
(a) (i) Msemaji ni Meya
(ii) Msemewa ni Tatu
(iii) Wako ofisini ma Meya.
(iv) tatu alikuwa ameginga wazo la wao kuiipwa vizuri na kuonyesha tofauti ya usafiri kwa waajiri a a watoto wao na wafanyakazi wengine.
(b)
- Ni mwenye tamaa. Anaidbinisha nvongeza za mishara kwa madiwani iii yeye pia afaidike.
- Ni mwongo. Anadanganya kuwa wameagiza dawa kumbe hall sivyo.
- Ni mwenye mapuuza. Anapoambiwa na Siki kuwa kitoto kimemfia Siki tnkononi anasema huyo ni mmoja tu, Cheneo ma watu wengi.
- Ni fisadi. Alinyakua viwanja vinane vya umma. Akampa Bili Vinnie.
- Ni katili anapoambiwa kuhusu kifo cha kitoto hajali asema huyo ni mmoja.
- Ni mbadhirifu. Anatumia pesa za umma ovyo. Kuagiza mvinyo na divai, kutoka ng‘ambo. Nvongeza za mishahara kiholela na kadhalika.
- Ni mwenye majisifu. Anajisifia cheo chake nautajiri waka.
- Ni mwizi. Alishirkiana na Bili. Diwani I, Diwani II kupanga njama ya kuiba na kuuza fimbo ya meya.
(c)
(i) Medi ako na mgao si sawa na wengine.
(ii) Beka kuongezea wakubwa hula kwanza na wao kupigania makombo.
(iii) Tatu anaongezea kuwa wanashindwa kuiipia watoto wao karo na pia wanakosa kumudu gbarama ya matibabu.
sharon kalunda answered the question on October 3, 2019 at 06:49
-
Pana jambo ninatukiya, kwangu hilo ni muhali,
(Solved)
SIPENDI KUCHEKA
Pana jambo ninatukiya, kwangu hilo ni muhali,
Kitenda naona haya, kujishusha yangu hali
Sipendi unipe hidaya, sipendi kutenda hili
Sipendi mimi kucheka
Sipendi mimi kucheka, kuchekea mawi
Sipendi na ya dhihaka, kwangu nyemi hiwi
Sipendi kwa hakika, mwovu kistawika
Halafuye nikacheka!
Masikini akiteswa
Yatima akinyanyaswa
Mnyonge naye akinyonywa
Sipendi hata ikiwa
Unazo nguvu najuwa
Ni hili sitatekezwa
Mbona lakini nicheke, kwayo furaha?
Na wewe ukajiweke, uli na siha?
Na yatima ali pwek.e, wa anahaha?
Amenyimwa haki yake, hanayo raha!
Na moyo wangu ucheke, kwa ha ha, ha!
Kucheka kwa kucheka Mimi katu sitacheka.
MASWALI
a) Shairi hili ni la aina gani? Thibitisha.
b) Taj a sababu zinazomfanya mshairi asitake kucheka.
c) Chambua umbo la shairi hili kwa kuzingatia ubeti wa mwisho.
d) Tambua nafsineni na nafsinenewa katika shairi hili.
e) Tambua toni ya shairi hili.
f) Fafanua uhuru wa mshairi katika shairi hili.
g) Andika ubeti wa pili kwa lugha tutumbi.
h) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi
i) Mawi
ii) Nyemi
Date posted:
October 3, 2019
.
Answers (1)
-
Eleza hali ya shaka ya mambo inavyojitokeza katika hadithi ya shaka ya mambo.
(Solved)
“Shaka ya Mambo” (Farouk Topan)
Eleza hali ya shaka ya mambo inavyojitokeza katika hadithi ya shaka ya mambo.
Date posted:
October 3, 2019
.
Answers (1)
-
Eleza jinsi wanacheneo walivyotatua shida zinazowakumba.
(Solved)
Mstahiki Meya
Eleza jinsi wanacheneo walivyotatua shida zinazowakumba.
Date posted:
October 3, 2019
.
Answers (1)
-
"Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi."
(Solved)
Mstahiki Meya
"Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Anayeambiwa alisema nini baada ya kuambiwa haya?
c) Thibitisha kuwa wanacheneo walipanda pojo.
Date posted:
October 3, 2019
.
Answers (1)
-
Taja aina nne za hadithi.
(Solved)
Taja aina nne za hadithi.
Date posted:
October 3, 2019
.
Answers (1)
-
Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii.
(Solved)
Kidagaa kimemwozea
Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii.
Date posted:
October 3, 2019
.
Answers (1)
-
Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.
(Solved)
Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
"Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …"
(Solved)
Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.
"Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …"
a) Eleza muktadha wa maneno haya.
b) Eleza umuhimu wa mrejelewa katika dondoo hili kwenye riwaya.
c) Eleza maisha ya msemaji yalivyokuwa kwa mujibu wa Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
"Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"
(Solved)
Damu nyeusi na hadithi zingine
"Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili.
c) Huku ukitoa mifano, thibitisha maudhui sita ambayo yamejitokeza katika hadithi ya Damu Nyeusi na wanayoyaendeleza.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
"Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."
(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Ni nini sifa za mvuto zinazowaleta pamoja mzungumzaji na mzungumziwa.
c) Tambua na ufafanue mbinu inayotumika katika dondoo.
d) Kwa mifano mwafaka fafanua tanzia hiyo inayorejelewa katika dondoo.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya.
(Solved)
Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya.
(a) Jazanda
(b) Uzungumzi nafsia
(c) Majazi
(d) Methali
(e) Taharuki
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.
(Solved)
Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine
(Solved)
Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine
(i) Mke wangu
(ii) Damu Nyeusi
(iii) Tazamana na Mauti
(iv) Mizizi na matawi
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
"Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
(Solved)
"Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Jadili.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,
(Solved)
Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali.
SIKUJUA!
1. Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,
Zisingenidhuru pembe, ngeu kuniandama,
Samli ni lembelembe, na minofu ya minyama.
2. Kama ningefuga mbuzi, na kondoo kundi zima,
Ningewajengea zizi, na maziwa nikakama,
Ningewachuna na ngozi, kutengenezea ngoma.
3. Kama ningefuga bata, nao kuku kwa ujima,
Chakula siyo matata, ni machicha na mtama,
Mayai ningeyapata, na kitoweo kizima.
4. Kumbe nimefuga punda, mashuzi ndio heshima,
Ni ukaidi na inda, mateke kurusha nyuma,
Nyama limekuwa nunda, mfugaji humuuma.
Kiitikio
Sikujua wa kufuga, mnyama mwenye faida
SHAIRI B
Afrika na Watu Wake
Mimi ninaona mgonjwa
Bado amelala kitandani.
Kama hatutamtoa miiba iliyobaki
Mgonjwa hataweka miguu yake chini
Ili kutembea bila ya kujiegemeza.
Miiba iliyomo ndani mwetu lazima
Pia iondolewe upesi kabla haijaingia
Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi.
Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma
Halafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi.
Lakini kuitoa miiba hii
Tunahitaji macho makali
Mikono isiyotetemeka
Moyo usio na huruma
Na kuona miiba ilipoingilia.
MASWALI
(a) Onyesha jinsi ujumbe unaopatikana katika ubeti wa nne wa Shairi A na Shairi la B unavyokatisha tamaa.
(b) Eleza maana ya mshororo huu kama unavyojitokeza kwenye ubeti wa pili wa shairi B.
Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma.
(c) Linganua sifa za kimuundo ukizingatia ubeti wa pili wa Shairi A na Shairi B.
(d) Ukizingatia Mshororo wa kwanza kwenye ubeti wa pili wa Shairi A, onyesha jinsi Mshairi alivyotumia kibali chake.
(e) Onyesha sifa moja ambayo inadhihirika kwenye shairi la B na ambayo hutawala tungo za aina hii.
(f) Nafsi neni amedhihirisha toni gani kwenye shairi A?
(g) Taja nafsi mbili nenwa kwenye shairi la B.
(h) Andika ubeti wa mwisho wa shairi B kwa lugha ya nadhari.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
(Solved)
SABUNI YA ROHO
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia,
Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima.
Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
Sura zao ‗mefufua, wanazuru kila njanja,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
Watazame mayatima, kwao kumekua duni,
Webebe waliokuwa, wainue walio chini,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Umevunja usuhuba, familia zazozana,
Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.
(Solved)
Mstahiki Meya
Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.
(Solved)
Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
"………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"
(Solved)
Damu Nveusi na Hadithi nyingine
"………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Thibitisha ufaafu wa anwani ya hadithi hii.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
"Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."
(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake .
(b) Eleza tamathali mbili zilizotumika katika dondoo hili.
(c) Eleza aina za kiu na njaa zilizomkumba mrejelewa wa kwanza.
(d) Mrejelewa wa pili alishindwa mtihani wa maisha. Jadili.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)