Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Eleza tofauti kati ya sauti /z/ na /f/

Eleza tofauti kati ya sauti /z/ na /f/

Answers


Kavungya
(a) /z/ - kikwamizo

(b) /f/ kipasuo
Kavungya answered the question on November 24, 2022 at 06:13

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo. UKANDAJI Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi? (Solved)

    Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo.
    UKANDAJI
    Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi? Watu
    wanaofahamika kutumia ukandaji kimatibabu toka jadi ni Wahindi,Wachina,Wagiriki,Warumi na Waafrika.
    Ukandaji unajulikana kuwa na manufaa makubwa kimatibabu. Mathalani,ukandaji hufungua vitundu
    vya ngozi. Ufunguzi huu huondoa sumu mwilini kupitia kwa utoaji jasho. Pili,ukandaji hupunguza mkazo wa
    misuli. Misuli ikiwa na mkazo zaidi kwa muda mrefu huleta urundikaji wa asidi. Ukandaji huondoa asidi
    hii,huufanya mwili kuwa mlegevu,humletea mtu uchangamfu na kuondoa uchovu.
    Halikadhalika,ukandaji huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi. Hali hii huhakikisha kuwa
    virutubishi vya mwili huweza kufikia viungo vyote vya mwili. Hili nalo huchangia kuzidisha uwezo wa mwili
    kujikinga na maradhi. Hewa safi ya oksijeni huweza pia kusambaa kote mwilini kupitia kwa uimarishaji wa
    mzunguko wa damu. Aidha,ukandaji wa taratibu na polepole hupunguza mkazo wa neva na kuziliwaza
    ukandaji wa kasi huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wake.
    Ukandaji unaweza kufanyiwa kiungo chochote mwili ni. Ukandaji huu huweza kuwa na matokeo
    mbalimbali mwilini.
    Mathalani,ukandaji wa njia ya chakula mwilini,hasa tumbo na utumbo,huimarisha usagaji wa chakula na
    kuchangia uondoaji wa uchafu na sumu mwilini. Nao ukandaji wa njia ya mkonjo hustawisha uondoaji wa
    chembechembe za sumu mwilini.
    Kwa kawaida,viganja vya mikono hutumika katika ukandaji. Viungo hivi vinapaswa kuwa na wororo.
    Wororo huu hupatikana kwa kutumia mafuta. Mafuta ambayo ni bora zaidi kwa shughuli za ukandaji ni ya
    ufuta au simsim. Matumizi ya kitu chochote kama ungaunga kinachoweza kuziba vitundu vya ngozi
    hayapendekezwi.
    Ukandaji wapaswa kutekelezwa kwa njia ifuatayo. Mtu aanzie mikono na miguu. Kisha aingie kukanda
    kifua,tumbo,mgongo na makalio. Hatimaye,akande uso na kichwa. Mtu anaweza kutumia kitambaa kukandia
    mgongo. Ni bora kutumia viganja vya mikono kukandia. Kwa njia hii,manufaa huwa maradufu.
    Kwanza,tutanufaika na ukandaji na wakati huo huo tutakuwa tukifanya mazoezi ya viungo. Wasioweza
    kujikanda,wanaweza kuomba msaada. Ni muhimu ukandaji ufuatiwe na kuoga kwa maji vuguvugu.
    Kwa walio na tatizo la shinikizo au mpumuko wa damu wanaweza kubadilisha utaratibu wa ukandaji.
    Waanzie kichwani,kisha waelekee usoni,kifuani,tumboni,mgongoni,makalioni,miguuni na kuhitimisha
    mikononi.
    Hata hivyo,ukandaji haupaswi kufanywa wakati mtu anaugua maradhi yoyote. Wanawake wajawazito
    nao wanatakiwa kuepuka ukandaji wa tumbo. Halikadhalika,ukandaji wa tumbo hauruhusiwi wakati mtu
    anaendesha,ana vidonda vya tumbo au uvimbe tumboni. Hatimaye,ukandaji haupendekezwi iwapo mtu ana
    maradhi ya ngozi.

    MASWALI
    (a) Ukandaji ni nini?
    (b) Eleza manufaa matatu ya ukandaji.
    (c) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa kwa njia gani?
    (d) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa na nani na kwa nini?
    (e) Onyesha ni lini ukandaji haupendekezwi.
    (f) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika:
    (i) ufunguzi
    (ii) auni
    (iii) maradufu
    (iv) maji vuguvugu
    (v) shinikizo la damu

    Date posted: November 23, 2022 .    Answers (1)

  • Nani kuku....? Sosi poa leo .... Mate ndo! ndo! ndo!. Ukimanga hii hutaona daktari kwa miaka kumi..... Ng’ombe je? nani? ......nani!... Ni wewe.... poa basi naja...... a.... (Solved)

    Nani kuku....? Sosi poa leo .... Mate ndo! ndo! ndo!. Ukimanga hii hutaona daktari kwa miaka
    kumi..... Ng’ombe je? nani? ......nani!... Ni wewe.... poa basi naja......
    a. Je, sajili hii inapatikana wapi?

    b. Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza sifa nne za sajili hii.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya maneno haya: Paka na baka (Solved)

    Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya maneno haya:
    Paka na baka

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Akifisha sentensi ifuatayo: mwalimu kazungu alimuuliza mwanafunzi je unataka kunidanganya kuwa ulifika shuleni mapema (Solved)

    Akifisha sentensi ifuatayo:
    mwalimu kazungu alimuuliza mwanafunzi je unataka kunidanganya kuwa ulifika shuleni mapema

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Andika kinyume cha sentensi hii: Alipoinama nilifurahi. (Solved)

    Andika kinyume cha sentensi hii: Alipoinama nilifurahi.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Tia shadda ili kutoa maana mbili tofauti ya neno ‘katakata’. (Solved)

    Tia shadda ili kutoa maana mbili tofauti ya neno ‘katakata’.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza maana ya aina zifuatazo za silabi: Silabi funge Silabi wazi Silabi mwambatano (Solved)

    Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza maana ya aina zifuatazo za silabi:
    Silabi funge
    Silabi wazi
    Silabi mwambatano

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Neno ‘chungu’ lina maana –enye kutokuwa na tamu. Eleza maana zake zingine mbili. (Solved)

    Neno ‘chungu’ lina maana –enye kutokuwa na tamu. Eleza maana zake zingine mbili.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Andika matumizi mawili ya mshazari. (Solved)

    Andika matumizi mawili ya mshazari.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Andika katika ukubwa. Mwanamwali huyu alijinunulia viatu vya ngozi. (Solved)

    Andika katika ukubwa.
    Mwanamwali huyu alijinunulia viatu vya ngozi.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Weka Nomino hizi katika ngeli zake. Raha Kumbikumbi (Solved)

    Weka Nomino hizi katika ngeli zake.
    Raha
    Kumbikumbi

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Akifisha sentensi hii: alikufa siku ya jumapili tarehe 20 mwezi wa januari mwaka wa 2011. (Solved)

    Akifisha sentensi hii:
    alikufa siku ya jumapili tarehe 20 mwezi wa januari mwaka wa 2011.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Kwa kutoa mifano mwafaka, onyesha mianzo tofauti katika ngeli ya U-ZI. (Solved)

    Kwa kutoa mifano mwafaka, onyesha mianzo tofauti katika ngeli ya U-ZI.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Andika vigezo vitatu vinavyotumiwa kuainisha irabu. (Solved)

    Andika vigezo vitatu vinavyotumiwa kuainisha irabu.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali Ajali haina kinga. Watu wengi wanapotajiwa neno ajali, fikira zao hukimbilia moja kwa moja hadi barabarani. (Solved)

    Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali
    Ajali haina kinga. Watu wengi wanapotajiwa neno ajali, fikira zao hukimbilia moja kwa moja hadi
    barabarani. Mara chachemawazo yao huenda viwandani, mashambani au kwenye viwanja vya
    michezo. Ni nadra sana watu kufikiraia kuwa nyumbani ndiko ajali nyingi zinztokea.
    Idadi kubwa ya ajali nyumbani hutokea kimchezo tu. Watu wengi wameteleza msalani na wanapata
    majeraha mabaya. Wengine wameteleza walipokanyaga vitu vyenye unyevu sakafuni, kama vile
    mafuta, mabaki ya chakula au hata maganda ya ndizi. Ulemavu walio nao watoto na hata watu
    wazima hutokana na ajali kama hizi wasizofikiria wtu wengi.
    Ajali vilevile hutokea watu wanapozama katika shughuli au kupata jazba kuu ya kutenda. Katika hali
    hii, huweza kujiumiza au kuwaumiza wengine bila kujua.
    Hapa tunazungumzia watu ambao hujaribu kubebe mizigo yenye uzani wasiokadiria. Madhara huwa
    kuteguka viungo na kuchanika misuli. Aghalabu hulemewa na kubanwa. Mwandishi wa makala haya
    siku moja alipanda kibao kuangika picha ukutani. Ingawa alikuwa mfupi, ari ilimsukuma
    kuchuchumia. Matokeo ni kibao kilijisukuma nyuma. Mhusika alianguka akajigonga kidevu. Kitendo
    hiki kilisababisha yeye kujiuma ulimi vibaya. Kuvunjika jino na hata kuzirai. Bahati ni kuwa alikuwepo
    mtu aliyempa huduma ya kwanza na kumkimbiza hospitalini.
    Hat hivyo ajali nyingi hutokana na vifaa vya nyumbani. Zana hizi ni pamoja na visu, meko ya gesi,
    mashine zinazotumia umeme na kadhalika na huwa hatari sana, hasa kwa watoto. Kitu kidogo hata
    kama wembe huweza kusababisha madhara makubwa. Kwa hakika hakuna yeyote kati yetu, hata
    waliokulia katika makasri ya fahari asiye na kovu. Makovu haya ambayo tunayaficha katika mavazi
    yetu ni ishara ya majeraha kutokana na ajali nyumbani. Je una kovu lolote?
    Unakumbuka ulivyolipata?
    Ingawa ajali hizi haziepukiki, yawezekana kuzipunguza. Ni muhimu kukuza tabia na mazoea ya kuwa
    waangalifu nyumbani. Kwa mfano, ni hatari kuepua chungu chenye maji yanayotokota mekoni kwa
    mikono mitupu. Aidha ni kutowajibika kuchanganya kitu chochote chenye unyevu na mafuta moto
    mekoni. Watu wengi wamebambuka ngozi na nyumba kuteketea kwa namna hii. Kwa hivyo ni vizuri
    kupata ujuzi wa jinsi ya kutumia vifaa na kuhakikisha tunavirudisha ipasavyo.
    Jambo la tatu na muhimu zaidi ni kuwepo kwa vifaa pamoja na uwezo wa kutoa huduma ya kwanza.
    Inawezekana kuokoa maisha au kuounguza majeraha kwa kuchukua hatua za dharura.

    Maswali
    1. Eleza maana ya methali ‘Ajali haina kinga’

    2. Kwa nini mwandishi anasema ajali nyumbani hutokea kimchezo?

    3. Ni mambo gani mengine yanayosababisha ajali nyumbani?

    4. Onyesha vile invyowezekana kupunguza ajali nyumbani.

    5. Eleza maana ya:
    (i) Jazba
    (ii) Makasri
    (iii) Makovu
    (iv) Kuepua

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Fafanua dhima tano za fasihi simulizi katika jamii yako. (Solved)

    Fafanua dhima tano za fasihi simulizi katika jamii yako.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Sanaa ni nini? (Solved)

    Sanaa ni nini?

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Taja majukumu mawili ya lugha rasmi. (Solved)

    Taja majukumu mawili ya lugha rasmi.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Taja sifa mbili za lugha ya kitaifa. (Solved)

    Taja sifa mbili za lugha ya kitaifa.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)

  • Eleza sifa tatu za sajili ya hospitali. (Solved)

    Eleza sifa tatu za sajili ya hospitali.

    Date posted: November 22, 2022 .    Answers (1)