
(i) Meya kukosa kustawisha mji wa Cheneo na kulinganisha ufanisi wake na miji midogo na dhaifu.
(ii) Meya kukataa kuonana na viongozi wa wafanyakazi. Na anapokutana nao anapuuza malalamishi yao.
(iii) Meya anapuuza mpango wa miaka kumi na kusema kuwa ana mipango ya millennia.
(iv) Mikutano ya baraza kufanywa kwa nadra, kama tunavyoelezwa na Diwani I kuwa inafanywa hasa wakati jambo kama mgomo kutokea.
(v) Meya anatoa ahadi za uongo. Alidanganya kuwa shehena ya dawa iko katika bahari kuu.
(vi) Uchafu unaenea kila mahali na uvundo kukoleza hata ndani mwa majumba kwa sababu wafanyakazi wamegoma.
(vii) Meya anakataa kuongea na wanahabari kwa kisingizio kuwa ana wageni.
(viii) Badala ya kutunza fimbo ya Meya, wanakula kiapo kuficha sin za wizi wa fimbo.
(ix) Askari badala ya kutoa ulinzi wanawafursha watu kutoka mjini.
(x) Badala ya kustawisha Cheneo, anaagiza nyimbo za kizalendo zichezwe kabla na baada ya habari miaka hamsini baada ya uhuru.
(xi) Viongozi kujiongeza mishahara kiholela, kujilipa overtime na marupurupu ilhali baraza lina nakisi.
(xii) Meya kujifanya kuwa hajui watu wa Cheneo wanateseka (njaa, umaskini, magonjwa). Amefumbia macho matatizo yao.
(xiii) Meya kutoshughulika kuboresha elimu Cheneo na kuwapeleka wanawe ng’ambo kusomea huko.
(xiv) Diwani I na Diwani II wamekosa kuwajibika kama washauri wa meya wanampotosha badala ya kumkosoa.
(xv) Meya kutegemea ushauri wa mtu asiye na taaluma wala sifa za uongozi kwa mfano kesi ya mwanakandarasi, kuuza fimbo.
Kavungya answered the question on October 4, 2019 at 13:35
-
Jaza viashiria vya uradidi vya mbali kidogo.
i) Mbuzi –
ii) Gazeti –
(Solved)
Jaza viashiria vya uradidi vya mbali kidogo.
i) Mbuzi –
ii) Gazeti –
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Andika sentensi tatu ambazo zaweza kuwa sahihisho la sentensi hii:-
Kule ndimo alipoingia
(Solved)
Andika sentensi tatu ambazo zaweza kuwa sahihisho la sentensi hii:-
Kule ndimo alipoingia
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
RIWAYA.
K Walibora: Kidagaa Kimemwozea.
“Kama ilivyo ada yake usiku uliotangulia alikuwa kenda kwa shughuli fulani alizoziita kusuluhisha mgogoro wa ardhi.”
Eleza migogoro inayojidhihirisha katika riwaya ya Kidagaa...
(Solved)
RIWAYA.
K Walibora: Kidagaa Kimemwozea.
“Kama ilivyo ada yake usiku uliotangulia alikuwa kenda kwa shughuli fulani alizoziita kusuluhisha mgogoro wa ardhi.”
Eleza migogoro inayojidhihirisha katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Ainisha nomino zilizopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo;
Kikosi cha askari kiliwanasa wezi waliohusika katika wizi wa ng‘ombe katika tarafa ya kindondoni.
(Solved)
Ainisha nomino zilizopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo;
Kikosi cha askari kiliwanasa wezi waliohusika katika wizi wa ng‘ombe katika tarafa ya kindondoni.
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Andika kinyume
Wavulana watatu wanaingia darasani kwa haraka.
(Solved)
Andika kinyume
Wavulana watatu wanaingia darasani kwa haraka.
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia kirejeshi “O”
Mtoto anayelia huchapwa
(Solved)
Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia kirejeshi “O”
Mtoto anayelia huchapwa
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali.Mungu naomba subira, subira nayo imaniImani iliyo bora, bora hapa dunianiDuniani mwa kombora, kombora nayo hianiHiani pamwe ukora wenye kuhini.Kuhini...
(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali.
Mungu naomba subira, subira nayo imani
Imani iliyo bora, bora hapa duniani
Duniani mwa kombora, kombora nayo hiani
Hiani pamwe ukora wenye kuhini.
Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhulu
Ufidhuli wa kudhuri, kudhuri wangu muwili
Muwili hata kiclari, kidari kuwa thakili
Thakili kisinawiri, kisinawiri misuli.
Misuli kuwa hafith, hafifu kama muwele
Muwele wa hitilafu, hitilafi ya nduwele
Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele
Milele kutoniafu, kutoniafu na vishale.
Vishale vinitomele, vitomele vikwato
Vikwato pia maole, maole kufanya mito
Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto
Kitoto kilo vipele, vipele vyenye fiakuto.
Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka
Kutamka wazi vino, vino subira kutaka
Kutaka imani mno, mno n’sipate wahaka
Wahaka wa matukano, matukano na mashaka.
Mashaka haya ya leo, leo yawe yamepita
Yaniepita na vilio, vilia vipishe nyota
Nyota njema ing’arao, ing’arao kunikita
Kunikita salamani, salamani nikadata.
a) Kwa nini nafsi neni inaomba subira na amani?
b) Shairi hili ni la aina gani kwa kuzingatia
(i) Mpangilio wa maneno
(ii) Mpangilio wa vina.
c) Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi
d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari.
e) Kwa kutolea mifano, eleza jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Tumia amba – rejeshi na nomino ulizopewa katika sentensi kuonyesha upatanisho wa kisarufi.
i) ukwenzi
ii) sandukuni.
(Solved)
Tumia amba – rejeshi na nomino ulizopewa katika sentensi kuonyesha upatanisho wa kisarufi.
i) ukwenzi
ii) sandukuni.
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Bainisha mofimu katika neno hili;
Alinizindusha
(Solved)
Bainisha mofimu katika neno hili;
Alinizindusha
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Taja ngeli za nomino zifuatazo;
i) Muundo
ii) Senti.
(Solved)
Taja ngeli za nomino zifuatazo;
i) Muundo
ii) Senti.
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Tumia neno kitoto kama;
i) kivumishi
ii) kielezi
(Solved)
Tumia neno kitoto kama;
i) kivumishi
ii) kielezi
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Taja na ueleze pingamizi zozote tano zinazokwamiza juhudi za kukuza Kiswahili
(Solved)
Taja na ueleze pingamizi zozote tano zinazokwamiza juhudi za kukuza Kiswahili
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Changanua sentensi hii kwa kutumia kielelezo cha visanduku.
Mzee aliyemdhulumu msichana yule ametiwa mbaroni tena.
(Solved)
Changanua sentensi hii kwa kutumia kielelezo cha visanduku.
Mzee aliyemdhulumu msichana yule ametiwa mbaroni tena.
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Eleza juhudi zozote tano za serikali ya Kenya katika kukuza Kiswahili
(Solved)
Eleza juhudi zozote tano za serikali ya Kenya katika kukuza Kiswahili
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Eleza matumizi ya "ku" katika sentensi hii.
Kucheza kwake kulifurahisha wengi
(Solved)
Eleza matumizi ya "ku" katika sentensi hii.
Kucheza kwake kulifurahisha wengi
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Tunga sentensi sahihi ukitumia kitenzi — nywa katika kauli ya kutendesha
(Solved)
Tunga sentensi sahihi ukitumia kitenzi — nywa katika kauli ya kutendesha
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Yakinisha sentensi hii
Mpishi asipokuwa mwangalifu chakula hakitaiva vizuri
(Solved)
Yakinisha sentensi hii
Mpishi asipokuwa mwangalifu chakula hakitaiva vizuri
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Ainisha viwakilishi katika sentensi hii
Usibanduke papa hapa
(Solved)
Ainisha viwakilishi katika sentensi hii
Usibanduke papa hapa
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Uchumi wa soko huria ni hali ya kiuchumi ambapo itokeapo amali, shughuli na harakati zote za kiuchumi ghairi ya zile...
(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Uchumi wa soko huria ni hali ya kiuchumi ambapo itokeapo amali, shughuli na harakati zote za kiuchumi ghairi ya zile ambazo ni za lazima kwa serikali au dola kama ulinzi, sheria na
mpangilio wa jamii huwa huria kwa watu binafsi. Msingi wa soko huria, sifa kuu ya utandawazi, ni kuibua na kudumisha mazingira na hali zinazochochea na kumruhusu mtu yeyote kuongozwa na hawaa, au matamanio ya kibiashara anayoyaona sawa pasi na hofu ya kuingilia na udhibiti wa serikali.
Mazingira hayo yanawapa watu satua ya kufanya maamuzi kuhusu hatima yao ya kiuchumi, uamuzi kuhusu suala la ajira yao, matumizi ya mtaji kipato na harija zake, na uwekezaji mzima. Suala mojawapo linaloibuka kuhusiana na mfano wa soko huria ni kuweka mipaka bainifu na wazi baina ya amali na shughuli zinazohusishwa na serikali na zile ambazo huachwa huria kwa watu. Kwa mfano, inaaminiwa kuwa haki ya kuishi na kulindwa dhidi ya shambulizi, liwe la kijambazi au la kigaidi, ni ya kimsingi ambayo haiwezi kuhusishwa na uwezo wa kiuchumi wa mtu binafsi. Aidha huduma za kimsingi za afya nazo zinaingia katika kumbo hili. Ikiwa huduma hizi zitaachwa huria pana uwezekano mkubwa kuwa zitaishia kuwa istihaki ya wenye mtaji na kipato cha juu tu.
Licha ya kuwepo kwa sheria au kanuni huria kutoka nyanja maalum, hutokea hali ambapo adhibiti wa kiserikali ni lazima. Hii hutokea pale ambapo ipo haja ya kuyalinda mazingira hasa kutokana na uchafuzi wa viwanda au tasnia. Aidha udhibiti huo ni lazima pale ambapo haki za watu wengine zinahusika: yaani ikiwa uhuru wa hata mtu mmoja unaadhirika kutokana na sera hizo pana haja ya kuingilia ili kuisawazisha hali yenyewe.
(a) Andika kwa muhtasari maana ya uchumi wa soko huria kulingana na taarifa hii.
(maneno 25-30)
(b) Eleza mawazo makuu yanayojitokeza katika aya ya pili na ya tatu.
(maneno 70-75)
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)
-
Toa maana ya semi Shupaa mwili.
(Solved)
Toa maana ya semi Shupaa mwili.
Date posted:
October 4, 2019
.
Answers (1)