Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Uchunguzi uliofanywa umeonyesha kuwa anasumbuliwa na uto mwingi mwilini. Uto unaweza kudondoshwa kwa kufanya mazoezi, kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na hata protini. Protini...

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata

Uchunguzi uliofanywa umeonyesha kuwa anasumbuliwa na uto mwingi mwilini. Uto unaweza kudondoshwa kwa kufanya mazoezi, kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na hata protini. Protini iwapo nyingi mwilini hugeuzwa kuwa glukosi ambayo huhifadhiwa mwilini. Hii huwa msingi wa unene pia ambao unahatarisha afya. Jamaa yake aliyeaga dunia alikuwa mgonjwa wa bolisukari ambayo inaweza kurithishwa. Kimsingi, lazima awe na welewa bora kabisa wa lishe. Mwenzake naye aliathiriwa na aflatoxins zilikuwa kwenye chakula alichokula.
(a) Sajili hii inapatikana wapi? Kwa nini?
(b) Taja sifa zinazohusishwa na sajili yenyewe

Answers


Maurice
(a) hospitalini/ uwanja kisayansi

(b) (i) Matumizi ya msamiati maalum

(ii) Matumizi ya vifupisho ambavyo vinaeleweka na wanaohusika na uwanja wenyewe

(iii) Kuwepo kwa maelezo yanayoambatanishwa na michoro kujaliza maelezo yanayotolewa

(iv) Matumizi ya alama zinazohusishwa na taaluma ya hisabati hasa katika maagizo ya
kutumia dawa

(v) Huweza kuwepo na matumizi ya maneno ya kilatini yanayohusishwa kwa kiasi kikubwa
na taaluma hii

(vi) Huweza kutumia neno mgonjwa kumweelezea mtu badala ya jina kama yule mgonjwa wa
homa ameruhusiwa kwenda nyumbani

(vii) Utohozi wa maneno hutumika

(viii) Kuna kuchanganya ndimi

(ix) Lugha hii ni ya heshima hasa upande wa mgonjwa

(x) Sarufi huzingatiwa
maurice.mutuku answered the question on October 8, 2019 at 10:02

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions