Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Fafanua sifa za Kenga kama zinavyojitokeza wazi katika tamthilia ya kigogo.

Fafanua sifa za Kenga kama zinavyojitokeza wazi katika tamthilia ya kigogo.

Answers


Francis
Kenga ni mshauri mkuu wa Majoka.
- Kenga in kibaraka, wakati takwimu zinaonyesha asilimia sitini ya wana Sagamoyo wako tayari kumpigia Tunu kura iwapo atasimama, anamtia Majoka moyo kwamba hayo ni maneno yametiwa chumvi.

- Kenga ni fisadi, pamoja na mzee Majoka wanahodhi mali ya umma. Anamegewa sehemu ya soko la Chapakazi.

- Kenga ni mshauri mbaya, anamshauri Majoka walifunge soko ili kulipiza kisasi kwa Sudi na kumnasa Ashua.

- Kenga ana taasubi ya kiume, haamini mwanamke anaweza kuwa shujaa Uk. 10. Vile vile anamuuliza Sudi kuwa amelishwa kiapo na huyo hawara wake akiashiria Tunu Uk. 12

- Kenga ni msaliti, anawasaliti wananchi wa Sagamoyo kwa kuhodhi mali ya umma badala ya kuwajibika katika kazi aliyopewa na wananchi.

- Kenga ni katili, anamwambia Majoka kwamba polisi wanafanya kazi yao vizuri kwa kuwajeruhi waandamanaji, pia anapanga njama na wahuni.
franco crick answered the question on January 31, 2018 at 16:56

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions