Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Eleza sifa za nahau

Eleza sifa za nahau.

Answers


KELVIN
a) Nahau huundwa kwa lugha ya mkato iliyo na ujumbe mzito wa mafumbo k.m kidudu mtu-mfitini.
b) Nahau mbili au zaidi zinaweza kuwa na maana moja k.m jamvi la wageni/bao la mkahawani –kahaba.
c) Nahau moja inaweza kuwa na maana zaidi ya moja k.m kushika mguu-kuomba radhi /kutoa shukrani kupiga mbio.
d) Maneno katika nahau hupoteza sifa zake za kawaida na kuchukua maana nyingine iliyo tofauti kabisa .k.m kula chumvi –kuwa mzee.
e) Nahau huundwa kwa maneno mawili au zaidi kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa-danganya.
f) Bega kwa bega pamoja.
g) Nahau huweza kuundwa kwa mitindo mbalimbali au kwa maneno ya kategoria mbambali k.m
i. Kitenzi na nomino –piga chuku, andika meza
ii. Kitenzi na kitezi-kufa kupona,pata shika
iii. Kitenzi na kielezi –jikaza kisabuni, kufa kikondoo
iv. Noino na nomino-askari kanzu, domo kaya
v. Nomino na kitenzi-mguu haumshiki, damu kumkauka.
vi. Nomino na vivumishi –nyoat njema, ndege mbaya
kalvinspartan answered the question on October 24, 2017 at 14:34

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions