Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

‘Shogake dada ana ndevu’ Safia Eleza sifa za wahusika wafuatao. i) Mwalimu Musi ii) Jairo iii) Sera iv) Mke wa Jairo

‘Shogake dada ana ndevu’ Safia
Eleza sifa za wahusika wafuatao.
i) Mwalimu Musi
ii) Jairo
iii) Sera
iv) Mke wa Jairo

Answers


Kavungya
i) Mwalimu Musi
• Ni karimu
• anampa Jairo zawadi alizopewa katika sherehe ya kumuaga.
• Anakubali mke wa Jairo na watoto wake waishi kwake.
• Alimpeleka mtoto wa Jairo shule na kumnunulia kitabu.
• Ana utu
• Anasisitiza watu waliofika katika sherehe ya kumuaga na hawakufaulu maishani wapewe fursa ya kutoa hotuba.
• Hakukasirishwa na yaliyosemwa na Jairo na alimpa zawadi zake zote.
• Ana utu kwani alikubali kuishi na mke wa Jairo kwake.
• Aliwafunza wanafunzi wake vizuri na mwishowe wakawa watu wenye vyeo katika jamii.
• Ni msiri.
• Alipompatia Jairo zawadi zake hakumwambia mkewe.
• Alikuwa tayari kukosolewa.

ii) Jairo
• Alikuwa mwanafunzi wa mwalimu mstaafu
• Alikuwa mtu ovyo
• Hali yake ya umaskini ilimfanya amlaumu mwalimu kwa kumpa tumaini za uongo.
• Hakufanya vizuri masomoni.
• Alishiriki ulevi.
• Aliamini pombe ilimpa raha ya kuishi.
• Alikosa uwajibikaji ndiposa akampeleka mkewe na watoto wake kwa mwalimu.
• Alikuwa mchoyo.
• Alisema hakuelewa ni kwa nini mwalimu alimshauri asilewe.
• Aliishi maisha ya dhiki. Hakuwa na viatu vya kuvaa.
• Alidai kuwa mwalimu Mosi angemwambia mapema kuwa hakuwa na akili ya kufaulu mtihani.
• Uraibu wa pombe uliharibu akili zake akawa kama mwenda wazimu.

iii) Sera
• Mke wa Mwalimu
• Ana utu na upendo
• Alisihi mumewe akubali waishi pamoja na mke wa Jairo na watoto wake.
• Aliishi na mumewe kwa upendo na amani.
• Anashirikiana na mke wa Jairo kufanya kazi za nyumbani, shambani na kutafuta kuni.
• Ana huruma na upendo.
• Anamtunza mumewe anapougua ugonjwa wa saratani

iv) Mke wa Jairo
• Ni mvumilivu
• Amejaa adha nyingi za maisha kutulia kwa Jairo.
• Ni mtiifu
• Anatii amri za mume wake
• Anapopelekwa kwa mwalimu kama zawadi anakataa kurudi kwake nyumbani.
• Alikuwa tayari kuwa mke wa pili au mafanyikazi wa mwalimu.
• Anashirikiana na mke wa mwalimu kufanya kazi za nyumbani , shambani na kutafuta kuni.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:12

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions