Mwongozo wa Kigogo Notes

Institution: Secondary

Course: Kiswahili

Content Category: Summaries

Posted By: 6965

Document Type: PDF

Number of Pages: 45

Price: KES 150
Buy with Email    Buy via WhatsApp
    

Views: 95008     Downloads: 124

Summary

Mwongozo wa tamthilia ya Kigogo.Ni mwongozo ambayo itamwezesha mwalimu pamoja na mwanafunzi kuwa na umilisi wa kuilewa Tamthilia yenyewe.Jipatie nakala yako.

Brief Overview:

MWONGOZO WA KIGOGO
MTIRIRIKO;
ONYESHO LA KWANZA.
TENDO LA KWANZA.
Ni katika karakana ya soko la Chapakazi,Sudi, Boza na Kombe wanafanya kazi ya
uchongaji.Sudi amefungulia radio huku wakiendelea na kazi yao.Ashua anawaletea chai
ya mkandaa na mahamri na kuondoka.
Habari inatolewa kwa wananchi wa Sagamoyo kuwa wana kipindi cha mwezi mzima
kusheherekea uhuru wao, wawaku buke majagina wao waliopigania uhuru na
kuwanasua kutoka utumwani, wimbo wa kizalendo unachezwa mara kwa mara.
Sudi anatofautiana na mpango wa kusheherekea uhuru kwa mwezi mzima;kwake
majagina wanaosheherekewa hawakufanya lolote katika historia ya Sagamoyo.
Kuna uchafuzi wa mazingira, viongozi hawajawajibika kusafisha soko wanadai kodi na kitu juu pia vitisho kwa wanasagamoyo.

WAZO KUU.
Kuna wale ambao wanaunga viongozi mkono kwa sababu wanafumbwa kwa mambo
yasiyo ya kimsingi.Aidha kuna wale ambao wamezinduka na kuhisi kuwa viongozi
hawajawajibika. Sudi haoni umuhimu wa sherehe za uhuru kupewa maandalizi ya
kifahali na kipindi cha mwezi mzima.

TENDO LA PILI.
Katika karakana sokoni,Kenga anawatembelea Sudi, Boza na Kombe.Ametumwa na
Majoka kuchukua vinyago vya mashujaa.Ni msimu wa mashujaa Sagamoyo, Sudi
anachonga kinyago cha shujaa wa kike ambaye kwake ni kiongozi halisi wa
Sagamoyo.Shujaa huyo hakufanya lolote, bali analifanyak sasa katika jimbo la
Sagamoyo.
Miradhi ya kuchonga vinyago inafadhiliwa kutoka nje na wananchi wanatakiwa kulipa
baada ya mwaka mmoja.
Sudi anashawishiwa kuchonga kinyago cha Ngao ili maisha yake yabadilike na jina lake
kushamiri;aidha apewe likizo ya mwezi mmoja ughaibuni.Sudi anakataa kuchonga
kinyago,Kenga anawapa keki lakini Sudi hali kwa kuwa ni makombo.Kombe anazinduka
kutokana na kauli hii, anamuunga mkono Sudi.Kenga anaondoka kisha Tunu anawasili
huku akihema na kusema kuwa mzee Kenga anapanga njama ya kuhutubia
wahuni.Wote wanaondoka.

WAZO KUU.
Maskini wanatumikizwa, wanadhalalishwa, kuletewa makombo na kukumbukwa katika
kipindi fulani tu ili kufaidi viongozi wao.
Miradi isiyo muhimu inafadhiliwa na wananchi kupakia na jukumu la kulipa ufadhili huo
kupitia kodi.Viongozi hushawishi wanyonge ili kuwatumikia.
TENDO LA TATU
Ni katika nyumba ya Sudi barazani baada ya soko kufungwa.Tunu na Sudi wanafika
kiwandani anapofanya kazi Siti,wafanyakazi wanagoma na vijana watano kuuliwa na
wafanyakazi kuumia.
Kiini cha maandamano ni bei ya chakula Kupandishwa soko linapofungwa.
Sudi na Tunu wamejitolea kutetea haki na uhuru wa wanasagamoyo hata kama ni kwa
pumzi zao za mwisho baada ya kufaulu.

WAZO KUU.
Kuna maandamano na migomo,walimu na wauguzi wanagoma.Migomo hiyo inatokana
na kutowajibika kwa viongozi ambao wana nia ya kujifaidi.

ONYESHO LA PILI
TENDO LA KWANZA.
Ni ofisini mwa Mzee Majoka, anaongea kwa simu Chopi anapoingia.Ashua anafika
kumwona Majoka,anataka kumkumbatia lakini Ashua anakataa.Majoka anakasirika
Ashua anapomwita mzee na kufurahi anapomwita Ngao, jina lake la ujana.
Ashua amefika kuomba msaada lakini Majoka anamtaka kimapenzi.Anajaribu kumbusu
lakiniAshua anakwepa.Majoka anamshawishi, anajisifu na kujilinganisha na Lyonga wa
uswahilini na Samsoni Myaudi.
Majoka anasema kuwa soko limefungwa kwa sababu ya uchafu, anatenga eneo hilo ili
kujenga hoteli ya kifahari.Wanasagamoyo wanalitegemea soko hilo kula, kuvaa na
kuendesha maisha yao.
Ashua anakataa kazi ya ualimu anayopewa Majoka and Mahoka academy, angekuwa
mwalimu mkuu katika shule mojawapo ya kifahari.

WAZO KUU.
Viongozi hunyanyasa wachochole ili kujifaidi, Majoka anafunga soko na kunyakua eneo
hilo kujijengea hoteli ya kifahari.Anataka kutumia mali na mamlaka yake kumteka Ashua
kimapenzi.

TENDO LA PILI.
Husda anamkabili Ashua kwa hasira, anamtusi kuwa kidudumtu, shetani wa udaku na
mwenye kuwinda wanaume wa watu.Wanaangushana na Ashua kuzabwa makofi.
Sauti ya kenga inamjia Majoka akilini kuwa soko lifungwe ili kulipiza kisasi kwa Sudi na
Ashua, kisha Ashua aitwe ofisini na Husda wakabiliane.
Mwango na Chopi wanawachukua Ashua na Husda ndani, agizo linatolewa Husda
atolewe ndani baada ya nusu saa.
............................................................


Below is the document preview. Purchase to access the complete document.

  • 317_0.jpg
  • 317_1.jpg
........

This is the end of this document preview. Buy to download the complete document.


More Resources


More Content By 6965


View all resources