Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Eleza kinaya katika Kigogo

Eleza kinaya katika Kigogo.

Answers


Noah
KINAYA KATIKA TAMTHILIA KIGOGO
1.Boza anadai kuwa kulipa kodi ni kuchenga nchi na kujitegemea.Kauli hii ni Kinaya kwa vile kodiwanayolipa Wanasagamoyo haitumiki kujenga nchi kwa vyovyote vile.
2.Boza anamwambia Sudi kuwa wanatia doa kwa kila jambo nzuri. Ni Kinaya kwa vile hakuna jambo nzuri ambayo Majoka amefanya Sagamoyo.
3.Wanasagamoyo kusheherekea miaka sitini ya uhuru ni kinaya kwani hakuna maendeleo Sagamoyo.
4.Boza anadai kuwa kinyago chake chapendeza na kufanana na shujaa Marara Bin Ngao, ni kinaya kwa kuwa kinyago hicho hakifanani na shujaa huyo.
5.Majoka kudai kuwa takataka za soko zitaaribu sifa nzuri za jimbo la Sagamoyo,ni kinaya kwa vile hakuna sifa nzuri Sagamoyo.
Kibet Koina answered the question on December 28, 2018 at 17:11

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions