Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Sahihisha sentensi zifuatazo. i. Hao mandugu wamekosana juu ya pesa. ii. Mtu mwenye anakula mkate ametumana aletewe chai.

      

Sahihisha sentensi zifuatazo.
i. Hao mandugu wamekosana juu ya pesa.
ii. Mtu mwenye anakula mkate ametumana aletewe chai.

  

Answers


Kavungya
i. Ndugu hao wamekosana kwa sababu ya pesa.

ii. Mtu mwenye kula mkate ametumana aletewe chai.
Kavungya answered the question on November 25, 2022 at 09:09


Next: Geuza kwa wingi. i. Njia hii huenda Kisumu ii. Wembe huu utafaa.
Previous: Onyesha Nomino na ueleze aina katika sentensi ifuatayo: Warembo walijifukiza manukato na kuvalia mavazi ya kupendeza.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Geuza kwa wingi. i. Njia hii huenda Kisumu ii. Wembe huu utafaa.(Solved)

    Geuza kwa wingi.
    i. Njia hii huenda Kisumu
    ii. Wembe huu utafaa.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi ifuatayo: Ningalifuzu katika mtihani wangu ningalituzwa.(Solved)

    Kanusha sentensi ifuatayo:
    Ningalifuzu katika mtihani wangu ningalituzwa.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Sahihisha sentensi ifutayo. Sukari zilizowekwa mfukoni zimenyeshewa.(Solved)

    Sahihisha sentensi ifutayo.
    Sukari zilizowekwa mfukoni zimenyeshewa.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Onyesha vitenzi kisha uvieleze ni vya aina gani. i. Kakangu amewahi kutembelea makavazi ya kitaifa. ii. Hamisi ni daktari wa meno.(Solved)

    Onyesha vitenzi kisha uvieleze ni vya aina gani.
    i. Kakangu amewahi kutembelea makavazi ya kitaifa.
    ii. Hamisi ni daktari wa meno.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Ainisha sentensi hii: Kilichopikwa(Solved)

    Ainisha sentensi hii:
    Kilichopikwa

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Andika maneno yaliyo na aina za silabi zifuatazo: i. Silabi za irabu pekee ii. Silabi za konsonanti, nusu irabu na irabu iii. Silabi za konsonanti pekee(Solved)

    Andika maneno yaliyo na aina za silabi zifuatazo:
    i. Silabi za irabu pekee
    ii. Silabi za konsonanti, nusu irabu na irabu
    iii. Silabi za konsonanti pekee

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI. Malezi mema Malezi bora si yale, mtoto kumdekeza Atafikia kilele, mzazi atampuza(Solved)

    SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI.
    Malezi mema
    Malezi bora si yale, mtoto kumdekeza
    Atafikia kilele, mzazi atampuza
    Utapiga makelele, wala hatasikiza.
    Daima usikubali, kuridhi kumpendeza
    Lazima uwe mkali, mengine kumkataza
    Na wala usikubali, maneno kuyaigiza.
    Mtoto ukimuita, hana budi kuginiza
    Sio mdomo kufyata, mamboye kuendeleza
    Ama dakika zapita,aje ikimpendeza.
    Mzazi usithubutu,mwanao kumteteza
    Uambiwapo na watu, mwanao alifanyiza
    Kuwa na hali ya utu, Kadhia kuchunguza.
    Iwapo amekusudi, makossa kuyatimiza
    Kumrudi huna budi,jukumu kutekekeza
    Lau usipomrudi, kosa taliendeleza.

    Maswali
    a) Eleza malezi mema jinsi yanavyosimuliwa na mshairi.
    b) Taja mambo matano wanayoshauriwa wazazi kutoyatenda
    c) Je, mzazi asipochukua jukumu lake, kuna athari gani kwa mtoto
    d) Toa methali moja inayoambatana na ujumbe wa Shairi hili
    e) Shairi hili lina mishororo ngapi
    f) eleza vina,vipande na mizani vya Shairi hili
    g) eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika Shairi.
    i. kumdekeza
    ii. kuginiza
    iii. mdomo kufyata
    iv. alofanyiza
    v. lau usipomrudi

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • “nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayuko" i. tambua kipera hiki ii. taja dhima moja ya kipera hiki kijumla(Solved)

    “nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayuko"
    i. tambua kipera hiki
    ii. taja dhima moja ya kipera hiki kijumla

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatia Malenga mlotukuka, kwa tungo zenu teule Tungo zenye kusifika, zenye nasaha tele(Solved)

    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatia
    Malenga mlotukuka, kwa tungo zenu teule
    Tungo zenye kusifika, zenye nasaha tele
    Naomba la uhakika, jawabu enyi wavyele
    Wa kuume tangu lini, kuukata wakushoto!
    Tangu dahari miaka, mikono ina upole
    Meungana pasi shaka, ni miwili vile vile
    Mmoja ukisumbuka, mwingine hujaa ndwele
    Wa kuume tangu lini, kuukata wa kushoto!

    MASWALI
    a. Shairi hili ni la arudhi. Dhibitisha kwa kutoa sababu tatu
    b. Nakili kibwagizo cha shairi hili
    c. Eleza ujumbe mmoja unaojitokeza kwenye shairi

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Matumizi ya lugha hutegemea mambo kadhaa. Yaeleze yoyote manne.(Solved)

    Matumizi ya lugha hutegemea mambo kadhaa. Yaeleze yoyote manne.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja na uonyeshe kiwakilishi kimilikishi.(Solved)

    Tunga sentensi moja na uonyeshe kiwakilishi kimilikishi.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Kwa kutumia sentensi moja onyesha vitenzi sambamba.(Solved)

    Kwa kutumia sentensi moja onyesha vitenzi sambamba.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Bainisha kivumishi katika sentensi hii. Matunda mawili yaliuzwa.(Solved)

    Bainisha kivumishi katika sentensi hii.
    Matunda mawili yaliuzwa.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Taja dhana zinazowakilishwa kisarufi na viambishi vilivyopigwa mistari. Walituchezea(Solved)

    Taja dhana zinazowakilishwa kisarufi na viambishi vilivyopigwa mistari.
    Walituchezea

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Bainisha ngeli ya nomino iliyopigiwa mistari. Jeshi la Kenya lilihamisha kifaru hadi mbuga ya Masai mara.(Solved)

    Bainisha ngeli ya nomino iliyopigiwa mistari.
    Jeshi la Kenya lilihamisha kifaru hadi mbuga ya Masai mara.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tambua aina za maneno zilizopigiwa mistari. Mwanafunzi mrefu alienda Nairobi(Solved)

    Tambua aina za maneno zilizopigiwa mistari.
    Mwanafunzi mrefu alienda Nairobi

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja na uonyeshe nomino dhahania.(Solved)

    Tunga sentensi moja na uonyeshe nomino dhahania.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tambua sauti yenye sifa zifuatazo. konsonanti, kipasuo, ghuna, sauti ya mdomo.(Solved)

    Tambua sauti yenye sifa zifuatazo.
    konsonanti, kipasuo, ghuna, sauti ya mdomo.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Taja ala sogezi mbili za kutamkia.(Solved)

    Taja ala sogezi mbili za kutamkia.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali FUNGUA SESAME Jina la Nimrod lilipotea mara tualipoanza kufanya kazi jijini Nairobi.(Solved)

    Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali
    FUNGUA SESAME
    Jina la Nimrod lilipotea mara tualipoanza kufanya kazi jijini Nairobi. Marafiki na jamaa zake
    waliamini kuwa alikuwa ameajiriwa huko mjini ingawa hakuna aliyeijua kazi yenyewe vizuri.
    Hata hivyo waliamini kuwa lazima alikuwa na kibonge cha kazi kwa sababu alivalia kinadhifu na
    kuishi maisha ya starehe. Tena yeye mwenyewe alikazania kusema kuwa amejiriwa kazi ya
    maana. Marafiki zake walimfahamu kama “Bwana Sesame”. Mtu wa kwanza aliyempa jina hilo
    alisema alipendezwa na ujuzi na maarifa yake. “huyu hakosi ufumbuzi wa tatizo lolote. Ni kama
    ule mlango wa kisa cha Ali Baba na Wezi arobaini. Ukisema ‘fungua Sesame’ unafungu katu,”
    alisema mtu huyo.
    Jamaa walioishi naye katika mtaa wa Urumo walishangazwa na utaratibu wake wa kazi. Mchana
    kutwa alishinda chumbani mwake. Mara nyingi utamkuta ametulia akitazama runinga yake
    ndogo. Wakati mwingine atakuwa akifanya kazi yake ndogo ndogo huku akipiga mluzi bubu,
    ambao haukusikika vizuri. Wakati mwingine atakuwa akiusikiliza muziki kwenye chombo chake
    cha muziki kilichotingisha jingo zima kutokana na sauti yake nene.
    Kwa kawaida alitoka chumbani jioni. Waliomjua walimchangamkia kutokana na
    uchangamfu wake. Alipenda sana mizaha. Waliopenda kupiga soga walivutiwa na maongezi
    yake hasa kuhusiana na magari. Aliyajua magari mengi. Mimi naweza kuijua aina ya gari kwa
    kuusikiliza mlio wake tu”, alisema kila wakati. “wacha kutuvungavunga Bwana wee,
    haiwezekani !” atasema mwingine. “nini? Unajua mimi ndiye Bwana Sesame mwenyewe!”
    atasema, halafu wote wataangua kicheko.
    Ilifika wakati kampuni kadha zilipoamua kuwapunguza wafanyakazi wake kutokana na hali
    mbaya ya kiuchumi. Lakini Bwana Sesame hakuwa mmoja wa hao. Hali yake ilibakia vile vile.
    Aliendelea kuvalia kinadhifu na kuishi maisha yake ya fawaishi. Wakati wenzake wanalalamikia
    hali ngumu ya maisha, Bwana Sesame hakuwa na lolote la kumsumbua. Aliendelea kukaa bila
    kazi wala bazi. Lakini watu walitambua kuwa alikua na mazoea yakutoka chumbani majira ya
    jioni. Hakuna aliyejua alirejea lini.
    Sikumoja Bwana Sesame alitoka jioni kama kawaida na kuelekea kwenye shughuli zake za
    kawaida. Siku hiyo jamaa mmoja wa mtaani alikumbana naye kwenye lango kuu. “Bwana
    Sesame,leo wapi yahe?alimwuliza. Bwana Sesame alimwangalia na kusema, “natoka nje kidogo
    yahe. Jiji hili lataka ustaarabu,’ alijibu. Yule jamaa alimwangalia na kumwabia, “nina shida
    kidogo, sijui kama utanifaa mwenzangu. Wajua tena hali zenyewe siku hizi,” alisema. Nini
    tena?’ aliuliza Bwana Sesame.
    “Nina gari langu ambalo halina redio. Natafuta moja ya bei nafuu.... Kitu kama sony hivi,”
    alisema. Bwana Sesame alimwangalia na kusema, “hiyo kazi nyepesi kwangu yahe, papai kwa
    kijiko!” alisema Bwana Sesame akicheka. Jamaa Yule alishukuru na wakaagana.
    Bwana Sesame alishika njia kuelekea sehemu zake za kawaida majira kama haya.Naye Yule
    jamaaa kapinda kama anaangalia mtaani, lakini baada ya muda akageuka na kuamua kumfuata
    Bwana Sesame.
    Bwana Sesame alishika tariki mpaka sehemu ya mazoea. Yule jamaa alimfuata kwambali na
    mwendo wa paka. Alimwona Bwana Sesame akiingia mahali palipokuwa na banda kuukuu.
    Muda si muda alitoka na jamaa wengine wakiwa wamevalia maguo ya ajabu. Yule jamaa
    aliwafuata hadi mahali palipokuwa na ujia mwembamba ulioachana na barabara kuu. Alijificha
    mahali, na kutokana nahali ya sehemu ile akawa haonekani.
    Muda si muda palitokeza gari dogolililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja. Bwana
    Sesame na wenzake walitokeza na kutupa gogo lililomzuia Yule mwanamke.
    Ghafla bin vuu walimvamia; wakaifungua milango ya gari mbio na kujivurumisha ndani. Gari
    lilitimuliwa kama risasi kuelekea upande wa pili. Wakati huo Yule jamaa ashaliangalia gari
    lenyewe na kuzihifadhi nambari zake. Alishika njia kurudi zake chumbani.
    Siku iliyofuata huyo jamaa hakuwa kazini. Alipokuwa akifungua kinywa alisikia sauti ya
    kugongwa kwa mlango. Aliinuka na kwenda kuufungua. Bwana Sesame aliingia ndani. “vipi
    yahe? Hujenda kazini leo? Au umelala sana Bwana?’ alisema Bwana Sesame kwa uchangamfu
    wake. Muda si muda alimwonyesha redio ya gari aliyokuwa nayo. “umeipata mara moja hii
    kumbe?’ aliuliza Yule jamaa. “si nilikwambia yahe! Mimi ndiyeBwana Sesame mwenyewe. Hii
    kwangu si kazi. Ninafahamiana na jamaa wengi wanaoifanya kazi hii,” alisema Bwana Sesame.
    “naona kweli. Ehh Bwana we! Ndipo waswahili wakasema,ukitaka kuvua vua na wavuvi!
    Alisema Yule jamaa. “ni kweli kabisa!’” alijibu Bwana Sesame huku akicheka kwa furaha.
    Yule jamaa alisimama kuelekea chumbani. Bwana Sesame alitulia akisubiri kupokea ujira
    wake. Muda mfupi ulipita, kasha mlango wa nyumba ukagongwa. “yahe Bwana, kunagogwa
    huku!” Bwana Sesame akasema. Yule jamaa alitoka chumbani na kuelekea mlangoni. Mlango
    ulipofunguliwa waliingia askari polisi wawili. Bwana Sesame hakuwa na upenyu wakutokea.
    Alitiwa mikononi.Hakujua kumbe Yule jamaa alikuwa kachero. Hapakuwa na ujanja tena. Siku
    hiyo pwagu alipata pwaguzi. Fungua Sesame haikufaa tena.

    Maswali
    1. Kwa nini Nimrod alibatizwa ‘Bwana Sesame’?
    2. Kwa nini watu walioishi mtaani Urumo walishangazwa na utaratibu wa kazi wa Bwana
    Sesame?
    3. Unafikiria ni kwanini Bwana Sesame alifahamu sana juu ya magari?
    4. Je, unafikiri yule jamaa aliagiza aletewe radio alikuwa na haja sana na kifaa hicho kama
    alivyosema?
    5. Bwana Sesame alikuwa kachero. Unakubali? Toa maelezo?
    6. Yule jamaa alipoingia chumbani na kumwancha Bwana Sesame sebuleni unafikiria
    alikwenda kufanya nini
    7. Je, hadithi hii ina mafunzo gani kwako?
    8. Eleza maana ya misemo ifuaayo kasha itumie katika sentensi
    a) Piga mluzi
    b) Piga soga
    c) Shika tariki

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)