Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Eleza sifa tano za kimsingi zinazotambulisha sajili ya siasa

Eleza sifa tano za kimsingi zinazotambulisha sajili ya siasa.

Answers


Peter
Sifa za sajili ya siasa
(a) Matumizi ya msamiati wa kisiasa kama vile uchaguzi, kura, mbunge, sheria n.k
(b) Msamiati wa heshima- Nawaomba wananchi watukufu mnipigie kura
(c) Matumizi ya lugha iliyojaa hadi mfano, mkinichagua nitawajengea hospitali, shule zaidi na kuwapa kazi vijana wote
(d) Wanasiasa wengine huharibu lugha katika uteuzi wao wa msamiati. Mfano hii uchaguzi mpaka mtu aangushwe
(e) Kurudiwarudiwa kwa kauli kama njia ya kusisitiza jambo lisemwalo. Mfano, Mimi nimeleta maendeleo, nikaleta maji, nikaleta stima, nikaleta sipitali…mwataka nani mwingine kweli?
(f) Mazungumzo huendelezwa kwa nafsi ya kwanza. Mfano, Mimi nimewatetea bungeni, nikaungana nanyi hapa, tukashikana mikono mpaka tukapata haki yetu
(g) Matumizi ya maswali ya balagha mfano, Msiponipa kura zenu, nani mwingine?
(h) Kuna matumizi ya mbinu ya tawasifu mfano, Mimi ndiye kiongozi aliyezindua mradi huo, nikamwalika kiongozi wa kitaifa akaja kuufungua kwa sababu anaheshimu kazi yangu nzuri
Musyoxx answered the question on July 25, 2018 at 13:57

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions