Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

1. Eleza maana ya istilahi hii: Usanifishaji 2. Eleza mambo manne yaliyochangia maenezi ya kiswahili kabla ya uhuru.

1. Eleza maana ya istilahi hii: Usanifishaji
2. Eleza mambo manne yaliyochangia maenezi ya kiswahili kabla ya uhuru.

Answers


ESTHER
1) Usanifishaji ni uamuzi wa kuchagua lugha moja au mojawapo ya lahaja za lugha na kuifanyia marekebisho ya kimatamshi, kisarufi kimaana na kimaandishi ili iweze kutumika kirasmi.
- Kusanifisha lugha ni kuifanya ikubalike na kutumiwa kwa njia iliyosawa na kila mtu.

2) a) Misafara ya wafanyibiashara baina ya pwani na bara.
b) Utawala wa wakoloni hasa wajerumani waliotumia kiswahili kuwasiliana na watawaliwa.
c) Juhudi za usambazaji wa dini ya Kiislamu na kikristo.
d) Juhudi za serikali za kikoloni kutoa sera zilizokinufaisha kiswahili mfano kamati y a usanifishaji - 1930
e) Matumizi ya lugha ya kiswahili katika vyombo vya habari.
f) Kuibuka kwa waandishi wa kisanii kwa lugha ya kiswahili Sheraban Bin Roberts. (4 x 2 = 8

ESTHER STEVE answered the question on April 28, 2018 at 15:47

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions