Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali FUNGUA SESAME Jina la Nimrod lilipotea mara tualipoanza kufanya kazi jijini Nairobi.

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali
FUNGUA SESAME
Jina la Nimrod lilipotea mara tualipoanza kufanya kazi jijini Nairobi. Marafiki na jamaa zake
waliamini kuwa alikuwa ameajiriwa huko mjini ingawa hakuna aliyeijua kazi yenyewe vizuri.
Hata hivyo waliamini kuwa lazima alikuwa na kibonge cha kazi kwa sababu alivalia kinadhifu na
kuishi maisha ya starehe. Tena yeye mwenyewe alikazania kusema kuwa amejiriwa kazi ya
maana. Marafiki zake walimfahamu kama “Bwana Sesame”. Mtu wa kwanza aliyempa jina hilo
alisema alipendezwa na ujuzi na maarifa yake. “huyu hakosi ufumbuzi wa tatizo lolote. Ni kama
ule mlango wa kisa cha Ali Baba na Wezi arobaini. Ukisema ‘fungua Sesame’ unafungu katu,”
alisema mtu huyo.
Jamaa walioishi naye katika mtaa wa Urumo walishangazwa na utaratibu wake wa kazi. Mchana
kutwa alishinda chumbani mwake. Mara nyingi utamkuta ametulia akitazama runinga yake
ndogo. Wakati mwingine atakuwa akifanya kazi yake ndogo ndogo huku akipiga mluzi bubu,
ambao haukusikika vizuri. Wakati mwingine atakuwa akiusikiliza muziki kwenye chombo chake
cha muziki kilichotingisha jingo zima kutokana na sauti yake nene.
Kwa kawaida alitoka chumbani jioni. Waliomjua walimchangamkia kutokana na
uchangamfu wake. Alipenda sana mizaha. Waliopenda kupiga soga walivutiwa na maongezi
yake hasa kuhusiana na magari. Aliyajua magari mengi. Mimi naweza kuijua aina ya gari kwa
kuusikiliza mlio wake tu”, alisema kila wakati. “wacha kutuvungavunga Bwana wee,
haiwezekani !” atasema mwingine. “nini? Unajua mimi ndiye Bwana Sesame mwenyewe!”
atasema, halafu wote wataangua kicheko.
Ilifika wakati kampuni kadha zilipoamua kuwapunguza wafanyakazi wake kutokana na hali
mbaya ya kiuchumi. Lakini Bwana Sesame hakuwa mmoja wa hao. Hali yake ilibakia vile vile.
Aliendelea kuvalia kinadhifu na kuishi maisha yake ya fawaishi. Wakati wenzake wanalalamikia
hali ngumu ya maisha, Bwana Sesame hakuwa na lolote la kumsumbua. Aliendelea kukaa bila
kazi wala bazi. Lakini watu walitambua kuwa alikua na mazoea yakutoka chumbani majira ya
jioni. Hakuna aliyejua alirejea lini.
Sikumoja Bwana Sesame alitoka jioni kama kawaida na kuelekea kwenye shughuli zake za
kawaida. Siku hiyo jamaa mmoja wa mtaani alikumbana naye kwenye lango kuu. “Bwana
Sesame,leo wapi yahe?alimwuliza. Bwana Sesame alimwangalia na kusema, “natoka nje kidogo
yahe. Jiji hili lataka ustaarabu,’ alijibu. Yule jamaa alimwangalia na kumwabia, “nina shida
kidogo, sijui kama utanifaa mwenzangu. Wajua tena hali zenyewe siku hizi,” alisema. Nini
tena?’ aliuliza Bwana Sesame.
“Nina gari langu ambalo halina redio. Natafuta moja ya bei nafuu.... Kitu kama sony hivi,”
alisema. Bwana Sesame alimwangalia na kusema, “hiyo kazi nyepesi kwangu yahe, papai kwa
kijiko!” alisema Bwana Sesame akicheka. Jamaa Yule alishukuru na wakaagana.
Bwana Sesame alishika njia kuelekea sehemu zake za kawaida majira kama haya.Naye Yule
jamaaa kapinda kama anaangalia mtaani, lakini baada ya muda akageuka na kuamua kumfuata
Bwana Sesame.
Bwana Sesame alishika tariki mpaka sehemu ya mazoea. Yule jamaa alimfuata kwambali na
mwendo wa paka. Alimwona Bwana Sesame akiingia mahali palipokuwa na banda kuukuu.
Muda si muda alitoka na jamaa wengine wakiwa wamevalia maguo ya ajabu. Yule jamaa
aliwafuata hadi mahali palipokuwa na ujia mwembamba ulioachana na barabara kuu. Alijificha
mahali, na kutokana nahali ya sehemu ile akawa haonekani.
Muda si muda palitokeza gari dogolililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja. Bwana
Sesame na wenzake walitokeza na kutupa gogo lililomzuia Yule mwanamke.
Ghafla bin vuu walimvamia; wakaifungua milango ya gari mbio na kujivurumisha ndani. Gari
lilitimuliwa kama risasi kuelekea upande wa pili. Wakati huo Yule jamaa ashaliangalia gari
lenyewe na kuzihifadhi nambari zake. Alishika njia kurudi zake chumbani.
Siku iliyofuata huyo jamaa hakuwa kazini. Alipokuwa akifungua kinywa alisikia sauti ya
kugongwa kwa mlango. Aliinuka na kwenda kuufungua. Bwana Sesame aliingia ndani. “vipi
yahe? Hujenda kazini leo? Au umelala sana Bwana?’ alisema Bwana Sesame kwa uchangamfu
wake. Muda si muda alimwonyesha redio ya gari aliyokuwa nayo. “umeipata mara moja hii
kumbe?’ aliuliza Yule jamaa. “si nilikwambia yahe! Mimi ndiyeBwana Sesame mwenyewe. Hii
kwangu si kazi. Ninafahamiana na jamaa wengi wanaoifanya kazi hii,” alisema Bwana Sesame.
“naona kweli. Ehh Bwana we! Ndipo waswahili wakasema,ukitaka kuvua vua na wavuvi!
Alisema Yule jamaa. “ni kweli kabisa!’” alijibu Bwana Sesame huku akicheka kwa furaha.
Yule jamaa alisimama kuelekea chumbani. Bwana Sesame alitulia akisubiri kupokea ujira
wake. Muda mfupi ulipita, kasha mlango wa nyumba ukagongwa. “yahe Bwana, kunagogwa
huku!” Bwana Sesame akasema. Yule jamaa alitoka chumbani na kuelekea mlangoni. Mlango
ulipofunguliwa waliingia askari polisi wawili. Bwana Sesame hakuwa na upenyu wakutokea.
Alitiwa mikononi.Hakujua kumbe Yule jamaa alikuwa kachero. Hapakuwa na ujanja tena. Siku
hiyo pwagu alipata pwaguzi. Fungua Sesame haikufaa tena.

Maswali
1. Kwa nini Nimrod alibatizwa ‘Bwana Sesame’?
2. Kwa nini watu walioishi mtaani Urumo walishangazwa na utaratibu wa kazi wa Bwana
Sesame?
3. Unafikiria ni kwanini Bwana Sesame alifahamu sana juu ya magari?
4. Je, unafikiri yule jamaa aliagiza aletewe radio alikuwa na haja sana na kifaa hicho kama
alivyosema?
5. Bwana Sesame alikuwa kachero. Unakubali? Toa maelezo?
6. Yule jamaa alipoingia chumbani na kumwancha Bwana Sesame sebuleni unafikiria
alikwenda kufanya nini
7. Je, hadithi hii ina mafunzo gani kwako?
8. Eleza maana ya misemo ifuaayo kasha itumie katika sentensi
a) Piga mluzi
b) Piga soga
c) Shika tariki

Answers


Kavungya
1. Alikuwa na ufumbuzi wa kila jambo

2. Alikaa mchana nyumbani na kutoka jioni. Alikuwa na utaratibu wa kufanya kazi wakati
usiokuwa wa kawaida.

3. Alihusika nayo sana. Inaelekea kuwa alikuwa mwizi wa magari. (kila hoja alama nusu)

4. La. Alikitumia hicho kama chambo tu.Ulikuwa mtego wa kumshika bwana Sesame.

5. La. Hakuwa kachero bali mhalifu. Alikuwa akifanya kazi ya uhalifu. Alikuwa mwizi wa
magari

6. Alikwenda kupiga simu. Kutoa taarifa kwa polisi.

7. a. siku za mwizi ni arubaini
b. Kuchuma halali ndiko kuchuma kufaako.

8. a). toa sauti kwa ulimi na mdomo
b. Kuzungumza, kupiga domo
(c) shika njia, fuata shuguli zako.
Kavungya answered the question on November 25, 2022 at 07:12

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions