Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Eleza uhusiano uliopo baina ya mafumbo na chemsha bongo

Eleza uhusiano uliopo baina ya mafumbo na chemsha bongo.

Answers


KELVIN
Mafumbo ni kauli zenye maana iliyojificha, mafumbo hutumia lugha fiche au ya kiistiari pamoja na tamathali nyingine za usemi. Humtaka anayeambiwa kudadisi mazingira yake na kufikiria ili kupata maana, mafumbo huchemsha bongo za wale wanaoshiriki katika kuyafumbua ingawa vitendawili ni aina za fumbo tunadai kwamba mafumbo kwa kawaida ni semi ndefu kuliko vitendawili.
Kuna mafumbo yaitwayo chemshabongo, chemshabongo ni maswali ambayo humtaka mtu kutumia akili na ujuzi kuyajibu. Maswali mengi ya aina hii ni ya kimapokeo, mengine hubuniwa na msemaji ili kukidhi mahitaji ya hadhira mahususi. Baadhi ya chemshabongo kwa hakika ni hesabu tu nyingine hutolewa kwa mraba unahitaji kujazwa.
kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 12:35

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions