Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Liandike ubeti ufuatao katika kiswahili sanifu Kisha itaje lahaja aliyotumia mtunzi.

Liandike ubeti ufuatao katika kiswahili sanifu Kisha itaje lahaja aliyotumia mtunzi.
"Malimwengu yote yawatiile
na dunia yao iwaokele
wachenenda zitea zao zilele
mato matumizi wayatumbiye"
Jawabu;
"Ulimwengu wote uwatii
na dunia yao iwaokoe
Wataenda Vita vyao vile macho yaliyofumbwa wayafumbue"
Hii ni lahaja ya kiamu.

(b) Kwa kutoa mifano kutoka ubeti huo na kwingineko ,zibainishe sifa Tisa zinazotofautisha lahaja hiyo na kiswahili sanifu.

Answers


Faith
Kiamu ilikuwa lahaja ya usomi na ushairi katika Karne zilizopita.Tofauti za kifonolojia Kati ya kiamu na kiswahili ni:
Kiambishi (-le) hutumiwa Kama kiishio cha kitenzi katika baadhi ya maneno ya mashairi yaliyoandikwa zamani kwa kiamu.
Kiamu - Kiswahili sanifu
Iwaokele - iwaokoe
Sauti (v) na (vy) hutamkwa Kama (z) kwa mfano
Zao - vyao
Vyombo - zombo
Sauti (ch) hutamkwa Kama (t) kwa mfano
Wachenenda - wataenda
Kicheko- kiteko
Macho - mato
Sauti (nj) hutamkwa Kama (nd) kwa mfano
Njia - ndia
Nje - nde

Titany answered the question on December 6, 2021 at 09:31

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions