayamhusu yeyote.
(g) Uhuru wa mshairi;
(i) Tabdila - ndiya badala ya njia
- ondokeya badala ya ondokea.
- sikiya badala ya sikia
- hunijiya badala ya hunijia
(ii) Mazida - Maiisha badala ya maisha
- Haistahamilikii badala ya haistahimiliki
- Siitaki badala ya sitaki
(iii) Inkisari - n‘ondokeya badala ya uniondokee.
- kunambiya badala ya kuniambia.
- Kaziyo badala ya kazi yako
(iv) lahoja - ndiya badala ya njia
- nde badala ya nje
- hino badla ya hiyo
- ziwate badala ya ziwache
(h) Msamiati.
(i) ndiya - njia
(ii) kisahani - fujo
(iii) nde – nje
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 10:57


Next: Give reasons why Thomas was doubtful about Jesus resurrection.
Previous: The following diagram shows the effect of electric current on lead (II) Chloride

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions