Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Ningeondoka ... mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.” (Shibe Inatumaliza) (a) Eleza muktadha wa maneno haya. (b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza katika dondoo. (c)...

      

“Ningeondoka ... mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.” (Shibe Inatumaliza)
(a) Eleza muktadha wa maneno haya.
(b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza katika dondoo.
(c) Kinaya kimetumika kwingine kwingi katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu. Thibitisha.
(d) Nini umuhimu wa msemaji katika hadithi?

  

Answers


Francis
(a) Eleza muktadha wa maneno haya.
? Haya ni maneno ya Jairo.
? Anahutubu katika sherehe ya kumuaga mwalimu Mosi ambaye alikuwa anastaafu kutoka kazi ya ualimu.
? Sherehe hii inafanyika shuleni.
? Jairo anamkosoa mwalimu Mosi kumpatia matumaini ya uongo masomoni ilhali alijua hawakuwa na uwezo wa kimasomo badala ya kumruhusu aende ajaribu mbinu nyingine ya kujikimu kimaisha ili awe mtu wa maana katika jamii.

(b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza katika dondoo.
? Jairo anamkosoa mwalimu kwa kumfunza na kumpa matumaini maishani badala ya kumwachilia mapema aende akaibe na kuua. Jairo analodokeza hapa ni kuwa ili mtu awe wa maana lazima aibe na aue.

(c) Kinaya kimetumika kwingine kwingi katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu. Thibitisha.
? Ni kinaya kwa Jairo kuuona uelekezi na ushauri wa mwalimu wake kama upotoshi na upotezaji wa muda. Jairo anadai alipotezewa muda kwa kupatiwa matumaini ya uongo.
? Ni kinaya pia kwa mwalimu Mosi kutaka ahutubie mtu ambaye atamkosoa badala ya kumsifu.
? Ni kinaya kwa Jairo kuona elimu haina manufaa yoyote ilhali wenzake walifaidi kutoka kwa elimu ya mwalimu wao.
? Ni kinaya kwa Jairo kumtoa bintiye na mkewe kama zawadi kwa mwalimu wake kama shukrani ya zawadi anazompa. Ni kinaya kwa mtu kubadili mkewe kama zawadi.
? Ni kinaya kwa Jairo kudai kuwa pombe ni kiliwazo cha kimawazo kinachomsahaulisha masaibu ya maisha na kumkosoa mwalimu wake kwa kumwonya dhidi ya matumizi ya pombe.
? Ni kinaya kwa mkewe jairo kukubali kitendo cha mumewe Jairo kumtoa kama zawadi kwa familia nyingine. Anakubali kubadilishwa na mali.
? Ni kinaya kwa Jairo kudai kuwa ufuska ndio raha ya maisha na kuwa uadilifu haufai. Anadai kuwa maisha ni bora bila nasaha za mwalimu.
? Ni kinaya kwa mkewe mwalimu Mosi, Sera kukubali na kumkaribisha mwanamke mwingine na watoto wake kwenye familia yake.

(d) Nini umuhimu wa msemaji katika hadithi?
? Ni kielelezo cha utovu wa nidhamu miongoni wa wanafunzi. Anakunywa pombe na hata kujihusisha katika ufuska.
? Kupitia kwake uwajibikaji wa mwalimu Mosi unajitokeza. Kama mwalimu, alimkanya kunywa pombe na hata ufuska.
? Anaendeleza maudhui ya umaskini katika hadithi.
? Anakuza sifa za wahusika wengine kama vile Mwalimu Mosi.
? Ametumiwa kudhihirisha ukweli wa methali “asante ya punda ni mateke.”
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 09:34


Next: “Hebu kwanza kanawe hilo dongo jekundu miguuni.” (Shibe Inatumaliza) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Fafanua sifa za wandani wa msemaji. (c) Jadili jinsi hadithi hii inavyoafiki...
Previous: Eleza namna maudhui ya ndoa yalivyosawiriwa katika hadithi ya Masharti ya Kisasa.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions