Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Jadili dhima ya fasihi katika jamii

Jadili dhima ya fasihi katika jamii

Answers


Andrew
Fasihi huelimisha-
jamii hufunzwa na kufahamisha masuala kadhaa kama mazingira.
Fasihi huburudisha jamii-
jamii huburudishwa kupitia vipera vya fasihi vinavyolenga aghalabu kutumbuiza, kufurahisha na kusisimua.
Fasihi hukuza lugha-
sanaa hii hukuza matumizi na ujuzi wa watumiaji wa lugha husika na kusababisha ukuaji wa lugha hiyo.
Fasihi hudumisha maadili-
jamii hupat kujulishwa, huonywa na huelekezwa kufuata mwelekeo na mienendo inayokubalika katika jamii husika.
Fasihi hukuza utangamano katika jamii-
kupitia sanaa kama nyimbo, vichekesho na miviga, watu huunganishwa na kuchangia kuwepo kwa amani na uelewano.
Fasihi hukuza kumbukizi-
sanaa hii huwezesha watu katika jamii kukumbuka hali na mambo ya kale na hivyo kukuza uwezo wao wa kukumbuka.
Fasihi huhifadhi tamaduni-
kila jamii ina tamaduni husika ambayo huhifadhiwa kwa njia ya sanaa za fasihi.
Fasihi hutambulisha jamii-
kila jamii ina mitindo yake ya kuwasilisha sanaa za fasihi ambayo huwa ni kitambulisho cha jamii hiyo.
Fasihi hukuza uwezo wa kufikiri-
vipera kama ngano na vitendawili huchochea jamii kufikiri ili kupata jawabu.
Andreaz answered the question on February 9, 2018 at 10:00

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions