Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Jibu maswali yote kwenye nafasi zilizoachwa wazi. Mawasiliano ni neno ambalo asili yake ni wasili. Wasili lina maana ya kufika kwa mtu, kitu, au jambo fulani baada...

      

Jibu maswali yote kwenye nafasi zilizoachwa wazi.
Mawasiliano ni neno ambalo asili yake ni wasili. Wasili lina maana ya kufika kwa mtu, kitu, au
jambo fulani baada ya mwendo au safari. Kwa hivyo kuwasiliana kuna maana watu, kitu au
mambo kufikiana kutoka mahali.
Katika siku za jadi mawasiliano yalikuwepo lakini ya shida. Hata hivyo, watu waliwasiliana kwa
kutumia moshi, ngomezi au kupiga mbiu. Mbinu hizi za jadi zilitumiwa baina ya vijiji ili
kujulisha wanakijiji jambo la dharura au kuwajulisha jambo lingine lolote. Mbiu ilitumika kwa
jambo la dharura. Njia za kusafirisha mizigo zilikuwa haba. Baadhi ya watu walitumia wanyama,
kama fahali au farasi kukokotea mizigo yuao.
Siku hizi mawasiliano yamepanuka sana. Mawasiliano ya kisasa yanahusisha simu, mtandao,
televisheni na wavuti. Mawasiliano ya kisasa yamefanya ulimwengu wa kisasa kuwa kijiji kimoja
kikubwa.
Kwa kuzingatia maudhui haya, vyombo au njia kama redio, simu, waraka, ndege, meli, motokaa
na wavuti vimepewa jina la vyombo vya mawasiliano. Hivyo basi yafaa tutathmini ni vipi
vyombo au njia hizi hufanya kazi ya kuwasiliana na huwasilisha nini. Vyombo hivi vinaweza
kuelezwa chini ya vichwa vitatu; usafiri, mazungumzo na picha. Vyombo mathalan baiskeli,
ndege, meli na magari hufanya kazi ya kuwasafirisha watu kutoka janibu moja hadi nyingine.
Watu wanaposafiri huwa wanasafirisha mali yao. Bidhaa kama kahawa, vyuma na mizigo
mingine husafirishwa kwa meli, ndege na magari kupitia majini, hewani au barabarani.
Bandari, viwanja vya ndege na barabara zimeimarishwa ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo.
Anayesafirisha bidhaa fulani na wakati huo anatakikana kukusanya nyingine, inamlazimisha
asiambatane na bidhaa hizo lakini ahakikishe zimewasili alikozikusudia. Hivyo basi njia nyingine
ya mawasiliano ilivumbuliwa.
Njia hii ambayo ni mazungumzo hutumia vifaa kama barua, simu, barua pepe na kipepesi.
Mtumiaji ataandika ujumbe na kuutuma kupitia shirika la posta au mashirika mengine ama
mtandao. Yamkini ilihitajika kuweza kujibizana na kuulizana kati ya watu hao wawili ndipo simu
ilipovumbuliwa na kumwezesha mtu kuzungumza na mwingine akiwa mbali sana. Watu
huzungumza na kufahamiana. Ilipohitaji mtu kukiona kitu anachozungumzia ndipo ilibidi kuunda
vifaa vya kuonyesha picha kama vile televisheni.
Ilikuwa fahari kubwa sana kwa Wakenya kuwasiliana na nchi ya Ghana wakati wa michuano ya
mpira ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika. Wakenya waliweza kuiona michezo hiyo moja
kwa moja ingawa kijiografia Kenya na nchi hiyo zina majira tofauti.
Mawasiliano tuliyotaja ni vyombo vya ufundi vilivyoundwa lakini kunayo maswasiliano ya ana
kwa ana. Mwalimu na mwanafunzi darasani huwasiliana kutumia midomo, mikono, macho,
kichwa na ishara nyinginezo. Wanapofanya hivyo huwa wanaelewana.
Ndege kama kuku akihisi adui hufanya ishara au mlio fulani wa kutahadharisha viranga wakek
katika michezo. Mwamuzi huwasiliana na wachezaji labda kwa kutumia firimbi au kipenga,
kengelel au ishara za mkono. Kengele pia hutumiwa shuleni ili kuonyesha kukamilika kwa
kipindi au kuhitajika mahali pengine.
Kwa muhtasari, mawasiliano hutumia chochote ilimradi ujumbe utokao kwa mtu, kitu au mahali
fulani ufike panapotarajiwa.

MASWALI:
(i) Taja anwani faafu ya kifungo hiki.

(ii) Vyombo vya mawasiliano vimeleta manufaa gani katika maisha ya watu?

(iii) Mawasiliano yameelezwa katika vipenge vitatu. Vitaje.

(iv) Andika visawe vya:
(a) Televisheni –
(b) Waraka –

(v) Nini maana ya:
(a) Ana kwa Ana –
(b) Ulimwengu umekuwa kijiji kimoja kikubwa –

  

Answers


Kavungya
(i) Taja anwani faafu ya kifungo hiki.
Mawasiliano

(ii) Vyombo vya mawasiliano vimeleta manufaa gani katika maisha ya watu?
- Kuwasafirisha watu na bidhaa kwa upesi
- Kuwasilisha ujumbe/taarifa/habari
- Kuona matukio yakiwepo mbali
- Kuimarisha uchumi na maendeleo

(iii) Mawasiliano yameelezwa katika vipenge vitatu. Vitaje.
- Usafiri
- Mazungumzo
- Picha

(iv) Andika visawe vya:
(a) Televisheni –Runinga
(b) Waraka – Barua

(v) Nini maana ya:
(a) Ana kwa Ana – Hali ya kuwa mnaonana
(b) Ulimwengu umekuwa kijiji kimoja kikubwa – Mawasiliano yamerahisishwa sana ulimwenguni
Kavungya answered the question on November 21, 2022 at 12:44


Next: Read the excerpt below and answer the questions that follow ...
Previous: Taja vigezo vitatu vinavyotumika kuainisha konsonati.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Taja majukumu matano ya fasihi simulizi.(Solved)

    Taja majukumu matano ya fasihi simulizi.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Fasihi simulizi ni nini?(Solved)

    Fasihi simulizi ni nini?

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi ifuatayo. Nyumba hiyo itafunguliwa.(Solved)

    Kanusha sentensi ifuatayo.
    Nyumba hiyo itafunguliwa.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Tambulisha maneno mbalimbali katika sentensi zifuatazo. i) Mwanafunzi mvumilivu alisoma vizuri. ii) Yule ameongea maneno mengi.(Solved)

    Tambulisha maneno mbalimbali katika sentensi zifuatazo.
    i) Mwanafunzi mvumilivu alisoma vizuri.

    ii) Yule ameongea maneno mengi.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Sentensi zifuatazo ziko katika nyakati / hali gani? a) Otieno hula samaki kila siku b) Yeye anaandika tu kitabu(Solved)

    Sentensi zifuatazo ziko katika nyakati / hali gani?
    a) Otieno hula samaki kila siku

    b) Yeye anaandika tu kitabu

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Andika sentensi zifuatazo kwa wingi. i) Ukuta ambao ulianguka ni huu. ii) Mwanagenzi yule amepita mtihani vizuri.(Solved)

    Andika sentensi zifuatazo kwa wingi.
    i) Ukuta ambao ulianguka ni huu.

    ii) Mwanagenzi yule amepita mtihani vizuri.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Tenganisha neno lifuatalo katika viambiu vyake mbalimbali. Aliyempigia(Solved)

    Tenganisha neno lifuatalo katika viambiu vyake mbalimbali.
    Aliyempigia

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Sauti mwambatano ni nini?(Solved)

    Sauti mwambatano ni nini?

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Toa mifano miwili ya sauti za nazali/ving’ong’o.(Solved)

    Toa mifano miwili ya sauti za nazali/ving’ong’o.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Andika konsonanti tatu ambazo ni vipasuo.(Solved)

    Andika konsonanti tatu ambazo ni vipasuo.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Taja aina mbili za konsonanti.(Solved)

    Taja aina mbili za konsonanti.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Viungo ambavyo hutumika katika utamkaji wa sauti huitwa aje?(Solved)

    Viungo ambavyo hutumika katika utamkaji wa sauti huitwa aje?

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Kiungo ambacho hutetemeka na kutoa sauti huitwaje?(Solved)

    Kiungo ambacho hutetemeka na kutoa sauti huitwaje?

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Taja: i) Irabu za mbele. ii) Irabu ya kati iii) Irabu za nyuma(Solved)

    Taja:
    i) Irabu za mbele.

    ii) Irabu ya kati

    iii) Irabu za nyuma

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Taja aina mbili kuu za sauti katika kiswahili.(Solved)

    Taja aina mbili kuu za sauti katika kiswahili.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Soma Ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali. Beata alikuwa msichana mrembo lakini alikuwa haambiliki, hasemezeki . Fauka ya hayo, alikuwa na tamaa isiyo na kifani.(Solved)

    Soma Ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali.
    Beata alikuwa msichana mrembo lakini alikuwa haambiliki, hasemezeki . Fauka ya hayo, alikuwa na tamaa
    isiyo na kifani.
    Alipokuwa katika shule ya msingi, walimu na wazazi walimfunza umuhimu wa kuwa na maadili.
    Isitoshe, alifunzwa masomo vyema lakini akili yake ilikuwa butu. Akawa haingizi chochote cha maana ila
    uchafu wa fikira. Nyumbani nako hakuzingatia maonyo. Alikuwa hatulii.
    Wakati fulani wa krismasi, Beata alipomaliza tu shule ya msingi, alikutana na mwanamume mmoja
    mliliwa na wasichana wengi; mtajika kwa mali na jina lake ni Mshikaji . Beata akadanganywa akadanganyika.
    Akatorokea kwa huyu Mshikaji ambaye alikuwa ameshawataliki wake wawili tayari. Akawa mke mlezi. Ikabidi
    awalee watoto waliobaki na baba yao baada ya mamazao kutanzuka. Beata mwanzoni aliona raha, ingawa
    alikereka kuitwa mama kabla hata ya kumpokea mwana wake mwenyewe. Aliwabeza waliokuwepo awali na
    akajiona kuwa yeye ndiye mchukuzi bora. Akadharau kuwa pakacha likivuja, nafuu huwa ni kwa yule
    mchukuzi. Aliwaona wenzake kama maua yaliyonyauka na lake ndilo kwanza linaonana na jua.
    Muda si muda, akajikuta ana wana watatu kwa kipindi kifupi. Mumewe naye hakutulia na mambo ya
    nje. Akaimarisha nyendo zake za kiguu na njia, akipochoka, akiingia garini na kuikata mitaa. Beata aende wapi?
    Alifungika nyumbani ndi ndi Akamlea mwana huyu na yule; wake na wale wa kambo. Vijisenenesenene
    vikazidi. Lakini akajaribu kuvumilia akidhani atazila mbivu, wapi! Alipoligema ilibidi alinywe. Siku zikaja na
    kupita. Beata akajuta kwa kutosikiliza wakuu na kumkimbilia mtu ambaye hata hakuwa anamuelewa vizuri.
    Pesa na raha alizokuwa amezikimbilia akawa anazisikia kama hadithi ndotoni. Kwao nako kukawa hakurudiki.
    Beata akawa majamzito tena kama kawaida akawa anaenda kliniki za wajawazito. Alipopimwa ikabainika
    kuwa ana ukimwi. Mtoto alipozaliwa akafariki. Yule mumewe akaanza kumnyanyasa.
    Baada ya miaka mitatu, bwana Mshikaji, aliyekuwa akijitapa kwa unene na mali, akaanza kupotelewa na
    kiriba chake cha tumbo. Homa za hapa na pale zikaanza kumyemelea. Vipelevipele vikamsambaa mwilini. Hata
    akamsingizia Beata kuwa ni yeye aliyeuleta huo ukimwi Ilikuwa ni wazi kuwa msambazaji alikuwa ni yeye
    bwana. Waliokuwa pembe za chaki waliujua ukweli ulipokuwa . Baadhi ya vidosho wake walishaanza
    kupukutika kama majani yafanyavyo wakati wa mapukutiko. Isitoshe, wengine walikuwa hoi vitandani wakiwa
    hawajui waingiao wala watokao. Ugonjwa wa kamata ulishawakamata. Mwisho akawa ni wa kulazwa na
    kutoka hospitali hizi na zile. Pesa zikawaishia, wakawa waya. Beata akawa hana budi kuviuguza vidonda
    ndugu vyake na vya mumewe. Hatimaye, mumewe akabwagwa chini na ukimwi na akafafo!
    Si ndugu si marafiki, hawakumuelewa Beata. Waliamuona kama pweza aliyejipalia makaa makubwa ya
    moto makali. Ada za shule zikawa ni shida. Huruma ikwaingia watu. Watu wakasema. “Lisilobudi hutendwa.”
    Wakaubeba mzigo kwa hiari yao. Wakawafanyia watoto harambee ya ada na peza za matibabu. Mwishowe
    Beata naye aliaga dunia akiwa bado mbichi kwa umri. Hata miaka ishirini alikuwa bado hajafikisha. Watoto
    ikabidi walelewe na wahisani.
    Hapo walimwengu wakaja kutambua ukweli kwamba, uzuri si hoja hoja ni tabia. Isitoshe mtu
    akikimbiliwa na kila mtu, ukimwi hatauepuka. Mtu akiupata, hufa. Anadidimiza watu wengi pamoja na familia
    yake. Jamii ilifunzwa pia kuwa unene si hoja. Hata watu vibonge huweza kuleta ukimwi. Basi, jamii hiyo
    ikaazimia kuwa wao hawatakuwa watumwa wa tabia iletayo ukimwi. Walitambua kuwa ukimwi unarudisha
    nyuma maendeleo na kuipakaza jamii mizigo isiyo tarajiwa. Nasi tutahadhari kabla ya hatari

    1. Andika kichwa kifaacho kisa hiki
    2. Ni jambo gani lililomkera Beata baada ya kuolewa na Mshikaji?
    3. Toa sababu moja iliyomfanya Beata kuwadharau wenzake waliomtangulia kwa mshikaji?
    4. Ni kwa nini Beata alianza kujuta?
    5. Toa sababu moja kuonysha kuwa Mshikaji ndiye aliyeusambza ukimwi
    6. Kulingana na kifungu hiki taja hasara zinazoletwa na ukimwi.
    7. Kwa nini walimu na wazazi hawangelaumiwa kwa yale yaliyompata Beata?
    8. Andika maana ya:
    i) butu
    ii) Kope zikawa si zake
    iii) Akiwa bado mbichi
    iv) Kuzanzuka
    v) Vijisenensenene.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Tambua kielezi katika sentensi ifuatayo. Kijana mkorofi ameadhibiwa vibaya(Solved)

    Tambua kielezi katika sentensi ifuatayo.
    Kijana mkorofi ameadhibiwa vibaya

    Date posted: August 17, 2020.  Answers (1)

  • Tambua kivumishi katika sentensi ifuatayo. Mwanafunzi mdogo amezungumza taratibu.(Solved)

    Tambua kivumishi katika sentensi ifuatayo.
    Mwanafunzi mdogo amezungumza taratibu.

    Date posted: August 17, 2020.  Answers (1)

  • Vita vina athari nyingi katika maisha ya binadamu, dhibitisha ukweli wa kauli hii ukiangazia riwaya ya chozi la heri.(Solved)

    Athari za vita katika riwaya ya Chozi la heri.

    Date posted: June 15, 2020.  Answers (1)

  • "Maisha yangu yalijaa shubiri tangu utotoni." Rejelea Chozi la heri.(Solved)

    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili.

    Date posted: June 15, 2020.  Answers (1)