Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Questions and answers: Kiswahili

Ask, answer and revise exam-style questions across Kenyan subjects and professional courses.

Q&A Categories

Exams With Marking Schemes

2200 Questions    View: All Solved Unsolved

Search Results...
  • Tumia neno kitoto kama; i) kivumishi ii) kielezi

    Date posted: October 4, 2019
  • Taja na ueleze pingamizi zozote tano zinazokwamiza juhudi za kukuza Kiswahili

    Date posted: October 4, 2019
  • Changanua sentensi hii kwa kutumia kielelezo cha visanduku. Mzee aliyemdhulumu msichana yule ametiwa mbaroni tena.

    Date posted: October 4, 2019
  • Eleza juhudi zozote tano za serikali ya Kenya katika kukuza Kiswahili

    Date posted: October 4, 2019
  • Eleza matumizi ya "ku" katika sentensi hii. Kucheza kwake kulifurahisha wengi

    Date posted: October 4, 2019
  • Tunga sentensi sahihi ukitumia kitenzi — nywa katika kauli ya kutendesha

    Date posted: October 4, 2019
  • Yakinisha sentensi hii Mpishi asipokuwa mwangalifu chakula hakitaiva vizuri

    Date posted: October 4, 2019
  • Ainisha viwakilishi katika sentensi hii Usibanduke papa hapa

    Date posted: October 4, 2019
  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Uchumi wa soko huria ni hali ya kiuchumi ambapo itokeapo amali, shughuli na harakati zote za kiuchumi ghairi ya zile ambazo ni za lazima kwa serikali au dola kama ulinzi, sheria na mpangilio wa jamii huwa huria kwa watu binafsi. Msingi wa soko huria, sifa kuu ya utandawazi, ni kuibua na kudumisha mazingira na hali zinazochochea na kumruhusu mtu yeyote kuongozwa na hawaa, au matamanio ya kibiashara anayoyaona sawa pasi na hofu ya kuingilia na udhibiti wa serikali. Mazingira hayo yanawapa watu satua ya kufanya maamuzi kuhusu hatima yao ya kiuchumi, uamuzi kuhusu suala la ajira yao, matumizi ya mtaji kipato na harija zake, na uwekezaji mzima. Suala mojawapo linaloibuka kuhusiana na mfano wa soko huria ni kuweka mipaka bainifu na wazi baina ya amali na shughuli zinazohusishwa na serikali na zile ambazo huachwa huria kwa watu. Kwa mfano, inaaminiwa kuwa haki ya kuishi na kulindwa dhidi ya shambulizi, liwe la kijambazi au la kigaidi, ni ya kimsingi ambayo haiwezi kuhusishwa na uwezo wa kiuchumi wa mtu binafsi. Aidha huduma za kimsingi za afya nazo zinaingia katika kumbo hili. Ikiwa huduma hizi zitaachwa huria pana uwezekano mkubwa kuwa zitaishia kuwa istihaki ya wenye mtaji na kipato cha juu tu. Licha ya kuwepo kwa sheria au kanuni huria kutoka nyanja maalum, hutokea hali ambapo adhibiti wa kiserikali ni lazima. Hii hutokea pale ambapo ipo haja ya kuyalinda mazingira hasa kutokana na uchafuzi wa viwanda au tasnia. Aidha udhibiti huo ni lazima pale ambapo haki za watu wengine zinahusika: yaani ikiwa uhuru wa hata mtu mmoja unaadhirika kutokana na sera hizo pana haja ya kuingilia ili kuisawazisha hali yenyewe. (a) Andika kwa muhtasari maana ya uchumi wa soko huria kulingana na taarifa hii. (maneno 25-30) (b) Eleza mawazo makuu yanayojitokeza katika aya ya pili na ya tatu. (maneno 70-75)

    Date posted: October 4, 2019
  • Toa maana ya semi Shupaa mwili.

    Date posted: October 4, 2019
  • Taja dhamira ya sentensi ifuatayo Kimbia mbio ulete sahani

    Date posted: October 4, 2019
  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Vijana wa siku hizi hujifikiria kuwa wao ni bora kuliko wazee wao. Wao hujifikiria kuwa wameelimika zaidi, wana busara zaidi, wanauelewa ulimwengu vizuri zaidi na wanaweza kujiamulia hatima yao bila uongozi wa wazazi wao. Wazee kwa upande wao, hawakubali kabisa madai ya aina hiyo. Kwao ni maasi tu. Wanachojua wazee kwa hakika ni kuwa vijana wa siku hizi hawaajibiki kwa lolote, wamedekezwa mno na wanapenda sana nafsi zao. Kwa sababu hiyo, vijana wanahitaji uongozi na ushauri wa wazeee. Je, kuishi kwingi ni kuona mengi? Ingawa wazee wanafikiria wanajua mengi kwa sababu ya umri wao, vijana hupenda sana kukosoa fikira za wazee wao. Hawakubali imani na itikadi za wazee wao. Kwa mfano; vijana hupendelea mitindo ya mywele ambayo wazee wao hufikiria kuwa kichaa tu. Wazee husifiwa sana enzi zao. Husifia jinsi walivyolelewa kwa kuchapwa na kufanyishwa kazi zinazohitaji uvumilivu mkubwa kama vile kuchanja kuni, kufyeka misitu, kutayarisha mashamba, kuwinda na kadhalika. Kwa sababu ya malezi hayo, wazee husema wao walirithi nidhamu nzuri na ushujaa. Vijabna kwa upande wao hawaoni chochote cha kujivunia katika zama za wazee wao; wao hufikiria kuwa wazee wao walilelewa kwa ukatili kwa sababu zama zao zilikuwa enzi za giza, kabla ya majilio ya uungwana na ustaarabu wa kisasa. Wazee husifia kuwakumbusha vijana ule msemo mashuhuri wa wahenga usemao kuwa ‘mwacha mila ni mtumwa.’ Kwa maoni ya wazee, vijana wengi wamekuwa watumwa kwa sababu wao huonyesha kwa vitendo kuwa hawadhamini desturi za wazee wao. Ka mfano; vijana hawafuati miiko ya jadi, hawapendi kuhudhuria sherehe za kienyeji, kwa mfano sherehe za kutoa makafara. Vijana pia hawapendi ngoma za kitamaduni, na isitoshe vijana hawazionei fahari koo zao. Vijana hawakubali kuwa wao ni watumwa wa mtu yeyote. Mila wanazosifia wazeee wao si vitu vyenye umuhimu wowote kwa vijana. Kwa mfano; baadhi ya miiko ni kisayansi. Kuhusu ukoo, si vijana wengi wanaona umuhimu wake. Ukoo na kabila zilikuwa muhimu zamani wakati ambapo kulikuwa hakuna serikali, bima na hata kazi ya mtu binafsi. Mambo haya sasa ni kama masalia ya zamani ambayo yamepitwa na wakati. Je, vijana hupenda sana burudani na anasa tu kama wanavyodai wazee! Wazee wengi hufikiria kuwa vijana hupoteza muda wao mwingi kujitafutia anasa na burudani kwa mfano vijana wengi hurandaranda barabarani au mitaani wakisingizia kupunga hewa. Wengine huenda sinema na kuhudhuria dansi na karamu zisizo na manufaa. Vijana kwa upande wao hawaoni kinachowawasha wazee wao; pilipili wasioila yawashia nini? (i) Katika makala haya wazee wana malalamiko yapi kuhusu vijana? (maneno 50-60) (ii) Msemo unaosema “Mwacha mila ni mtumwa” unathibitishwa vipi katika maoni ya wazee katika makala haya? (maneno 15- 25)

    Date posted: October 4, 2019
  • Akifisha sentensi ifuatayo iii ilete dhana tatu tofauti; Fatuma Khamisi mjukuu wa Rashid na Rehema wametoroka shule

    Date posted: October 4, 2019
  • Andika sentensi hii katika hali ya umoja. Vilifi vivi hivi ndivyo vimekuwa vikitumiwa na meli zizi hizi kutia nanga bandarini.

    Date posted: October 4, 2019
  • Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa. “Michezo yetu ya mpira itang’oa nanga kesho,” mwalimu alimwambia mwanafunzi yule.

    Date posted: October 4, 2019
  • Eleza maana mbili zinazopatikana katika sentensi ifuatayo; Tafadhali niletee pia nichezee.

    Date posted: October 4, 2019
  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Kwa hali nyingine , tunaweza kusema kuwa uchafuzi wa mazingira ni uharibifu wa vile vitu vinavyowazunguka binadamu na wanyama maishani mwao. Kuna uchafuzi wa aina mbalimbali na kila uchafuzi humhusu binadamu kwa njia fulani. Maendeleo ya viwanda duniani ni sababu mojawapo ya uchafuzi wa hewa. Mitambo katika karakana huwa inatoa moshi mwingi wakati bidhaa zinapotengenezwa. Moshi husambaa eneo kubwa na kuchanganyika na hewa inayovutwa na binadamu. Uchafu hutupwa ovyo ovyo na kuwa hatari kwa afya ya binadamu. Maji machafu huweza kutiririkia mtoni, maziwani na hata baharini. Yale yanayotiririka mitoni na maziwani huchafua maji ambayo hutumiwa na watu wa eneo hilo kwa kunywa, kupika na kunywesha mifugo wao. Yale yanayotiririka baharini huwa ni hatari kwa samaki wanaotegemewa na binadamu kuwa kitoweo muruwa. Ongezeko la watu pia ni hali nyingine ya uchafuzi wa mazingira. Halaiki ya watu hufanya uharibifu wa misitu ya asili. Hii ni kwa sababu ya kutaka kuongeza ekari za mashamba. Hili husababisha mmomonyoko wa udongo ; hivyo basi kuiacha ardhi bila rutuba yoyote. Katika hali hii, kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa nchi nyingi duniani huzoroteshwa. ‘‘Maisha ya binadamu hutegemea kilimo kwa kila hali kwa hivyo kilimo kinapozoroteka hata uchumi nao huathirika. Kila uchao tunasikia kwamba nchi fulani imekabiliwa na njaa. Ufugaji wa wanyama wengi bila mpango maalum pia huharibu mazingira ya asili kama nyasi na vichaka. Watu wengi hufuga ng’ombe, mbuzi na kondoo. Kwa kuwa hawana mahali maalum pa kuwalisha, huzunguka nao huku na huko kutafuta nyasi na majani ya kuwalisha. Wanyama wanaotangishwatangishwa namna hiyo humaliza majani na nyasi zote na kuacha ardhi tupu ambayo hatimaye huyabisika kwa jua. Ardhi ya namna hii haishiki maji mvua inyeshapo. Nchi iliyoneemeka huweza kuwa jangwa lililo na chungu ya mchanga. Watu wanapoongezeka huko mashambani huwabidi wakate misitu ili waanzishe maskani mapyapamoja na mashamba yao. Miti hukatwa bila hadhari na mabiwi ya matawi pamoja na majani huchomwa moto. Jambo la kusikitisha ni kwamba miti hiyo inapokatwa hakuna mingine inayopandwa kuchukua mahali pake. Mahitaji ya binadamu ya kuendeleza njia za mawasiliano pia huzusha balaa nyingine. Barabara zinazidi kuongezeka na pia watu wanaozidi kuongezeka pamoja na mazao yao. Kwanza, barabara zinapotengenezwa misitu hukatwa mahali zinapopitia. Pili, wingi wa magari huzidi na baadhi ya hayo hutoa moshi unaoharibu hewa. Njia kadha wa kadha za kuzuia uharibifu wa mazingira zimependekezwa. Ingawa suluhisho timamuhalijafikiwa, Serikali nyingi duniani zimo katika harakati za kutafuta suluhisho la uchafuzi huo. Njia mojawapo ni kukomesha ujenzi wa viwanda katika miji mikuu na mahali palipo na watu wengi.Wenye viwanda pia wanahimizwa kufikiria jinsi ya kutupa takataka na maji machafu bila kudhuru afya ya binadamu. Watu wakizingatia suala la upangaji wa uzazi na kuwa na familia ndogo ndogo, idadi ya watu haitaongezeka kwa kasi kwa hivyo itakuwa hakuna haja ya kuanzisha makao mapya mara kwa mara. Serikali nyingi zimechukua jukumu la kuwaelimisha raia juu ya madhara yanayotokana na uharibifuwa mazingira. Raia wanahimizwa kupanda miti kwa wingi. Jitihada zinazofanywa kuzuia uchafuzi wa mazingira hukumbana na matatizo. Tatizo kubwa ni fedha za kuendeleza miradi inayopendekezwa. Shida nyingine ni kwamba juhudi zingine huwa zinamwingilia binadamu na mali yake. Maswali. (a) Fupisha aya za kwanza sita za taarifa uliyosoma (maneno 50-60) (b) Fupisha aya za mwisho tano kwa maneno 40-45

    Date posted: October 4, 2019
  • Kanusha sentensi ifuatayo; Angalimpata babu yangu angalimpeleka hospitalini.

    Date posted: October 4, 2019
  • Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mistari. Uchochole wa kijinsia umepigwa marufuku na kiongozi mwenye msimamo dhabiti mno.

    Date posted: October 4, 2019
  • Tunga sentensi yenye muundo ufuatao KN(N+S)+KT(T+E+E)

    Date posted: October 4, 2019
  • Iandike sentensi ifuatayo upya katika hali yakinishi. Hapo napo sipo nitakapo.

    Date posted: October 4, 2019
  • Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali kulingana na maagizo Imesemwa na kurudiwa tena kwamba, iwapo tuna maono ya kujiondoa katika umaskini wa kupindukia, ni lazima tukipe kilimo umuhimu. Zaidi ya wakenya milioni kumi wamo katika hatari ya kufa njaa katika maeneo mbali mbali kwa sasa kufuatia uhaba wa chakula nchini. Kiini kikubwa cha njaa hiyo ni mapuuza ya muda mrefu katika sekta ya kilimo. Imesahaulika kuwa karibu asilimia sabini na tano ya wakenya wanategemea kilimo kwa chakula na mapato ya kifedha kila siku. Kilimo hutoa karibu robo tatu ya nafasi za kazi kwa wananchi na pia huletea serikali karibu robo ya mapato yake kutokana na mauzo ya mazao katika mataifa ya nje. Wataalamu wa maswala ya zaraa wanaeleza kuwa pato la nchi linalotokana na kilimo huangamiza njaa mara nne zaidi ya mapato yanayotokana na shughuli nyinginezo za kiuchumi. Hiyo ni kwa sababu shughuli za kilimo hulenga kuzalisha vyakula moja kwa moja. Imebainika kuwa, katika mataifa mengi yanayostawi, asilimia sabini na tano ya wananchi huishi katika maeneo ya mashambani na idadi hii hutegemea kilimo kujimudu kimaisha ilhali hapa Kenya ni asilimia nne pekee ya bajeti inayowekezwa katika kilimo. Kwa wakati huo, ushuru unaotozwa bidhaa za kilimo katika maeneo haya umebainika kuwa mkubwa. Hii imepelekea uwekezaji katika kilimo kupungua na hivyo kuchangia kukithiri kwa baa la njaa. Wakati umewadia kwa serikali za Afrika na wapangaji wa masuala ya uchumi kuweka juhudi maradufu katika kushabikia kilimo ili kumaliza njaa na umaskini. Kuna haja ya kuwajulisha, kuwahimiza na kuwaelimisha wakulima wa mashamba madogo madogo kuhusu mihimili ya zaraa kama vile uzalishaji wa matunda na mboga, ufugaji wa ndege, samaki na ng’ombe mbali na kuweka mikakati ya kuanzisha nafasi za kazi katika sekta ya kilimo. Serikali itafikia lengo hili iwapo itaanza kufadhili kilimo, kupunguza gharama za pembejeo za kilimo, kuweka sera zinazodhibiti uuzaji na ununuzi wa vyakula hasa baina ya mataifa na kuongeza sehemu ya bajeti inayotengewa kilimo. Bila hilo hatutakuwa na lingine bali kukimbilia mataifa yaliyostawi kuomba misaada ili kuwanusuru raia wetu kutokana na ghadhabu ya njaa. (a) Fupisha aya mbili za mwanzo (maneno 50 -55) (b) Bila kubadili maana, fupisha aya mbili za mwisho (Maneno 55-60)

    Date posted: October 4, 2019
  • Mafuta yanayopatikana kwenye fukwe za bahari, moshi wa magari, takataka na bidhaa nyinginezo zinazotupwa hapa na hapa ni vichafuzi vya mazingira. Vichafuzihuadhiri afya zetu na kuathiri wanyama na mimea. Wanadamu wanayachafua mazingira yao kwa kila aina ya bidhaa mbaya za kikemikali zinazotoka viwandani mwa kawi / nguvu. Bidhaa hizo ni matokeo ya maisha ya siku hizi anayoishi binadamu. Licha ya ukweli huu, ni muhimu kujua kuwa uchafuzi wa mazingira haukuanza leo. Miaka na miaka iliyopita, viwanda vimekuwa vikitoa mawingu makubwa ya moshi yenye sumu. Hata hivyo, uchafuzi wa mazingira umeongeza mara dufu kutokana na kuongezeka kwa viwanda. Uchafuzi umesambaa ardhini, kwenye anga na majini. Msambao huu unapatikana katika pembe zote za ulimwengu wetu. Je, kuna aina zipi za uchafu? Kwanza, kuna uchafu wa hali ya anga. Huko juu angani kuna tabaka linalojulikana kama ozoni. Tabaka hili ni aina ya gesi ya oksijeni na linaunda kinga fulani dhidi ya miale ya jua. Miale hiyo ya jua huweza kusababisha saratani ya ngoziinapomfikia binadamu. Hata hivyo, uchafu wa mazingira unaelekea kuliathiri tabaka hili vilevile baadhi ya kemikali zinazotumiwa katikajokofu au kwenye mikebe ya marashi ya kupulizia na upakiaji bidhaa, huuharibifu ukanda huo.Uchafu mwingine ni uchafuzi wa kiajali. Uchafuzi huu hutokea bila binadamu kukusudia. Mfano mzuri ni meli inayovuja mafuta baharini. Mafuta haya huwaathiri na kuwaua wanyama wanaoishi baharini kama samaki na ndege na hata kuyaharibu mazingira yenyewe. Miji mikubwa hukumbwa na uchafuzi mwingine unaohusiana na kuwako kwa idadi kubwa ya magari. Magari haya hutoa moshiunaochanganya gesi ambazo huungana na nyingine zinazoletwa na viwanda vikubwa. Mchanganyiko huu unapoungana na maji , husababisha mvua ya asidi. Mvua hii huweza kuiua mimea , kuathiri majengo na hata kuwaua wanyama wa pori ambao huenda wakayatumia maji hayo. Magari hayo hutoa moshi uliochanganyika na madini aina ya risasi ambayo huweza kuathiri siyo tu mazingira bali pia mfumo wa akili wa binadamu. Uchafuzi mkubwa ni utupwaji ovyo wa takataka. Fauka ya hayo, watu hufukia ardhini takataka ambazo huweza kuwa na matokeo mabaya kwa sababu ya kupenyeza kwenye udongo na maji yanayotumiwa na watu na mimea. Kila siku tunatupa takataka bila kujali wala kukubali. Takataka hizi ni kama makopo, mifuko ya plastiki, mabaki ya sigara au maganda ya matunda. Baadhi ya takataka ni hatari kwa wanyama na nyingine huweza pia kusababisha majanga kama moto. Aidha, hufanya mazingira yaonekane machafu.Sote tunajukumu kubwa la kuchangia kupunguza uchafu wamazingira. Kwanza, kuelimisha na kutambua umuhimu wa usafi wa mazingira yetu . Tunapaswa kutia takataka zetu kwenye vijalala maalum au mahali tunapoweza kuzichoma na kuziteketeza. Tuhakikishe tunatunza vitu kama mifuko, chupa na kadhalika ambavyo huweza kuundwa upya na kutumika tena. Hali kadhalika, katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwepo na juhudi za kuwahimiza wenye magari kutumia mafuta ya gari ambayo hayana madini ya risasi. Kwa njia hii, tutasaidia kuyaboresha mazingira yetu. Vilevile pana umuhimu wa kutilia mkazo utumiaji wa bidhaa ambazo zinaweza kuoza na kuvunjikavunjika au kusagika na kuwa sehemu ya udongo. Hatua ya kwanza ya kupambana na uchafuzi wa mazingira ni kujielimisha na kuwajibika. Kila mmoja akitoa mchango wake, tutafanikiwa. Kumbuka: kinga na kinga ndipo moto uwakapo. a) Ongezeko la viwanda limechangiaje uchafuzi wa mazingira ? b) Tabaka la ozoni huathiriwaje na uchafuzi? c) Eleza athari zozote tatu za kutotunza mazingira. d) Kwa nini miji mikubwa hukumbwa na uchafuzi kuliko sehemu nyingine? e) Eleza nui mbili za uchafuzi wa mazingira zilizotajwa katika kufungu hiki. f) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika kifungu. i) Msambao - ii) Makopo - iii) Kinga –

    Date posted: October 4, 2019
  • Tumia maneno yafuatayo katika sentensi moja ili kubainisha tofauti zao kimaana; i) Chuuza ii) Chuza

    Date posted: October 4, 2019
  • Eleza tofauti kati ya ama za vielezi vifuatavyo; i) Vielezi vya namna mfanano na; Vielezi vya namna hali. ii) Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vielezi vya hapo juu.

    Date posted: October 4, 2019
  • Andika sentensi moja ukitumia kivumishi cha nomino.

    Date posted: October 4, 2019
  • Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yafuatayo. Faragha ni muhimu kwa binadamu kwani huwa ndio wakati ambapo mtu atakuwa akitulia pekee mahali na huku akijiuliza ni mema mangapi ameyatenda siku hiyo, maovu mangapi ameyafanya, na kama siku hiyo ilikuwa ya manufaa au la. Si binadamu wote ambalo wanapendelea kutumia wakati wao wa faragha kwa kupiga domo, nyumbani, kustawisha mabustani yao ya maua au mimea, au hata kuchukua kitabu au magazeti ya kusoma na kujifunza. Watu kama hawa huwa na fikira na mawazo mbalimbali juu ya umuhimu wa thamani ya wakati wa faragha. Watu kama hao utawakuta wakikusanyika katika makundi kwa matarajio ya kujinufaisha kwa mapato fulani au kujiingiza katika upigaji wa kamari. Wengine hunufaika wakasifu mafanikio yao ya siku ya mkusanyiko na baadhi yao ambapo hufanya mhanga wa michezo hii huibuka huku wakilaani na kuapiza bahati zao mbaya. Kuna kundi jingine ambao hustahabu vilabu vya usiku kwa kujiliwaza au kujitumbuiza ili wapate kujituliza mawazo yao, wakayatafuta makali na kileo. Mwanzo wa ushirika kama huu huwa mzuri, watu huongea na kutoleana mawaidha yenye muafaka kiungwana kabisa. Lakini mara tu baada ya kuyakata makali haya kwa muda hivi, washiriki wake hupumbazwa na huanza kuyakata matindi mithili ya komba mpaka kiasi cha kubwata maneno ovyo ovyo na hatimaye kupoteza mbali fahamu. Ndipo kuruka kwa akili na kuanza zahama zenye kuonyesha utoto badala ya utu uzima. Kadiri makali hayo yanavyosiliwa kwa kuiva kwake, ndivyo wafuasi na mashabiki wake huyatumia kwa wingi na hata kuyaabudu, huyaabufu; huyabugia bila kujali uzito. Na iwapo ndio kwanza wapokee mabunda yao, hakuna la kutia kikomo tafrija hizo ila uzito wa matendo ya ubadhirifu hujitokeza baada ya kurudi nyumbani, kulala fofofo na wazindukanapo siku ya pili yake ndipo wagundue walivyo taabani. Mtindo wa matumizi ya faragha hutokea tangu mwanzo wa mazingira ya mtu; hivyo tangu utoto wake; tabia njema na zipasazo huhitajiwa kufunzwa. Sehemu kubwa ya mafunzo haya muhimu hutokana na malezi ya nyumbani chini ya uongozi wa mama na baba. Kama wasemavyo wahenga, mtoto akuavyo ndivyo alivyolelewa. Na mama mtu awe nyoka, hapana budi kuwa mwanawe naye atainuka kustahabu unyoke” wa mama yake. Hivyo ni wajibu wa wazazi kujenga mazingira yanayofaa kwa vizazi vya kesho kwa kuelekezwa namna yake. Ingewezekana himizo kubwa lingesisitizwa katika marekebisho ya tabia za wazazi kuwezesha manufaa yake. Ingewezekana, himizo kubwa lingesisitizwa katika marekebisho ya tabia za wazazi kuwezesha watoto kuiga mtindo au mitindo ya maisha yanayofaa. Kielezo chema ni kuwa na mzazi mwenye tabia njema kwa mtoto wake, rafiki zake na kwa jamii yake. (a) Ni nini umuhimu wa faragha kwa binadamu kwa mujibu wa aya ya kwanza? (b) Eleza jinsi watu wengine wanavyoharibu wakati wao wa faragha kwamambo ya upotovu kwa kurejelea aya ya pili na ya tatu (maneno 30) (c) Eleza mchango wa mzazi kwa mwanawe kuhusu matumizi bora ya wakati wa faragha. Zingatia aya ya mwisho

    Date posted: October 4, 2019
  • Jadili sababu tano zinazofanya "sheng" isiwe lugha ya taifa.

    Date posted: October 4, 2019
  • Eleza maana ya; i).Mkembe. ii).mkebe.

    Date posted: October 4, 2019
  • Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yafuatayo. Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kutoka kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo. Ubongo wa mwanadamu hutekeleza shughuli hii kwa namna tatu. Kwanza ubongo hunasa jambo kisha huliihifadhi. Baadaye huanzisha mfumo wa kutoa kilicho hifadhiwa. Ubongo ukiathirika kwa namna yeyote katika moja wapo ya njia hizi, basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika. Ingawa inaaminika kuwa uwezo wa kukumbuka hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine, wataalamu wa maswala ya kiakili wanabaini kuwa uwezo huu unaweza kuimarishwa. Uimarishaji huu huhitajika mikakati madhubuti. Njia mojawapo ya kustawisha uwezo wa kukumbuka ni kupitia kwa lishe. Vyakula vilivyosheheni vitamini B vyenye amino asidi husaidia kuimarisha uwezo wa kukumbuka. Vyakula kama hivi ni mboga, nyama (hasa maini), bidhaaa za soya, matunda, maziwa, ,bidhaa za ngano, samaki, pamoja na mayai. Vyakula vingine muhimu katika ustawishaji huu ni vile vyenye madini ya chuma. Madini haya huwezesha usambazaji wa hewa katika ubongo kwa wepesi. Vyakula ambavyo vina madina haya ni mboga za kijani, mawele, ndengu, soya, matunda kama maembe, ufuta (simsim) pamoja na nyama, hasa maini na mayai. Ubongo wa mwanadamu aliye hai hufanya kazi kila wakati awe macho au amelala. Utendaji kazi wake huendeshwa na glukosi mwilini. Kwa hivyo, vyakula vyenye sukari hii ni muhimu kuliwa. Hata hivyo, lazima mtu awe mwangalifu na kuhakikisha kuwa mwili una kiwango cha sukari kisicho hatarisha maisha. Haya yanawezekana kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mboga na matunda. Njia ya pili ni kupiga marufuku vileo kama pombe na nikotini. Vileo hivi huathiri utaratibu wa kunasa, kuhifadhi na kutoa yaliyo ubongoni. Iwapo mtu ana tatizo la kuyakumbuka majina ya watu, ni muhimu kufanya mazoezi ya kusikiliza kisha kurudia majina hayo wakati wa mazungumzo. Ni bora kulihusisha jina na sura ya mtu. Kwa njia hii ubongo utanasa jina na kile kinacholengwa. Woga na kuvurugika kiakili ni mambo mengine tunayopaswa kuepuka kila wakati. Ni kawaida mtu kupata woga wakati anapokabili jambo asilokuwa na uhakika na matokeo yake kama mtihani au mahojiano. Lakini anapaswa kuwa makini. Woga huo usikiuke mpaka na kumvuruga kiakili. Vurugu hizi huathiri kilichohifadhiwa ubongoni na pia namna ya kukitoa. Halikadhalika, mwili wenye siha nzuri huhakikisha kuwa ubongo ni timamu. Wataalamu wengi wa siha wanakubali kuwa na mazoezi ya kunyoosha viungo hustawisha ubongo na hivyo kuhakikisha kuweko kwa uwezo wa kukumbuka mambo. Ni muhimu kuwa na taratibu ya kunyoosha viungo kila wakati. Fauka ya hayo, mazoezi ya kiakili, kama vile kusoma makala yanayovutia, kujaza mraba na michezo mingine kama mafumbo, vitenzi ndimi ni muhimu katika kustawisha uwezo wa kukumbuka. Jamii ya watu wenye uwezo kuyakumbuka mambo ni ya jamii iliyopiga hatua kimaendeleo. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuimarisha uwezo wa kukumbuka kila wakati. a) Kwa maneno 60 – 65 fupisha mchango wa chakula katika uimarishaji wa uwezo wa kukumbuka. b) Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno 80 – 90

    Date posted: October 4, 2019