Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

(a) Nini maana ya kufa kwa lugha. (b) Eleza sababu zozote tano zinazochangia kufa kwa lugha

(a) Nini maana ya kufa kwa lugha.
(b) Eleza sababu zozote tano zinazochangia kufa kwa lugha.
(c) Taja aina tatu za makosa ya lugha.

Answers


ESTHER
(a) Kukoma / kuacha matumizi ya lugha fulani katika eneo lugha fulani.
(b) (i) Uchache wa wazungumzaji – idadi ya watu wanaozungumza lugha fulani wanapopungua,
lugha hiyo inakabiliwa na tisho la kufifia
(ii) Hadhi – Lugha ambazo halienziwi na wanajamii au kuchukuliwa kuwa hazina hadhi
huishia kufa.
(iii) Kuhama kwa watu – watu wanapohama kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Lugha zao huathiriwa na wengine husahau lugha zao kabisa.
(iv) Kutoungwa mkono na taasisi mbalimbali – Lugha yoyote isipoungwa mkono na taasisi
kama elimu, dini na vyombo vya habari hukabiliwa na tisho la kufa.
(v) Athari za elimu – watoto wanapofunzwa lugha zingine katika shule, lugha zao
za mama huathiirka.
(vi) Sababu za kisiasa.

(c ) (i) Makosa ya kimantiki
(ii) Makosa ya kimuundo
(iii) Makosa ya kimatamshi
ESTHER STEVE answered the question on April 28, 2018 at 15:49

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions