Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Zingatia picha ifuatayo kisha ujibu maswali.

      

Zingatia picha ifuatayo kisha ujibu maswali.
pic31020191638.png
(a) Tambua kipera cha fasihi simulizi kinachowakilishwa na muktadha wa picha hii.
(b) Toa sababu mbili za jawabu lako katika swali la (a).
(c) Jadili sifa zozote tano zinazotambulisha kipera hiki.
(d) Jadili udhaifu wa kipera hiki katika jamii ya kisasa.

  

Answers


sharon
(a) Kipera cha miviga.
(b) Sababu mbili za jawabu lako katika swali (a)
- Ni miviga/sherehe ya tohara.
- Kuna ngariba.
- Kuna anayepashwa tohara.
- Kuna wadhamini wa wanaotahiriwa.
- Kuna wachezaji wa ngoma/nyimbo.
- Wachezaji wana maleba maalum.
- Kuna wanaoshuhudia sherehe hii wanajoni. Za kwanza
(c) Jadili sifa zozote tano zinazotambulisha kipera hiki.
- Hufanyika mahali maalum kwa kutegemea aina ya sherehe.
- Huhusisha matendo au uigaji tofauti.
- Wahusika huwa na mavazi maalum km tohara, arusi.
- Vifaa maalum hutumika kama mgwisho, njuga, kisu nk.
- Hutegemea/hutofautiana kulingana na jamii.
- Aghalabu huambatana na uimbaji na hata ngoma mbalimbali kulingana na maudhui ya sherehe.
- Mara nyingi huwa na viongozi maalum.
- Huandamana na utoaji wa nasaha tofauti. Za kwanza
(d)
Udhaifu wa kipera hiki.
- Baadhi ya miviga huhatarisha maisha na afya ya wanajamii km. tohara kwa wasichana, kurithi mke wa mtu aliyeaga.
- Baadhi ya miviga hukinzana na malengo ya kitaifa km. kutia unyagoni kwa lazima ni ukuikaji wa haki za kibindamu.
- Hujaza watu hofu km. utoaji kafara ya binadamu, kufukuza pepo na mizuka.
- Baadhi ya miviga huhusisha ushirikina km. Mazishini – waweza kuzua uhasama.
- Baadhi ya mivigha hugharimu pesa nyingi/mali nyingi km. Maombolezo.
sharon kalunda answered the question on October 3, 2019 at 13:52


Next: "Wema wako umeniua kabisa………Nina jishtaki mwenyewe kila siku kwa miaka na miaka".
Previous: Kuna mfanano mkubwa kati ya ulumbi na hotuba. Thibitisha.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions