Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Huku ukizingatia riwaya ya kidagaa kimemwozea na ken walibora eleza umuhimu wa wahusika wafuatao Matuko Weye, Mtemi Nasaba Bora, Lowela

Huku ukizingatia riwaya ya kidagaa kimemwozea na ken walibora eleza umuhimu wa wahusika wafuatao Matuko Weye, Mtemi Nasaba Bora, Lowela

Answers


ESTHER
Umuhimu Wa Matuko Weye:
1. Ni kielelezo cha dhuluma walizopitia na wanazopitia waliopigania uhuru. Ni kinaya kuwa japo alihusika katika ukombozi, zawadi yake ni umaskini na wehu. Waliokula matunda ya uhuru hawakuchoka.
2. Kupitia kwake tunatambua changamoto za wakombozi. Hawana uhuru wa kujieleza, wanafungwa seli duni bila makosa na kuachiliwa hata bila kupelekwa kortini.
3.Ametumika kuwadhihaki wanatomoko. Japo ni mwehu anaelewa sokomoko haiongozwi vyema na tofauti na wananchi wenye akili razini, hanyamazi.
MTEMI NASABA BORA
1. kielelezo cha ukoloni mambo-leo ambapo mabwana weusi walinyakua uongozi na kuwadhulumu waafrika wenzao huku wakiua ndoto ya uhuru halisi
2. Kielelezo cha uozo unaoendelezwa na viongozi wa kiafrika. Ukware, ufisadi, udikteta Ubabe-dume n.k. Ndio maana kwake kumejaa uchafu - jazanda ya uozo
3. Kielelezo cha hatima ya viongozi dhalimu. Uongozi wa kiimla hauna budi kufika mwisho.

LOWELA
1. Kielelezo cha changamoto za elimu ya msichana. Mapenzi baina ya Wanafunzi na wazee Unaosababisha mimba za mapema na kuacha Shule.
2. Kielelezo cha uozo unaoendelezwa na vijana katika harakati za kutafuta raha na anasa kama vile kutupa Mtoto asiye na hatia

ESTHER STEVE answered the question on December 12, 2017 at 19:30

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions