Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

USHAIRI Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata: KIBARUWA: Abdilatif Abdalla Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa! Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa Kwenye shamba hilo kubwa sasa...

USHAIRI
Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata:
KIBARUWA: Abdilatif Abdalla

Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!
Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa
Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa
Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa
Ndipo mte ukatipuza!

Buni hiyo itakaangwa buni hiyo itapondwapondwa
Buni hiyo itasagwa na buni hiyo itafyondwafyondwa
Bali itabaki nyeusi kama ngozi yangu Kibaruwa
Waulize ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
Iulize na mito kwa furaha maji itiririkao
Uulize na upepo mkali kwa ghadhabu uvumao-.

Viulize: Ni nani araukaye na mapema kuzitema mbuga na kuzilaza?
Viulize: Ni nani akweaye minazi tangu kuchapo hadi lingiapo giza?
Viulize: Ni nani abebeshwaye mizigo hadi maungo yakageuka shaza?
Halfuye hana faida moja apatay wala malipo yanayotosheleza-
Isipokuwa kusundugwa na kutupiwa matambara na vyakula viliyooza?
Viulize: Ni nani huyo ni nani!

Viulize: Ni nani aliyemaye mashamba na kuyapoliliya?
Na mimea kochokocho ikajaa kwa uzito ikajinamiya?
Hatimaye nani atajirikaye mali yakammiminikiya
Akatoa na kitambi kama mja mzito wa miezi tisiya
Na akaongeza magari na wanawake kutoka na kuingiya?
Viulize: Ni nani huyo nani

Na hao ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
Nayo hiyo mito kwa furaha maji itirikao
Na huo upepo mkali wenye ghadhabu uvumao
Vyote hivyo vitatu vitakujibu kawa umoja wao
“Ni Kibaruwa Manamba ndiye mtendaji hayo!”

a) Eleza dhamira ya shairi hili.
b) Kwa kutoa mifano, eleza aina mbili za idhini ya kishairi alizotumia mshairi
c) kwa kurejelea ubeti wa tatu taja na ueleze tamathali ya usemi na mbinu ya kimuundo mshairi aliyoitumia

Answers


Kavungya
(a) Maisha ya wafanyakazi na vibarua shambani ni duni na ilhali wanaofaidika
ni wengine

(b)(i) Tabdila- mvuwa, kibarua, tisiya
(ii) Lahaja – mte, kutipuza, mtilizi
(iii) Mazida- tisiya
(iv) Inkisari – ikijinamiya, lingiapo
(v) Kuboronga sarufi – uuliza na upepo

(c)(i) Tamathali za usemi
(ii) Tahishishi/ uhuishi – ndege watambuizao, upepo uvumao kwa ghadhabu, mito
itiririkayo kwa furaha
(iii) Taswira – maji itiririkao, upepo mkali wa ghadhabu uvumao
(iv) Takriri/ uradidi- waulize, iulize, uulize
Kavungya answered the question on June 29, 2019 at 07:10

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions