Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Eleza hali ya shaka ya mambo inavyojitokeza katika hadithi ya shaka ya mambo.

“Shaka ya Mambo” (Farouk Topan)
Eleza hali ya shaka ya mambo inavyojitokeza katika hadithi ya shaka ya mambo.

Answers


sharon
(a) Esther ana shaka ya mambo iwapo atabadilishiwa zamu na Grace ili aingie asubuhi na kutoka saa nane aende chuoni kusomea usekretari.
(b) Esther ana shaka ya mambo kwa kuwa siku hiyo Kamata hakuja kumjulia hali kama ilivyo kawaida yake apatapo nafasi na isitoshe anapompigia simu haipokei.
(c) Esther ana shaka ya mambo iwapo kweli Kamata anamjali au anashughulika kutafuta pesa.
(d) Esther ana shaka ya mambo iwapo uhuru alioutafuta ataupata kwani hata mzee Mwinyi anamchunga kama alivyochungwa nyumbani kwao.
(e) Esther ana shaka ya mambo iwapo Kamata atamfikishia pesa yule mteja mzungu aliyezisahau mezani kwani hakumjua.
(f) Mzungu mteja ana shaka ya mambo iwapo atapata usafiri kuelekea Dubai kwa mkutano siku iliyofuata kwani ndege aliyostahili kusafiria imehairishwa mara mbili.
(g) Esther ana shaka ya mambo iwapo Grace na Kamata wana uhusiano wa kimapenzi kwani Grace alimwita kamata mpenzi na walitoka pamoja siku hiyo.
(h) Esther anaposimamiwa na mvulana kwenye matatu ana shaka ya mambo Kamata anaweza kusimama na kumwachia kiti.
(i) Abiria mmoja aliyetaka kuingia matatu ana magari ya matatu yanaruhusiwa kuingia uwanja wa ndege.
(j) Esther ana shaka ya mambo mle vilabuni anamopenda Kamata kumpeleka mna usalama.
(k) Esther ana shaka ya mambo iwapo Kamata bado anamjali hasa baada ya kukataa kwenda naye disko tena ikizingatiwa kwamba wavulana hukosa subira.
(l) Esther and shaka ya mambo kuhusu uhusiano wa Kamata kwa vile wanaishi mtaa mmoja, walisoma pamoja na huja kazini pamoja.

sharon kalunda answered the question on October 3, 2019 at 06:10

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Eleza jinsi wanacheneo walivyotatua shida zinazowakumba. (Solved)

    Mstahiki Meya
    Eleza jinsi wanacheneo walivyotatua shida zinazowakumba.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • "Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi." (Solved)

    Mstahiki Meya
    "Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi."
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Anayeambiwa alisema nini baada ya kuambiwa haya?
    c) Thibitisha kuwa wanacheneo walipanda pojo.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Taja aina nne za hadithi. (Solved)

    Taja aina nne za hadithi.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii. (Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa. (Solved)

    Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • "Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …" (Solved)

    Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.
    "Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …"
    a) Eleza muktadha wa maneno haya.
    b) Eleza umuhimu wa mrejelewa katika dondoo hili kwenye riwaya.
    c) Eleza maisha ya msemaji yalivyokuwa kwa mujibu wa Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • "Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza" (Solved)

    Damu nyeusi na hadithi zingine
    "Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili.
    c) Huku ukitoa mifano, thibitisha maudhui sita ambayo yamejitokeza katika hadithi ya Damu Nyeusi na wanayoyaendeleza.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • "Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru." (Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    "Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Ni nini sifa za mvuto zinazowaleta pamoja mzungumzaji na mzungumziwa.
    c) Tambua na ufafanue mbinu inayotumika katika dondoo.
    d) Kwa mifano mwafaka fafanua tanzia hiyo inayorejelewa katika dondoo.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya. (Solved)

    Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya.
    (a) Jazanda
    (b) Uzungumzi nafsia
    (c) Majazi
    (d) Methali
    (e) Taharuki

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano. (Solved)

    Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine (Solved)

    Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine
    (i) Mke wangu
    (ii) Damu Nyeusi
    (iii) Tazamana na Mauti
    (iv) Mizizi na matawi

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • "Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (Solved)

    "Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
    Jadili.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama, (Solved)

    Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali.

    SIKUJUA!
    1. Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,
    Zisingenidhuru pembe, ngeu kuniandama,
    Samli ni lembelembe, na minofu ya minyama.

    2. Kama ningefuga mbuzi, na kondoo kundi zima,
    Ningewajengea zizi, na maziwa nikakama,
    Ningewachuna na ngozi, kutengenezea ngoma.

    3. Kama ningefuga bata, nao kuku kwa ujima,
    Chakula siyo matata, ni machicha na mtama,
    Mayai ningeyapata, na kitoweo kizima.

    4. Kumbe nimefuga punda, mashuzi ndio heshima,
    Ni ukaidi na inda, mateke kurusha nyuma,
    Nyama limekuwa nunda, mfugaji humuuma.

    Kiitikio
    Sikujua wa kufuga, mnyama mwenye faida

    SHAIRI B
    Afrika na Watu Wake

    Mimi ninaona mgonjwa
    Bado amelala kitandani.
    Kama hatutamtoa miiba iliyobaki
    Mgonjwa hataweka miguu yake chini
    Ili kutembea bila ya kujiegemeza.

    Miiba iliyomo ndani mwetu lazima
    Pia iondolewe upesi kabla haijaingia
    Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi.
    Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma
    Halafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi.

    Lakini kuitoa miiba hii
    Tunahitaji macho makali
    Mikono isiyotetemeka
    Moyo usio na huruma
    Na kuona miiba ilipoingilia.

    MASWALI
    (a) Onyesha jinsi ujumbe unaopatikana katika ubeti wa nne wa Shairi A na Shairi la B unavyokatisha tamaa.
    (b) Eleza maana ya mshororo huu kama unavyojitokeza kwenye ubeti wa pili wa shairi B.
    Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma.
    (c) Linganua sifa za kimuundo ukizingatia ubeti wa pili wa Shairi A na Shairi B.
    (d) Ukizingatia Mshororo wa kwanza kwenye ubeti wa pili wa Shairi A, onyesha jinsi Mshairi alivyotumia kibali chake.
    (e) Onyesha sifa moja ambayo inadhihirika kwenye shairi la B na ambayo hutawala tungo za aina hii.
    (f) Nafsi neni amedhihirisha toni gani kwenye shairi A?
    (g) Taja nafsi mbili nenwa kwenye shairi la B.
    (h) Andika ubeti wa mwisho wa shairi B kwa lugha ya nadhari.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia? (Solved)

    SABUNI YA ROHO
    Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
    Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia,
    Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
    Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
    Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
    Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima.
    Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
    Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
    Sura zao ‗mefufua, wanazuru kila njanja,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
    Watazame mayatima, kwao kumekua duni,
    Webebe waliokuwa, wainue walio chini,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
    Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
    Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Umevunja usuhuba, familia zazozana,
    Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
    Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
    Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
    Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
    Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
    Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii. (Solved)

    Mstahiki Meya
    Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua. (Solved)

    Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee" (Solved)

    Damu Nveusi na Hadithi nyingine
    "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Thibitisha ufaafu wa anwani ya hadithi hii.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……." (Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."
    (a) Weka dondoo hili katika muktadha wake .
    (b) Eleza tamathali mbili zilizotumika katika dondoo hili.
    (c) Eleza aina za kiu na njaa zilizomkumba mrejelewa wa kwanza.
    (d) Mrejelewa wa pili alishindwa mtihani wa maisha. Jadili.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • "Duniani kuna watu na viatu" (Solved)

    Tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
    "Duniani kuna watu na viatu"
    (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
    (b) Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao. (Solved)

    Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.
    (i) Diwani wa tatu
    (ii) Bili
    (iii) Mhubiri
    (iv) Diwani I na II

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)