Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Anwani ya hadithi TUMBO LISILOSHIBA ni mwafaka kwa hadithi hii. Fafanua

Anwani ya hadithi TUMBO LISILOSHIBA ni mwafaka kwa hadithi hii. Fafanua

Answers


Kavungya
Tumbo lisiloshiba ni hadithi iliyopewa anwani inayosadifu yanayotendeka hadithini kwa sababu:
• Jiji licha ya kwamba lina majengo mengi bado linahitaji kupanuliwa ndio sababu ardhi ya wanamadongoporomoka inapangwa kunyakuliwa.
• Jitu linalokuja mkahawani kwa mzee Mago lina tumbo lisiloshiba, linaagiza lipewe vyakula vyote vilivyokuwa vimeandaliwa wateja wengine, pia linakunywa chupa kadhaa za soda.
• Jitu linaapa na kuahidi kuwa lingehitaji chakula maradufu zaidi siku iliyofuata. Jambo lililowashangaza kina mzee Mago na wenzake.
• Jitu lilikuja siku iliyofuata kunyakua ardhi ya madongoporomoka. Hili linaashiria kuwa tumbo halishibi si chakula tu mbali rasilimali za raia kama ardhi.
o Tumbo lisiloshiba linasimamia wenye mamlaka ambao hawatosheki. Wanamiliki mali nyingi lakini bado wanahitaji kumiliki kidogo walicho nacho wanyonge
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:20

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions