Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine, jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi. (a) Tulipokutana Tena (b) Mapenzi ya...

      

Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine, jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi.
(a) Tulipokutana Tena
(b) Mapenzi ya Kifaurongo
(c) Shogake Dada ana Ndevu
(d) Mame Bakari
(e) Mtihani wa Maisha

  

Answers


Francis
(a) Tulipokutana Tena
? Wazazi wa Bogoa - ni walezi wema ingawa ni maskini hawataki Bogoa alelewe na wazazi wengine.
? Bi. Sinai anamfanya Bogoa mtumwa.
? Bi. Sinai anamnyima Bogoa uhuru wa kucheza na watoto wengine.
? Babake Bogoa anamtisha Bogoa kwa mkwaju.
? Mamake Bogoa alimpenda Bogoa - anamtayarisha asubuhi kabla ya kuondoka.

(b) Mapenzi ya Kifaurongo
? Wazazi wa Penina wamewajibika katika kumlea Penina. Wanampa fedha za kutosha kila wiki.
? Licha ya kuwa maskini wazazi wa Dennis wanajizatiti sana kumsomesha hadi chuo kikuu.
? Wazazi wa Dennis walijitaabisha ili kumtunza.
? Wazazi wa Penina wanalipa kodi yake.

(c) Shogake Dada ana Ndevu
? Wanawapeleka wanao shuleni. k.m wazaziwe Safia wanampa nafasi ya kusoma.
? Wazazi hawa pia wana mapuuza. Wanamwamini mwanao kupita kiasi.
? Wazazi wake Safia wanampa kazi nyumbani k.m kufagia.
? Mamake Safia anamjulia hali anapoona mabadiliko.
? Habiba Chechei hawajamlea mtoto wao Mkadi vizuri.

(d) Mame Bakari
? Babake Sara ni mkali sana, Sara anapobakwa anaogopa kumwambia kuwa ana uja uzito.
? Baadaye anabadilika wa kuwa mpole, anamfariji.
? Mamake Sara ni dhaifu, hawezi kumsaidia Sara.
? Wazazi wa Sara wanalipa gharama zote za uja uzito wake.
? Wazazi wa Sara wanafika hospitalini kumjulia hali.

(e) Mtihani wa Maisha
? Wazazi wa Samueli wanajinyima ili kuwasomesha watoto wao.
? Babake Samueli anauza ng’ombe ili kumsomesha Samueli.
? Mamake Samueli anatumiwa kuonyesha mapenzi ya mzazi ni ya kudumu.
? Babake Samueli anatumiwa kuonyesha kutamauka kwa wazazi.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 11:22


Next: ‘Kusema kweli lakini hata mimi sikuwa na nadhari katika kumpenda msichana huyu ... Nilimpenda kufa! Lakini! Kwao bure tu!’ (Shibe Inatumaliza) (a) Eleza dondoo. (b) Taja mtindo...
Previous: “Akanyangapo chini ardhi inatetemeka...Amejitia hamnazo. Kabwela kama mimi nina faida gani? (Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Fafanua mbinu tatu za...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions