-
Andika maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii :-
Alimlilia mwanawe
Date posted:
October 7, 2019
-
Mti wa zambarau ni rahisi kukatwa ukiwa unatumia msumeno. (Anza Ni rahisi...)
Date posted:
October 7, 2019
-
Aliogopa kumwangalia simba aliyekula mzoga. (Tumia neno ‘Ogofya’ bila ya
kubadililsha ya sentensi:-)
Date posted:
October 7, 2019
-
Badilisha sentensi hizi hadi usemi wa taarifa:-
(i) “Nitarudi tu ikiwa mtakubali kuomba msamaha”. Juma alisema
(ii) “Elezeni vile mlivyokuja hapa na namna mtakavyokwenda.” Mwalimu mkuu alisema
Date posted:
October 7, 2019
-
Weka sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea:-
Mmea ambao unapandwa katika msimu wa masika unamea
Date posted:
October 7, 2019
-
Andika sentensi ifuatayo bila kutumia “amba”:-
Jitu ambalo linatusumbua sharti liadhibiwe vikali
Date posted:
October 7, 2019
-
Eleza maana ya semi hizi :
(i) Kunja jamvi
(ii) Piga kambi
Date posted:
October 7, 2019
-
Taja mianzo mitatu tofauti ya ngeli ya U-ZI
Date posted:
October 7, 2019
-
Tunga sentensi mbili kubainisha maana tofauti ya maneno yafuatayo:-
(i) Kuna
(ii) guna
Date posted:
October 7, 2019
-
Bainisha matumizi ya maneno yaliyopigwa mstari
(i) Mbio hizi hazitakufikisha mbali
(ii) Mwambie Abedi asifanye mbio kuhusu hiyo kazi.
Date posted:
October 7, 2019
-
Andika katika hali ya ukubwa
Mwanamke huyu amezaa watoto wanne.
Date posted:
October 7, 2019
-
Unda nomino mbili mbili kutokana na vitenzi vifuatavyo:-
(i) abudu
(ii) fisidi
Date posted:
October 7, 2019
-
Changanua kwa kutumia mishale
‘Mimi sikumwona wala Mwenda hakumwona’
Date posted:
October 7, 2019
-
‘Msipokuwa wenye bidii hamtayapata mafanikio maishani.’ Yakinisha katika umoja
Date posted:
October 7, 2019
-
Tumia ‘‘O’’ rejeshi ya kati
Lisemwalo silo liwalo
Date posted:
October 7, 2019
-
Tunga sentensi ambayo ina aina za maneno uliyopewa:-
N + V + V + T
Date posted:
October 7, 2019
-
Andika kwa usemi wa taarifa:-
“Wasichana wakielimishwa wataweza kuwa bora kuliko wavulana,” Naibu wa Chansela
wa chuo Kikuu aliwaambia mahafala.
Date posted:
October 7, 2019
-
Badili sentensi zifuatazo katika kauli iliyoonyeshwa kwenye mabano
(i) Si vizuri mwanafunzi kumwibia mwenzake pesa (Kutendeana)
(ii) Mpishi aliharibu mchuzi huu kwa kuongeza chumvi nyingi. (tendeka)
Date posted:
October 7, 2019
-
Ng’oa kisiki hiki haraka askari akaamrisha mahabusu
(Andika kwa msemo halisi)
Date posted:
October 7, 2019
-
Taja sauti mbili ambazo hutamkwa nyuma ya ulimi kati ya hizi
/h/,/o/,/y/,/u/,/kh/,/g/,
Date posted:
October 7, 2019
-
Andika katika usemi wa taarifa :
“Karibu Rahma, tafadhali kaa,” Musa akasema . Ahsante, je, habari za hapa?’ Rahma aliuliza
Date posted:
October 7, 2019
-
Bainisha aina mbili za vishazi katika sentensi hii :-
Shamba lile kubwa litauzwa kesho
Date posted:
October 7, 2019
-
Tumia – ‘ako’ katika sentensi kama:
i) Kivumishi
ii) Kiwakilishi
iii) Kitenzi
Date posted:
October 7, 2019
-
Sahihisha:
i) Kila mwanafunzi alipewa ndazi na mayai moja
ii) Nipee huo mkoba nitoemo vitabu zangu
Date posted:
October 7, 2019
-
Andika udogo wa:
Magari yote yaliyobakia yatauzwa na mzee yule mwembamba
Date posted:
October 7, 2019
-
Taja sifa mbalimbali za sauti zifuatazo:
/Z/
/K/
Date posted:
October 7, 2019
-
Changanua sentensi ifuatayo ukitumia njia ya matawi :-
Amekuja kuwatembelea manusura waliopata ajali ya ndege
Date posted:
October 7, 2019
-
Sisi tunajua sheria ingawa tu wafisadi
Anza: Japo………….
Date posted:
October 7, 2019
-
Ainisha viambishi katika neno lifuatalo:
atakuajiri
Date posted:
October 7, 2019
-
Andika katika wingi
Meza ii hii ndiyo aliyotumia kulia
Date posted:
October 7, 2019