-
Ni nini maana ya neno kirai ?
Date posted:
October 7, 2019
-
Nyambua vitenzi hivi kulingna na kauli ya kutendua na kutendama
Date posted:
October 7, 2019
-
Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mishale.
Hakimu alimwadhibu kinyama.
Date posted:
October 7, 2019
-
Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo na ueleze ni shamirisho ya aina gani?
Wazazi wanalipia watoto karo kwa hundi;
Date posted:
October 7, 2019
-
Ngeli ya LI-YA hujumulisha nomino za vitu vya aina mbalimbali. Toa mifano minne
ambayo ni tofauti na uelezee
Date posted:
October 7, 2019
-
Tambulisha aina za vitenzi vilivyotumika katika asentensi hizi
(i) Kazi hii ni nzuri.
(ii) Mazingira yamekuwa yakihifadhiwa.
Date posted:
October 7, 2019
-
Tunga sentensi ya neno moja yenye mofimu zifuatazo
(i) Nafsi ya tatu umoja
(ii) Wakati uliopita
(iii) ‘O’ rejeshi
(iv) kitendwa
(v) mzizi
(vi) kiishio
Date posted:
October 7, 2019
-
Sauti zifuatazo hutamkiwa wapi?
(i) /f/
(ii) /v/
Date posted:
October 7, 2019
-
Tunga sentensi moja moja kuonyesha tofauti kati ya vitate vifuatavyo:
(i) Pamba
(ii) Bamba
Date posted:
October 7, 2019
-
Andika kwa umoja
Uovu waliotuonyesha hautasahaulika
Date posted:
October 7, 2019
-
Andika sentensi ifuatayo katika udogo:
Mbwa mdogo amekanyagwa na gari.
Date posted:
October 7, 2019
-
Sahihisha sentensi ifuatayo:
Ukienda mle pao atakuweko
Date posted:
October 7, 2019
-
Tambua kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi hii :-
Chakula ambacho ni muhimu, huweza kujenga au kobomoa mwili wako.
Date posted:
October 7, 2019
-
Unda nomino kutokana na vitenzi hivi:-
(i) Chapa
(ii) Goma
Date posted:
October 7, 2019
-
Onyesha shamirisho kipozi, kitondo na ala katika sentensi ifuatayo:
Kamau alimlimia mamake shamba kwa trekta
Date posted:
October 7, 2019
-
Nyambua kitenzi ‘oa’ katika hali tatu zifuatazo: tendewa, tendwa, tendea
Date posted:
October 7, 2019
-
Ainisha viambishi katika neno lifuatalo :-
Kilichokikata
Date posted:
October 7, 2019
-
Bainisha ngeli za nomino hizi :-
(i) Kisu
(ii) Nyavu
(iii) Chai
Date posted:
October 7, 2019
-
Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vielelezo vya vishale:
Kiarie ni mwanafunzi mtiifu
Date posted:
October 7, 2019
-
Kanusha sentensi hizi kwa wingi:-
(i) Mtoto huenda shuleni kila siku
(ii) Mwalimu amemfunza mwanafunzi vizuri
Date posted:
October 7, 2019
-
Andika sentensi ifuatayo kwa usemi halisi:
Mwalimu alipoingia darasani aliuliza kitabu chake kilipokuwa.
Date posted:
October 7, 2019
-
Onyesha maneno yaliyokopwa toka lugha za kigeni na kuswahilishwa kwa kuyaongezea
irabu kama Bint (Kiarabu) – Binti
Toa mifano minne
Date posted:
October 7, 2019
-
Sauti hizi ni za aina gani na hutamkwa wapi?
(i) gh
(ii) j
Date posted:
October 7, 2019
-
Andika upya sentensi hii kwa kuandika kinyume cha kila neno lilipigwa mstari:-
Wifi alipovaa nguo na kusimama ajuza yule alikaa
Date posted:
October 7, 2019
-
Geuza sentensi hii hadi udogo:-
Nyoka yule mrefu alifukuzwa na watu wengi
Date posted:
October 7, 2019
-
Unda majina mawili mawili kutoka vitenzi hivi na utumie katika sentensi ili
kubainisha maana
(i) Safiri
(ii) Zaa
Date posted:
October 7, 2019
-
Tumia kivumishi kilichoko kwenye mabano kukamilisha sentensi:-
(i) Bibi yule alinunua gari ________________________(-pya)
(ii) Mti (-ingine) _______________________uliangushwa badala ya ule wa kwanza.
Date posted:
October 7, 2019
-
Tunga sentensi nne kuonyesha matumizi na maana nne za kijineno ’ki’
Date posted:
October 7, 2019
-
Sahihisha sentensi ifuatayo na uiweke katika wingi:-
Ningalifanya kazi ningekuwa tajiri
Date posted:
October 7, 2019
-
Kanusha sentensi hii:-
Tungewalaki kama tungejua watakuja
Date posted:
October 7, 2019