Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Eleza ni kwa nini lahaja ya kiunguja ilichaguliwa kwa msingi wa kusanifisha lugha ya kiswahili na wala sio kimvita au kiamu

Eleza ni kwa nini lahaja ya kiunguja ilichaguliwa kwa msingi wa kusanifisha lugha ya kiswahili na wala sio kimvita au kiamu

Answers


Faith
• Lahaja ya kiunguja ilikuwa imeenea sana kuliko lahaja ya kimvita ambayo ilikuwa ikitumiwa katika sehemu za Mombasa pekee.
• Lahaja ya kiunguja ilikuwa rahisi sana kufahamika kuliko kimvita kwani matamshi yake yaliwatatanisha watu wengi.
• Lahaja ya kiunguja ilikuwa inaweza kupokea msamiati toka lahaja au lugha nyingine kwa urahisi kuliko kimvita au kiamu.
• Lahaja ya kiunguja ilikuwa inaweza kubadilika kulingana na mazingira na wakati isivyo lahaja ya kiamu na kimvita.
• Lahaja ya kiunguja ilikuwa na historia ndefu ya kimatumizi na ilikuwa imefanyiwq utafiti sana na Ludwig kraph kuliko lahaja ya kimvita.
• Lahaja ya kimvita ilikuwa na uwezo wa kutambulisha matumizi sanifu na yasiyosanifu.

Titany answered the question on December 6, 2021 at 09:50

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions