Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Eleza ni kwa nini lugha ya Kiswahili ilisanifishwa wakati wa ukoloni

Eleza ni kwa nini lugha ya Kiswahili ilisanifishwa wakati wa ukoloni

Answers


Faith
Lugha ya Kiswahili ilisanifishwa ili kukidhi mahitaji ya kidini na elimu kama ifuatavyo.
• Kuwepo kwa lahaja nyingi za kiswahili,wingi huu wa lahaja ulitatiza sana mawasiliano katika shughuli za kibiashara ,kielimu n.k ambazo zilihitaji kuelewa kwa lahaja moja ili kueleweka na watu wote.
• Kulikuwa na hati tofauti zilizotumiwa kuandika kiswahili.Mwanzoni kulikuwa na hati ya kiarabu na baadaye kirumi.Ni kutokana na hali hii ndipo kulikuwa na tofauti katika kuendeleza maneno kukawa na haja ya kutafuta namna moja ya kuendeleza.
• Kulikuwa na haja ya kutafsiri maandishi ya biblia takatifu na kutakani kwa lugha moja ili watu waweze kusoma na kupata wokovu.
• Kulikuwa na haja ya kuwasilisha injili na dini kwa lugha moja ili kuepuka kutoeleweka kwa maandishi na injili.
• Kulikuwa na haja ya kutumia lahaja moja shuleni kwa kufundishia ili kuleta uelewano baina ya walimu na wanafunzi.

Titany answered the question on December 6, 2021 at 09:51

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions