Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Kwa kutumia sentensi moja onyesha vitenzi sambamba.

      

Kwa kutumia sentensi moja onyesha vitenzi sambamba.

  

Answers


Kavungya
Baba alikuwa akisoma kitabu.
Kavungya answered the question on November 25, 2022 at 07:59


Next: Bainisha kivumishi katika sentensi hii. Matunda mawili yaliuzwa.
Previous: Tunga sentensi moja na uonyeshe kiwakilishi kimilikishi.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index

Related Questions


 • Bainisha kivumishi katika sentensi hii. Matunda mawili yaliuzwa.(Solved)

  Bainisha kivumishi katika sentensi hii.
  Matunda mawili yaliuzwa.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Taja dhana zinazowakilishwa kisarufi na viambishi vilivyopigwa mistari. Walituchezea(Solved)

  Taja dhana zinazowakilishwa kisarufi na viambishi vilivyopigwa mistari.
  Walituchezea

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Bainisha ngeli ya nomino iliyopigiwa mistari. Jeshi la Kenya lilihamisha kifaru hadi mbuga ya Masai mara.(Solved)

  Bainisha ngeli ya nomino iliyopigiwa mistari.
  Jeshi la Kenya lilihamisha kifaru hadi mbuga ya Masai mara.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Tambua aina za maneno zilizopigiwa mistari. Mwanafunzi mrefu alienda Nairobi(Solved)

  Tambua aina za maneno zilizopigiwa mistari.
  Mwanafunzi mrefu alienda Nairobi

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Tunga sentensi moja na uonyeshe nomino dhahania.(Solved)

  Tunga sentensi moja na uonyeshe nomino dhahania.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Tambua sauti yenye sifa zifuatazo. konsonanti, kipasuo, ghuna, sauti ya mdomo.(Solved)

  Tambua sauti yenye sifa zifuatazo.
  konsonanti, kipasuo, ghuna, sauti ya mdomo.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Taja ala sogezi mbili za kutamkia.(Solved)

  Taja ala sogezi mbili za kutamkia.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali FUNGUA SESAME Jina la Nimrod lilipotea mara tualipoanza kufanya kazi jijini Nairobi.(Solved)

  Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali
  FUNGUA SESAME
  Jina la Nimrod lilipotea mara tualipoanza kufanya kazi jijini Nairobi. Marafiki na jamaa zake
  waliamini kuwa alikuwa ameajiriwa huko mjini ingawa hakuna aliyeijua kazi yenyewe vizuri.
  Hata hivyo waliamini kuwa lazima alikuwa na kibonge cha kazi kwa sababu alivalia kinadhifu na
  kuishi maisha ya starehe. Tena yeye mwenyewe alikazania kusema kuwa amejiriwa kazi ya
  maana. Marafiki zake walimfahamu kama “Bwana Sesame”. Mtu wa kwanza aliyempa jina hilo
  alisema alipendezwa na ujuzi na maarifa yake. “huyu hakosi ufumbuzi wa tatizo lolote. Ni kama
  ule mlango wa kisa cha Ali Baba na Wezi arobaini. Ukisema ‘fungua Sesame’ unafungu katu,”
  alisema mtu huyo.
  Jamaa walioishi naye katika mtaa wa Urumo walishangazwa na utaratibu wake wa kazi. Mchana
  kutwa alishinda chumbani mwake. Mara nyingi utamkuta ametulia akitazama runinga yake
  ndogo. Wakati mwingine atakuwa akifanya kazi yake ndogo ndogo huku akipiga mluzi bubu,
  ambao haukusikika vizuri. Wakati mwingine atakuwa akiusikiliza muziki kwenye chombo chake
  cha muziki kilichotingisha jingo zima kutokana na sauti yake nene.
  Kwa kawaida alitoka chumbani jioni. Waliomjua walimchangamkia kutokana na
  uchangamfu wake. Alipenda sana mizaha. Waliopenda kupiga soga walivutiwa na maongezi
  yake hasa kuhusiana na magari. Aliyajua magari mengi. Mimi naweza kuijua aina ya gari kwa
  kuusikiliza mlio wake tu”, alisema kila wakati. “wacha kutuvungavunga Bwana wee,
  haiwezekani !” atasema mwingine. “nini? Unajua mimi ndiye Bwana Sesame mwenyewe!”
  atasema, halafu wote wataangua kicheko.
  Ilifika wakati kampuni kadha zilipoamua kuwapunguza wafanyakazi wake kutokana na hali
  mbaya ya kiuchumi. Lakini Bwana Sesame hakuwa mmoja wa hao. Hali yake ilibakia vile vile.
  Aliendelea kuvalia kinadhifu na kuishi maisha yake ya fawaishi. Wakati wenzake wanalalamikia
  hali ngumu ya maisha, Bwana Sesame hakuwa na lolote la kumsumbua. Aliendelea kukaa bila
  kazi wala bazi. Lakini watu walitambua kuwa alikua na mazoea yakutoka chumbani majira ya
  jioni. Hakuna aliyejua alirejea lini.
  Sikumoja Bwana Sesame alitoka jioni kama kawaida na kuelekea kwenye shughuli zake za
  kawaida. Siku hiyo jamaa mmoja wa mtaani alikumbana naye kwenye lango kuu. “Bwana
  Sesame,leo wapi yahe?alimwuliza. Bwana Sesame alimwangalia na kusema, “natoka nje kidogo
  yahe. Jiji hili lataka ustaarabu,’ alijibu. Yule jamaa alimwangalia na kumwabia, “nina shida
  kidogo, sijui kama utanifaa mwenzangu. Wajua tena hali zenyewe siku hizi,” alisema. Nini
  tena?’ aliuliza Bwana Sesame.
  “Nina gari langu ambalo halina redio. Natafuta moja ya bei nafuu.... Kitu kama sony hivi,”
  alisema. Bwana Sesame alimwangalia na kusema, “hiyo kazi nyepesi kwangu yahe, papai kwa
  kijiko!” alisema Bwana Sesame akicheka. Jamaa Yule alishukuru na wakaagana.
  Bwana Sesame alishika njia kuelekea sehemu zake za kawaida majira kama haya.Naye Yule
  jamaaa kapinda kama anaangalia mtaani, lakini baada ya muda akageuka na kuamua kumfuata
  Bwana Sesame.
  Bwana Sesame alishika tariki mpaka sehemu ya mazoea. Yule jamaa alimfuata kwambali na
  mwendo wa paka. Alimwona Bwana Sesame akiingia mahali palipokuwa na banda kuukuu.
  Muda si muda alitoka na jamaa wengine wakiwa wamevalia maguo ya ajabu. Yule jamaa
  aliwafuata hadi mahali palipokuwa na ujia mwembamba ulioachana na barabara kuu. Alijificha
  mahali, na kutokana nahali ya sehemu ile akawa haonekani.
  Muda si muda palitokeza gari dogolililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja. Bwana
  Sesame na wenzake walitokeza na kutupa gogo lililomzuia Yule mwanamke.
  Ghafla bin vuu walimvamia; wakaifungua milango ya gari mbio na kujivurumisha ndani. Gari
  lilitimuliwa kama risasi kuelekea upande wa pili. Wakati huo Yule jamaa ashaliangalia gari
  lenyewe na kuzihifadhi nambari zake. Alishika njia kurudi zake chumbani.
  Siku iliyofuata huyo jamaa hakuwa kazini. Alipokuwa akifungua kinywa alisikia sauti ya
  kugongwa kwa mlango. Aliinuka na kwenda kuufungua. Bwana Sesame aliingia ndani. “vipi
  yahe? Hujenda kazini leo? Au umelala sana Bwana?’ alisema Bwana Sesame kwa uchangamfu
  wake. Muda si muda alimwonyesha redio ya gari aliyokuwa nayo. “umeipata mara moja hii
  kumbe?’ aliuliza Yule jamaa. “si nilikwambia yahe! Mimi ndiyeBwana Sesame mwenyewe. Hii
  kwangu si kazi. Ninafahamiana na jamaa wengi wanaoifanya kazi hii,” alisema Bwana Sesame.
  “naona kweli. Ehh Bwana we! Ndipo waswahili wakasema,ukitaka kuvua vua na wavuvi!
  Alisema Yule jamaa. “ni kweli kabisa!’” alijibu Bwana Sesame huku akicheka kwa furaha.
  Yule jamaa alisimama kuelekea chumbani. Bwana Sesame alitulia akisubiri kupokea ujira
  wake. Muda mfupi ulipita, kasha mlango wa nyumba ukagongwa. “yahe Bwana, kunagogwa
  huku!” Bwana Sesame akasema. Yule jamaa alitoka chumbani na kuelekea mlangoni. Mlango
  ulipofunguliwa waliingia askari polisi wawili. Bwana Sesame hakuwa na upenyu wakutokea.
  Alitiwa mikononi.Hakujua kumbe Yule jamaa alikuwa kachero. Hapakuwa na ujanja tena. Siku
  hiyo pwagu alipata pwaguzi. Fungua Sesame haikufaa tena.

  Maswali
  1. Kwa nini Nimrod alibatizwa ‘Bwana Sesame’?
  2. Kwa nini watu walioishi mtaani Urumo walishangazwa na utaratibu wa kazi wa Bwana
  Sesame?
  3. Unafikiria ni kwanini Bwana Sesame alifahamu sana juu ya magari?
  4. Je, unafikiri yule jamaa aliagiza aletewe radio alikuwa na haja sana na kifaa hicho kama
  alivyosema?
  5. Bwana Sesame alikuwa kachero. Unakubali? Toa maelezo?
  6. Yule jamaa alipoingia chumbani na kumwancha Bwana Sesame sebuleni unafikiria
  alikwenda kufanya nini
  7. Je, hadithi hii ina mafunzo gani kwako?
  8. Eleza maana ya misemo ifuaayo kasha itumie katika sentensi
  a) Piga mluzi
  b) Piga soga
  c) Shika tariki

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Taja vipera vitano vya semi.(Solved)

  Taja vipera vitano vya semi.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata. Mwatani: Rusha hiyo ball haraka tumechelewa five minutes. Twende daro. Omoshi: Harakisha mode anacome.(Solved)

  Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
  Mwatani: Rusha hiyo ball haraka tumechelewa five minutes. Twende daro.
  Omoshi: Harakisha mode anacome.
  Bwana Kipiti: Nendeni darasani haraka! Kisha kiranja awape vitabu vyenu vya insha
  ili mwandike barua.
  Mwatani: Sawa mwalimu. Samahani kwa kuchelewa uwanjani.
  Omoshi: Je, tutaandika barua rasmi au barua ya kawaida?
  Bwana Kipiti: Mwandike barua rasmi. Je, mnakumbuka muundo wake?
  Omoshi na Mwatani: Ndio mwalimu. Ulitufundisha jana. Asante sana mwalimu.
  Bwana Kipiti: Kumbukeni idadi ya maneno. Idadi ya maneno ni muhimu katika uandishi
  wa insha.

  (i) Eleza sajili katika dondoo.
  (ii) Eleza sifa nane za sajili hii zinazopatikana katika dondoo.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Ainisha vielezi katika katika sentensi ifuatayo. Mwanafunzi mzuri ni yule afanyaye mazoezi vizuri kila siku shuleni.(Solved)

  Ainisha vielezi katika katika sentensi ifuatayo.
  Mwanafunzi mzuri ni yule afanyaye mazoezi vizuri kila siku shuleni.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Tumia o-rejeshi kati katika sentensi ifuatayo. Kuta ambazo zilijengwa zimebomoka.(Solved)

  Tumia o-rejeshi kati katika sentensi ifuatayo.
  Kuta ambazo zilijengwa zimebomoka.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Kamilisha methali ifuatayo. Asiye na nadhari...(Solved)

  Kamilisha methali ifuatayo.
  Asiye na nadhari...

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Andika kwa wingi. Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri.(Solved)

  Andika kwa wingi.
  Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Badilisha kitenzi kisaidizi kilicho kwenye sentensi ifuatayo kiwe kishirikishi. Mvule alikuwa akilala bwenini.(Solved)

  Badilisha kitenzi kisaidizi kilicho kwenye sentensi ifuatayo kiwe kishirikishi.
  Mvule alikuwa akilala bwenini.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa. Uteo alionunuliwa umezeeka sana.(Solved)

  Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa.
  Uteo alionunuliwa umezeeka sana.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Yakinisha: Usipolipa usiingie ndani.(Solved)

  Yakinisha:
  Usipolipa usiingie ndani.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya i. Posa ii. Poza(Solved)

  Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya
  i. Posa
  ii. Poza

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Kanusha sentensi katika hali ya kuamrisha wingi. Kimbia haraka – Amka -(Solved)

  Kanusha sentensi katika hali ya kuamrisha wingi.
  Kimbia haraka –
  Amka -

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

 • Tunga sentensi yenye kivumishi cha jina.(Solved)

  Tunga sentensi yenye kivumishi cha jina.

  Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)