Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

"Huu ni ukoloni mamboleo"

      

Mstahiki Meya
"Huu ni ukoloni mamboleo"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza umuhimu wa msemewa katika tamthilia hii.
(c) Jadili namna ukoloni mamboleo unavyojitokeza katika tamthilia.

  

Answers


sharon
(a) Muktadha.
(i) Mnenaji ni Siki.
(ii) Mnenewa ni Meya.
(iii) Wakiwa nyumbani kwa Meya.
(iv) Siki alikuwa ameenda kumwona Meya nyumbani mwake ili kumjulisha kuhusu matatizo ya wanacheneo.
(b) Msemewa ni Meya.
(i) Meya ni kielelezo cha viongozi wabadhirifu.
Anatumia pesa za baraza ovyo ovyo. Anaagiza vileo kutoka Urusi.
(ii) Meya anawakilisha viongozi dhalimu katika jamii.
Anawalipa wafanyikazi mishahara duni.
(iii) Meya ni kielelezo cha viongozi wabinafsi
Anajali maslahi yake na familia yake. Anajipatia vipande vinane vya ardhi.
(iv) Meya anawakilisha viongozi fisadi. Anajinyakulia vipande vya ardhi ya umma ili kujitajirisha.
(v) Meya ni kielelezo cha viongozi dikteta. Anafanya mambo kulingana na maoni na mawazo yake tu.
(c) Ukoloni mamboleo.
(i) Mapendeleo: Meya anaidhinisha nyongeza ya mishahara kwa madiwani na walinda usalama huku akipuuza nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi wa Cheneo.
(ii) Udikteta: Meya analazimisha mambo aidha hatambui mchango wa wanacheneo.
(iii) Ubadhirifu: Anapanga kuwapokea mameya wageni kwa kuwaandalia karamu kubwa.
(iv) Udhalimu: Meya anawalipa wafanyikazi mishahara duni. Anawatisha kuwa, wanaogoma watafutwa kazi.
(v) Unyanyasaji: Meya anatumia vyombo vya dola kuwanyamazisha wanacheneo.
(vi) Ufisadi: Meya anashirikiana na Bili na madiwani kuuza fimbo ya meya ambayo ni kitambulisho cha umeya.
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 10:32


Next: If 25.0cm3 of 0.1 M H2SO4 solution neutralized a solution containing 1.06g of sodium carbonate in 250cm3 of solution, calculate the molarity and volume of...
Previous: Explain why a hole in a ship near the bottom is more dangerous than the one near the top

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions