Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Vitanza ndimi huwa na dhima gani katika jamii

Vitanza ndimi huwa na dhima gani katika jamii.

Answers


KELVIN
a) Vitanza ndimi hukuza matamshi bora mtu anapotamka kwa haraka na kwa usahihi, hutia makali stadi zake za kimatamshi. Kupitia hali hii uzoefu wa kutamka vyema hujengwa.
b) Hukuza uwezo wa kufikiri kwa haraka, baadhi ya vitanza ndimi hutatanisha kuwaza haraka ili kuteua neno sahihi la kutamka.
c) Kuburudisha, kimsingi vitanza ndimi vilinuiwa kuibua ucheshi na kuchangamsha hadhira.
d) Hukuza ubunifu, anayebuni vitanza ndimi anahitaji kuwa na ujuzi mpana wa lugha na ubunifu ili kuteua maneno yanayokaribiana kimatamshi na kimaana.
e) Hukuza lugha, vitanza ndimi vilivyobuniwa katika vipindi mbalimbali huhifadhiwa na kupitishwa kwa vizazi vijavyo kama malighafi katika kipera cha vitanza ndimi.
f) Huhifadhi utamaduni na kuurithisha, maarifa ya kipera cha vitanza ndimi yasingehifadhiwa na kurithishwa kama vipera vingine vya fasihi simulizi, tusingevisoma leo.
g) Ni kitambulisho cha jamii, vitanza ndimi huakisi mazoea ya jamii husika kila jamii ina vitanza ndimi vyake mahususi.
h) Hujenga uhusiano bora wa kirafiki, ucheshi unaoibuliwa na vitanza ndimi hujenga uhusiano bora miongoni mwa washiriki.

kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 12:34

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions