Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Questions and answers: Kiswahili

Ask, answer and revise exam-style questions across Kenyan subjects and professional courses.

Q&A Categories

Exams With Marking Schemes

2200 Questions    View: All Solved Unsolved

Search Results...
  • Soma Ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali. Beata alikuwa msichana mrembo lakini alikuwa haambiliki, hasemezeki . Fauka ya hayo, alikuwa na tamaa isiyo na kifani. Alipokuwa katika shule ya msingi, walimu na wazazi walimfunza umuhimu wa kuwa na maadili. Isitoshe, alifunzwa masomo vyema lakini akili yake ilikuwa butu. Akawa haingizi chochote cha maana ila uchafu wa fikira. Nyumbani nako hakuzingatia maonyo. Alikuwa hatulii. Wakati fulani wa krismasi, Beata alipomaliza tu shule ya msingi, alikutana na mwanamume mmoja mliliwa na wasichana wengi; mtajika kwa mali na jina lake ni Mshikaji . Beata akadanganywa akadanganyika. Akatorokea kwa huyu Mshikaji ambaye alikuwa ameshawataliki wake wawili tayari. Akawa mke mlezi. Ikabidi awalee watoto waliobaki na baba yao baada ya mamazao kutanzuka. Beata mwanzoni aliona raha, ingawa alikereka kuitwa mama kabla hata ya kumpokea mwana wake mwenyewe. Aliwabeza waliokuwepo awali na akajiona kuwa yeye ndiye mchukuzi bora. Akadharau kuwa pakacha likivuja, nafuu huwa ni kwa yule mchukuzi. Aliwaona wenzake kama maua yaliyonyauka na lake ndilo kwanza linaonana na jua. Muda si muda, akajikuta ana wana watatu kwa kipindi kifupi. Mumewe naye hakutulia na mambo ya nje. Akaimarisha nyendo zake za kiguu na njia, akipochoka, akiingia garini na kuikata mitaa. Beata aende wapi? Alifungika nyumbani ndi ndi Akamlea mwana huyu na yule; wake na wale wa kambo. Vijisenenesenene vikazidi. Lakini akajaribu kuvumilia akidhani atazila mbivu, wapi! Alipoligema ilibidi alinywe. Siku zikaja na kupita. Beata akajuta kwa kutosikiliza wakuu na kumkimbilia mtu ambaye hata hakuwa anamuelewa vizuri. Pesa na raha alizokuwa amezikimbilia akawa anazisikia kama hadithi ndotoni. Kwao nako kukawa hakurudiki. Beata akawa majamzito tena kama kawaida akawa anaenda kliniki za wajawazito. Alipopimwa ikabainika kuwa ana ukimwi. Mtoto alipozaliwa akafariki. Yule mumewe akaanza kumnyanyasa. Baada ya miaka mitatu, bwana Mshikaji, aliyekuwa akijitapa kwa unene na mali, akaanza kupotelewa na kiriba chake cha tumbo. Homa za hapa na pale zikaanza kumyemelea. Vipelevipele vikamsambaa mwilini. Hata akamsingizia Beata kuwa ni yeye aliyeuleta huo ukimwi Ilikuwa ni wazi kuwa msambazaji alikuwa ni yeye bwana. Waliokuwa pembe za chaki waliujua ukweli ulipokuwa . Baadhi ya vidosho wake walishaanza kupukutika kama majani yafanyavyo wakati wa mapukutiko. Isitoshe, wengine walikuwa hoi vitandani wakiwa hawajui waingiao wala watokao. Ugonjwa wa kamata ulishawakamata. Mwisho akawa ni wa kulazwa na kutoka hospitali hizi na zile. Pesa zikawaishia, wakawa waya. Beata akawa hana budi kuviuguza vidonda ndugu vyake na vya mumewe. Hatimaye, mumewe akabwagwa chini na ukimwi na akafafo! Si ndugu si marafiki, hawakumuelewa Beata. Waliamuona kama pweza aliyejipalia makaa makubwa ya moto makali. Ada za shule zikawa ni shida. Huruma ikwaingia watu. Watu wakasema. “Lisilobudi hutendwa.” Wakaubeba mzigo kwa hiari yao. Wakawafanyia watoto harambee ya ada na peza za matibabu. Mwishowe Beata naye aliaga dunia akiwa bado mbichi kwa umri. Hata miaka ishirini alikuwa bado hajafikisha. Watoto ikabidi walelewe na wahisani. Hapo walimwengu wakaja kutambua ukweli kwamba, uzuri si hoja hoja ni tabia. Isitoshe mtu akikimbiliwa na kila mtu, ukimwi hatauepuka. Mtu akiupata, hufa. Anadidimiza watu wengi pamoja na familia yake. Jamii ilifunzwa pia kuwa unene si hoja. Hata watu vibonge huweza kuleta ukimwi. Basi, jamii hiyo ikaazimia kuwa wao hawatakuwa watumwa wa tabia iletayo ukimwi. Walitambua kuwa ukimwi unarudisha nyuma maendeleo na kuipakaza jamii mizigo isiyo tarajiwa. Nasi tutahadhari kabla ya hatari 1. Andika kichwa kifaacho kisa hiki 2. Ni jambo gani lililomkera Beata baada ya kuolewa na Mshikaji? 3. Toa sababu moja iliyomfanya Beata kuwadharau wenzake waliomtangulia kwa mshikaji? 4. Ni kwa nini Beata alianza kujuta? 5. Toa sababu moja kuonysha kuwa Mshikaji ndiye aliyeusambza ukimwi 6. Kulingana na kifungu hiki taja hasara zinazoletwa na ukimwi. 7. Kwa nini walimu na wazazi hawangelaumiwa kwa yale yaliyompata Beata? 8. Andika maana ya: i) butu ii) Kope zikawa si zake iii) Akiwa bado mbichi iv) Kuzanzuka v) Vijisenensenene.

    Date posted: November 21, 2022
  • Tambua kielezi katika sentensi ifuatayo. Kijana mkorofi ameadhibiwa vibaya

    Date posted: August 17, 2020
  • Tambua kivumishi katika sentensi ifuatayo. Mwanafunzi mdogo amezungumza taratibu.

    Date posted: August 17, 2020
  • Athari za vita katika riwaya ya Chozi la heri.

    Date posted: June 15, 2020
  • a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili.

    Date posted: June 15, 2020
  • Nini maana ya kishazi?toa mifano ya vishazi.

    Date posted: May 10, 2020
  • Toa sababu nne zinazosababisha watu kufanya makosa katika matumizi ya lugha.

    Date posted: November 20, 2019
  • Fafanua mambo manne yaliyochochea usanifishaji wa Kiswahili wakati wa ukoloni nchini.

    Date posted: November 20, 2019
  • Tambua aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo. Gaidi aliyepigwa risasi alikuwa amebeba bunduki.

    Date posted: November 20, 2019
  • Ni hisia zipi zinazodhihirika katika matumizi haya ya vihisishi. (i) Maskini! Alinyimwa msaada na serikali (ii) Wallahi! Nikikutana naye atajuta kwa nini kazaliwa.

    Date posted: November 20, 2019
  • Ondoa ‘o’ rejeshi bila kubadilisha maana. Kuimba kulikosifika siku nyingi sasa kunatia shaka

    Date posted: November 20, 2019
  • Fafanua aina ya hali katika sentensi hii. Mtoto acheza mpira

    Date posted: November 20, 2019
  • Eleza matumizi ya kwa katika sentensi ifuatayo. Aliyeshtakiwa kwa wizi alipigwa na watu kwa mawe kisha akapelekwa na msamaria mwema kwa tabibu.

    Date posted: November 20, 2019
  • Toa maana mbili zinazojitokeza katika sentensi ifuatayo. Nilimwonea Karamuni

    Date posted: November 20, 2019
  • Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia neno ‘haya’ kama: (i) Nomino (ii) Kivumishi

    Date posted: November 20, 2019
  • Sentensi zifuatazo ni za aina gani? (i) Japo alijitahidi hakufaulu. (ii) Alijitahidi japo hakufaulu.

    Date posted: November 20, 2019
  • Nyambua kitenzi kifuatacho katika kauli ya kutendama. ‘Shika’

    Date posted: November 20, 2019
  • Huku ukitoa mfano mmoja mmoja fafanua miundo miwili ya ngeli ya U-I.

    Date posted: November 20, 2019
  • Akifisha sentesi zifuatazo. (i) Yangu anaimba mama wimbo (ii) Amicus curiae ni msamiati uliovuma nchini baada ya uchaguzi mkuu.

    Date posted: November 20, 2019
  • Tambua mofimu mbili ambazo si mofimu tegemezi. Kunguru, kijiti, mwanambee, parafujo, majembe

    Date posted: November 20, 2019
  • Unda kivumishi kutokana na kitenzi ‘sadiki’.

    Date posted: November 20, 2019
  • Tunga sentensi ya neno moja yenye viungo vifuatavyo. (i) Kiambishi cha nafsi ya kwanza umoja (ii) Njeo (iii) Yambwa tendwa (iv) Mzizi (v) Kauli ya kufanyiza (vi) Kiishio

    Date posted: November 20, 2019
  • Taja kiwakilishi ngeli cha nomino ‘UMASKINI’

    Date posted: November 20, 2019
  • Eleza tofauti kati ya kiimbo na shadda.

    Date posted: November 20, 2019
  • (b) Tofautisha vitamkwa vifuatavyo. (i) /ny/ (ii) /ng’/

    Date posted: November 20, 2019
  • Taja sifa mbili za mizizi wa kitenzi.

    Date posted: November 20, 2019
  • Sekta za umma humu nchini hazina kifani katika uzembe. Unapohitaji huduma za posta, umeme, maji, mawasiliiano, utayarishaji wa mishahara na malipo mengine, utalazimika kusubiri kwa siku, miezi na hata miaka ili upate haki yako, hata wakati mwingine ukakosa! Wafanyakazi wa sekta hii hukosa kutimiza majukumu yao ipasavyo kutokana na ukosefu wa motisha yaani mishahara duni, uhaba wa nyenzo za kutekeleza majukumu yao na kutozingatia kazi kwa wakaguzi na viongozi wa wafanyakazi. Minghairi ya hali hii, visa vya ufisadi ndiyo sifa inayopambanua huduma za umma. Baadhi ya wafanyakazi hupatikana ofisini na katika maeneo ya kazi kwa nadra sana kwa sababu huwa wanakimbilia kwingineko kutafuta malipo ya kujazia mishahara yao duni kujikimu kimaisha. Athari za matendo haya zimekuwa kukokota kukua kwa uchumi, ukosefu wa imani kwa huduma za umma na utoaji wa huduma hafifu. Kufuatia udhaifu huu, katika siku za majuzi, sekta za kibinafsi zimetambulika kuwa muhimu sana katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Uchumi wa mataifa yanayopendelea sekta za kibinfasi yametambuliwa kukua kwa kasi kuliko yale yanayoandama mfumo kongwe wa serikali kutawala shughuli za uzalishaji mali. Lakini kwa kuwa mashirika ya kibinafsi, aidha, yamebainika kuwa na udhaifu wa aina yake, serikali inaposhirikiana kindakindaki na sekta hii, ustawishaji wa hali za kazi utajiri. Kwa kuwa dhamira kuu ya mashirika ya kibinafsi huwa kujizolea faida kemkem, yamekuwa yakifanyiza wafanyakazi wao kazi nyingi kupita kiasi ambayo mara nyingine huwadhuru kiafya. Japo mshahara wao ni afadhali kuliko wa sekta ya umma, baadhi ya sera huwa kandamizi na hutinga fursa za wafanyakazi kukuza majukumu yao binafsi, mengi yakiwa muhimu kwa jamii kijumla. Ushirikiano wa serikali na mashirika ya kibinafsi, kwa hivyo, una uwezo mkubwa wa kustawisha na kupanua mawanda ya uchumi. Utakuwa dawa mujarabu kwa udhaifu wa pande zote. Sekta za kibinafsi zikijizolea faida nyingi kwa upande mmoja, zitasaidia katika kuondoa uzembe, utepetevu na mapuuza yanayotamalaki huduma za serikali kwani yatalenga uzalishaji mwingi ili kutimiza malengo yao. (a) Eleza mawazo muhimu ya aya tatu za mwanzo kwa maneno 50 – 55. (b) Fupisho aya tatu za mwisho bila kubadilisha maana iliyokusudiwa kwa maneno 75 – 80.

    Date posted: November 20, 2019
  • Takwimu za tafiti za umaskini kila mara huonyesha kuwa bara la Afrika ndilo bara maskini kabisa kote duniani. Takriban wakaazi kiasi cha asilimia themanini hawawezi kumudu kutumia dola moja kwa siku. Toka kaskazini hadi kusini. mashariki hadi magharibi mwa bara, makaazi ya vibanda yametamalaki. Wakaazi wengi hulala njaa kutokana na ukosefu wa chakula. Watu wa mitaani waliovaa mararuraru wamejaa katika miji ya bara hili. Swali ni: Je, kwa nini umaskini umeliganda bara la Afrika hivi mithili ya kupe? Kwa nini bara huselelea katika lindi la uchochole? Ili kuelewa sababu za umaskini kuganda barani Afrika, yampasa mtu ima fa ima kurejelea historia ya bara hili. Kwa kipindi cha karne nyingi, Afrika ilidhibitiwa na walowezi pamoja na mabeberu. Wanawake ambao wangelistwawisha bara hili kiuchumi walitwaliwa kimabavu na kupelekwa, huku wamefungwa minyororo, kustawisha uchumi wa mabara mengine. Afrika ikaporwa nguvu ambayo ni rasilmali kuu katika ustawishaji wa uchumi. La kusikitisha ni kuwa Afrika haikufidiwa kutokana na wizi huu. Badala yake iliongezewa mizigo mingine. Baada ya kipindi cha biashara ya utumwa kumalizika, Afrika ilijipata katika janga jingine. Wakoloni wakaliingilia bara kwa pupa. Wakaligawanya katika koloni mbalimbali miongoni mwao. Wakaingiwa na wendawazimu kuiba malighafi ya bara hili. Wakaiba mashamba, madini, miti na chochote cha maana walichokipata. Badala ya malighafi haya kutumika kunawirisha bara la Afrika, yalitwaliwa kustawisha chumi za walikotoka wakoloni. Afrika ikaachwa kuzidi kudidimia katika lindi la umaskini. Wakoloni walipotoka barani Afrika na kuzipa dola nyingi za Afrika ‘uhuru’, waliacha mkururo wa madhila. Madhila haya hayangeikubalia Afrika kujikomboa kutoka katika biwi la uchochole. Tatizo la kwanza na kubwa zaidi ni wakoloni kugawanya na kukatakata Afrika katika mataifa mengi. Mgawanyo huu ukawa haukufuata utaratibu wowote. Kwa sababu hii, watu wa nasaba moja wakawekwa katika nchi tofauti. Mathalani , watu wa nasaba ya Kisomali waligawanywa na kuwekwa chini ya nchi huru ya Somali, wengine chini ya dola la Uhabeshi, huku wengine wakiwa nchini Kenya na Jibuti. Watu kama hawa hawakutaka mpango huu. Waliokuwa Kenya na Uhabeshi wakachukua silaha na kupigana ili warejeshwe chini ya himaya moja ya taifa huru la Somali. Watu kama hawa wakatumia muda mwingi kupigana; muda ambao ungetumika kuinua Afrika kiuchumi. Mapigano haya ya wenyewe kwa wenyewe yamekithiri kote katika bara la Afrika. Halikadhalika, mkoloni hakufanya juhudi zozote za kuanzisha viwanda ambavyo vingenyanyua uchumi wa Afrika na kuwatoa Waafrika katika biwi la ufukara. Palipokuwa na ari yoyote ya kuanzisha kiwanda, kilipoanzishwa hakikusaidia Afrika kiuchumi. Vilikuwa viwanda vya kupunguza zigo la bidhaa na kuzifanya kuwa nyepesi ili zisafirishwe kwa ajili ya viwanda vya nchi walizotoka wakoloni. Kwa kipindi cha muda ambao mkoloni amekuwa na maingiliano na wakaazi wa Afrika, amehakikisha kuwa mwafrika amekuwa mtegemezi wake. Malighafi ya Afrika yalipelekwa kutayarishiwa viwanda vya wakoloni. Kisha mwafrika alirudishiwa zikiwa bidhaa kamili za kutumiwa. Mwafrika akaonyeshwa kuwa chochote kilichotoka kwa wakoloni ni bora zaidi ya chake alichozalisha. Hii ikawa ni mbinu moja ya wakoloni kuwafukarisha Waafrika. Hata sasa, kilichotoka Ulaya, hata kama ni cha hali ya chini, huonekana bora zaidi kuliko alichozalisha Mwafrika Kwa upande mwingine, inadhihirika kuwa wakoloni hawajawahi kuondoka na kuwaachia Waafrika jukumu kamili la kuendesha uhuru wao kisiasa, kijamii na kiuchumi. Waliondoka kupita mlango mmoja na kurudi kwa wa pili. Mlango wa pili ukawa ni ukoloni kuchukua sura nyingine, sura ya ukoloni mamboleo. Kupitia ukoloni huu, wakoloni hudhibiti uchumi na maendeleo ya Afrika kupitia asasi mbili walizozianzisha, yaani Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani. Ili kupata mikopo ya maendeleo, asasi hizi hutoa masharti ambayo hukwamiza badala ya kuchangia kuleta maendeleo barani Afrika. Sasa hivi pana haja ya wana wa Afrika kufanya vikao vya dhurura ili kujadiliana kuhusu suluhisho la tatizo hili sugu la umaskini barani. Lazima wawahimize Waafrika wote kujikomboa kiakili na kung’amua kuwa maendeleo ya bara lazima yaongozwe na yadhibitiwe na Waafrika wenyewe. Wawahimize kuacha hulka za kukimbilia mataifa yaliyowafanya watumwa na kuwakalia kikoloni kwa misaada ya maendeleo. Misaada hii si ya dhati bali ni ya chati na hailengi kuondoa umaskini barani bali kuuendeleza. Pana haja pia Waafrika kuwa na miungano ya kiuchumi. Miungano hii husaidia katika uteteaji wa soko pamoja na bei za bidhaa zao ikilinganishwa na taifa moja kuyaendeleza mambo haya. Halikadhalika, Waafrika wanapaswa kutambua kile wanachotaka na kupanga mikakati ya kufikia mahitaji ya kimsingi kwa wananchi wake. Kwa mfano, uimarishaji wa mbinu msingi ambazo zitachangia kuimarisha uchumi wa mataifa wahitaji kuwa mstari wa mbele badala ya ununuzi wa magari na ndege za hadhi za kuwabebea viongozi. (a) Ipe taarifa uliyoisoma anwani mwafaka. (b) Kutamalaki kwa umaskini barani Afrika kunadhihirishwa na nini. (c) Onyesha jinsi ambavyo wakoloni wameendeleza umaskini barani Afrika. (d) Thibitisha kwa kutoa hoja tatu, dhana ya kuwa “Waafrika wenyewe ndio wamechangia kuwepo kwa umaskini wa bara la Afrika.” (e) Umaskini barani Afrika unaweza kukabiliwa vipi kwa mujibu wa makala haya? (f) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika taarifa: (i) kuselelea…………… (ii) mabeberu…………

    Date posted: November 20, 2019
  • Halleluyah… Mungu asifiwe sana… shetani ashindwe… Tambua na utoe sifa za sajili hii.

    Date posted: October 31, 2019
  • Eleza dhima ya sentensi hii. Rudi ulikotoka.

    Date posted: October 31, 2019