Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Akanyangapo chini ardhi inatetemeka...Amejitia hamnazo. Kabwela kama mimi nina faida gani? (Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Fafanua mbinu tatu za...

      

“Akanyangapo chini ardhi inatetemeka...Amejitia hamnazo. Kabwela kama mimi nina faida gani? (Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine)
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
(c) Eleza madhila kumi yaliyompata ‘kabwela’.

  

Answers


Francis
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
? Haya ni mawazo ya Dennis.
? Anamrejelea Shakila.
? Mahali - katika afisi ya Shirika la kuchapisha magazeti.
? Tukio - ni baada ya kumwona mamake Shakila (pandikizi la mama) akipita huku akisubiri kufanya mahojiano.

(b) Fafanua mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
? Chuku - akanyagapo chini, ardhi inatetemeka.
? Taswira - picha ya ardhi ikitetemeka
? Nahau - kujitia hamnazo

(c) Eleza madhila kumi yaliyompata ‘kabwela’.
? Anakosa kazi katika shirika la magazeti
? Kuachwa na Penina
? Kukejeliwa na Daktari Mabonga
? Hapewi pesa za masurufu na wazazi
? Kushindwa kujibu maswali wakati wa mahojiano – anaaibika
? Njaa – anaamua kupika uji
? Hana nguo za kisasa/ simu/tarakilishi n.k.
? Anasumbuka kiakili kwa sababu ya hali /asili/umaskini
? Kufukuzwa na Penina
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 11:25


Next: Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine, jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi. (a) Tulipokutana Tena (b) Mapenzi ya...
Previous: “Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto. Rudi, rudi kwa Mola wako.” (a) Fafanua muktadha wa maneno haya. (b) Eleza hulka tatu za msemewa. (c) Taja maovu anayoyafanya msemewa.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions