Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo. UKANDAJI Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi?

Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo.
UKANDAJI
Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi? Watu
wanaofahamika kutumia ukandaji kimatibabu toka jadi ni Wahindi,Wachina,Wagiriki,Warumi na Waafrika.
Ukandaji unajulikana kuwa na manufaa makubwa kimatibabu. Mathalani,ukandaji hufungua vitundu
vya ngozi. Ufunguzi huu huondoa sumu mwilini kupitia kwa utoaji jasho. Pili,ukandaji hupunguza mkazo wa
misuli. Misuli ikiwa na mkazo zaidi kwa muda mrefu huleta urundikaji wa asidi. Ukandaji huondoa asidi
hii,huufanya mwili kuwa mlegevu,humletea mtu uchangamfu na kuondoa uchovu.
Halikadhalika,ukandaji huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi. Hali hii huhakikisha kuwa
virutubishi vya mwili huweza kufikia viungo vyote vya mwili. Hili nalo huchangia kuzidisha uwezo wa mwili
kujikinga na maradhi. Hewa safi ya oksijeni huweza pia kusambaa kote mwilini kupitia kwa uimarishaji wa
mzunguko wa damu. Aidha,ukandaji wa taratibu na polepole hupunguza mkazo wa neva na kuziliwaza
ukandaji wa kasi huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wake.
Ukandaji unaweza kufanyiwa kiungo chochote mwili ni. Ukandaji huu huweza kuwa na matokeo
mbalimbali mwilini.
Mathalani,ukandaji wa njia ya chakula mwilini,hasa tumbo na utumbo,huimarisha usagaji wa chakula na
kuchangia uondoaji wa uchafu na sumu mwilini. Nao ukandaji wa njia ya mkonjo hustawisha uondoaji wa
chembechembe za sumu mwilini.
Kwa kawaida,viganja vya mikono hutumika katika ukandaji. Viungo hivi vinapaswa kuwa na wororo.
Wororo huu hupatikana kwa kutumia mafuta. Mafuta ambayo ni bora zaidi kwa shughuli za ukandaji ni ya
ufuta au simsim. Matumizi ya kitu chochote kama ungaunga kinachoweza kuziba vitundu vya ngozi
hayapendekezwi.
Ukandaji wapaswa kutekelezwa kwa njia ifuatayo. Mtu aanzie mikono na miguu. Kisha aingie kukanda
kifua,tumbo,mgongo na makalio. Hatimaye,akande uso na kichwa. Mtu anaweza kutumia kitambaa kukandia
mgongo. Ni bora kutumia viganja vya mikono kukandia. Kwa njia hii,manufaa huwa maradufu.
Kwanza,tutanufaika na ukandaji na wakati huo huo tutakuwa tukifanya mazoezi ya viungo. Wasioweza
kujikanda,wanaweza kuomba msaada. Ni muhimu ukandaji ufuatiwe na kuoga kwa maji vuguvugu.
Kwa walio na tatizo la shinikizo au mpumuko wa damu wanaweza kubadilisha utaratibu wa ukandaji.
Waanzie kichwani,kisha waelekee usoni,kifuani,tumboni,mgongoni,makalioni,miguuni na kuhitimisha
mikononi.
Hata hivyo,ukandaji haupaswi kufanywa wakati mtu anaugua maradhi yoyote. Wanawake wajawazito
nao wanatakiwa kuepuka ukandaji wa tumbo. Halikadhalika,ukandaji wa tumbo hauruhusiwi wakati mtu
anaendesha,ana vidonda vya tumbo au uvimbe tumboni. Hatimaye,ukandaji haupendekezwi iwapo mtu ana
maradhi ya ngozi.

MASWALI
(a) Ukandaji ni nini?
(b) Eleza manufaa matatu ya ukandaji.
(c) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa kwa njia gani?
(d) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa na nani na kwa nini?
(e) Onyesha ni lini ukandaji haupendekezwi.
(f) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika:
(i) ufunguzi
(ii) auni
(iii) maradufu
(iv) maji vuguvugu
(v) shinikizo la damu

Answers


Kavungya
(a) Ni shughuli ya kusugua na kubinyabinya viungo vya mwili kwa mikono au mashine.

(b)(i) Hufungua vitundu vya ngozi,jambo ambalo husaidia kuondoa sumu mwilini kupitia kwa
utokaji jasho.
(ii) Kupunguza mikazo ya misuli. Mikazo ya misuli mwilini kwa muda mrefu huleta
ulundikaji wa asidi mwilini; jambo ambalo ni hatari.
(iii) Huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi.
Hii hurahisisha virutubishi vya mwili kufika sehemu zote mwilini
(iv) Huondoa uchovu na kuleta uchangamfu mwilini.
(iv) Ukandaji huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wa neva hizo.

(C) Ukandaji unatakiwa kufanywa kwa kutumia mafuta,hasa ya ufuta au simsim kisha mtu
aanzie mikononi na miguuni,aingie kifuani,tumboni,mgongoni na makalioni.
Hatimaye,aingie usoni na kumalizia kichwani,iwapo anayehusika ana tatizo la shinikizo
la damu,utaratibu auazie kichwani kisha aelekee usoni,kifuani,tumboni na kumalizia
mgongoni.

(D) Unatakiwa kufanywa na mtu mwenyewe. Hii ni kwa kuwa atakuwa akijikanda vizuri na
pia atakuwa akifanya mazoezi ya kunyoosha viungo.

(E) -Wakati mtu anaugua maradhi yoyote.
-wakati mwanamke ni mjamzito
-wakati mtu anaendesha,asikande tumbo au akiwa na vidonda vya tumbo
-wakati mtu ana maradhi yoyote ya ngozi

(F)(i) kufungua
(ii) kusaidia,msaada
(iii) Mara mbili
(iv) Maji yasiyo baridi wala moto sana
(v) Mpumuko wa damu au moyo kupiga sana kwa kasi isiyokuwa ya kawaida
Kavungya answered the question on November 23, 2022 at 07:29

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions