Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and answers: Kiswahili

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

2287 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Sauti hizi hutamkiwa wapi? /d/ /k/(Solved)

    Sauti hizi hutamkiwa wapi? /d/ /k/

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yatakayofuata Leo hii suala la kuwaonyesha watoto mapenzi ni suala la ziada. Kuna mambo mengine mengi maishani mwetu ambayo tunayachukulia kuwa...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yatakayofuata Leo hii suala la kuwaonyesha watoto mapenzi ni suala la ziada. Kuna mambo mengine mengi maishani mwetu ambayo tunayachukulia kuwa muhimu zaidi. Ni vizuri tuwaokoe watoto wetu, tusije tukawalilia baadaye. Kuna vitendo vya ukatili ambavyo watoto hutendewa. Hivi majuzi tumekuwa na visa vya vilenge kung’olewa mimbani viumbe hawa walipokatiziwa uhai, maiti zao zilitupwa kama takataka. Hiyo ni miili ambayo ilipatikana je, ni maelfu mangapi ya miili mingine kama hiyo inayotupwa? Hii tu ilikuwa tone ndogo tu la bahari ya dhambi ambazo zote tunaogelea ndani. Mambo kama haya ni mazao ya mimea yetu ambayo tulipanda sisi ambao hatuchelewi kujiita watu walio huru, walio na maendeleo na wa kisasa. Tumekuwa watu wa kupuuza mambo ya kimapokeo ya kuzingatia utu na kuficha aibu aghalabu tumejitia usasa kwa kutazama filamu na video chafu, kusikiliza muziki wenye maneno machafu. Tunapoona watoto wetu wakitembea nusu uchi, hatushughuliki hata kidogo kuwakanya. Kama ni kosa, sisi sote tumehusika kwa njia moja au nyingine kwa njia tofauti. Ni vizuri tuelewe kuwa sisi ni wakuuzaji na walizi wa ndugu zetu kwa kila njia. Tutawaokoa watoto kwa kukataa mambo yote yanayowanyanyasa. Lazima tuwaonyeshe watoto mapenzi, mapenzi si chakula, mavazi na makazi tu. Mapenzi si kuwaachia vijana uhuru watende watendavyo. Mapenzi sio kuwanunulia watoto vitu vya bei ghali au kuacha kuwakemea wanapokosa mwelekeo. Mapenzi kwa watoto ni kuwaheshimu na kuwatendea kama binadamu yeyote. Lazima mzazi akumbuke kwamba mtoto hujifunza kutoka kwake. Mtoto atakutendea isitoshe jinsi unavyomtendea. Isitoshe jinsi unavyomtendea mtoto wako ndivyo atakavyowatendea watoto wake na wale wote ambao atapata kuhusiana nao kwa njia moja au nyingine. Tuwaokoe watoto wetu katika viwango vyote vya ukuaji. Kusiwe na mwanya baina ya mzazi na mtoto. Watoto wawe kutuambia yote yanayowahangaisha mioyoni mwao, na hali hii itawapa wazazi fursa ya kuwasaidia. Mtoto anapokosa, tuwe tayari kumwonyesha kosa lake na kumwadhibu kwa mapenzi. Mtoto wa mwenzetu akipotoka pia tuwe tayari kumkosoa na kuwaarifu wazazi wake. Tuwache ubinafsi wetu kumbuka kuwa mwana wa mwenzio ni wako. Ni jambo la busara kuhakikisha kuwa kama wazazi, tuzingatie haki zote za watoto. Maswali 1. Kwa nini suala la kuwaonyesha watoto mapenzi limekuwa la ziada. 2. Ni mambo gani ambayo yanaweza kutufanya tuwalilie watoto wetu baadaye? 3. Toa sababu zinazowafanya watu kuavya mimba. 4. Ni mambo yapi ambayo yanachangia kupotoka kwa jamii? 5. Mwandishi ametumia tamathali za usemi. Zitaje huku ukitoa mifano kwa kila mojawapo. 6. Andika maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika habari. (a) Vilenge (b) Mwanya

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Kamilisha au kuanzisha methali zifuatazo: i. Fumbo mfumbie……………… ii. Baniani mbaya …………… iii. …………….si kazi kudamirika iv. ………… Sanda.(Solved)

    Kamilisha au kuanzisha methali zifuatazo: i. Fumbo mfumbie……………… ii. Baniani mbaya …………… iii. …………….si kazi kudamirika iv. ………… Sanda.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza sifa tano za hadithi.(Solved)

    Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza sifa tano za hadithi.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Taja vipera vinne vya fasihi simulizi.(Solved)

    Taja vipera vinne vya fasihi simulizi.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Eleza dhima nne za lugha.(Solved)

    Eleza dhima nne za lugha.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Taja sifa nne za lugha.(Solved)

    Taja sifa nne za lugha.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Ni nini maana ya lugha?(Solved)

    Ni nini maana ya lugha?

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Andika sentensi hizi katika nyakati zilizo kwenye mabano. Wageni walisafiri kwenda ng’ambo. (ujao) Mtoto anakula chakula. (mazoea)(Solved)

    Andika sentensi hizi katika nyakati zilizo kwenye mabano. Wageni walisafiri kwenda ng’ambo. (ujao) Mtoto anakula chakula. (mazoea)

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Eleza maana mbili za neno paa.(Solved)

    Eleza maana mbili za neno paa.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Onyesha kikundi Nomino na Kikundi Tenzi katika sentensi sifuatazo Mwizi aliyetoroka amepatikana mjini Mwanafunzi mwerevu amepita vizuri(Solved)

    Onyesha kikundi Nomino na Kikundi Tenzi katika sentensi sifuatazo Mwizi aliyetoroka amepatikana mjini Mwanafunzi mwerevu amepita vizuri

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Andika kinyume cha sentensi hii. Tajiri aliyekashifiwa amebarikiwa. (Solved)

    Andika kinyume cha sentensi hii. Tajiri aliyekashifiwa amebarikiwa.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Jaza jedwali lifuatalo kwa kauli mwafaka.(Solved)

    Jaza jedwali lifuatalo kwa kauli mwafaka. fig11.png

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Andika ukubwa wa sentensi uliyopewa. Kijiti hiki kilipotezwa na kitoto hiki.(Solved)

    Andika ukubwa wa sentensi uliyopewa. Kijiti hiki kilipotezwa na kitoto hiki.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Yakinisha sentensi uliyopewa. Mama hakuenda sokoni wala hakupika.(Solved)

    Yakinisha sentensi uliyopewa. Mama hakuenda sokoni wala hakupika.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Andika sentensi zifuatazo upya kwa kutumia kirejeshi ‘amba’ Gunia lililoletwa ni lake. Wavu umekatika. Wavu ni wao. (Solved)

    Andika sentensi zifuatazo upya kwa kutumia kirejeshi ‘amba’ Gunia lililoletwa ni lake. Wavu umekatika. Wavu ni wao.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Taja aina tatu za maktaba.(Solved)

    Taja aina tatu za maktaba.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Majina yafuatayo yamo katika ngeli gani: Nywele Maji Jibwa(Solved)

    Majina yafuatayo yamo katika ngeli gani: Nywele Maji Jibwa

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Ainisha viambishi katika sentensi ifuatayo: Alimtembelea(Solved)

    Ainisha viambishi katika sentensi ifuatayo: Alimtembelea

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Akifisha sentensi hii. sikukuu ya madaraka nilikwenda eldama ravine kumwona yohana naye akasema atakuja kuniona pamoja na mkewe mariamu siku ya jumapili.(Solved)

    Akifisha sentensi hii. sikukuu ya madaraka nilikwenda eldama ravine kumwona yohana naye akasema atakuja kuniona pamoja na mkewe mariamu siku ya jumapili.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Andika kwa umoja. Machaka ya waridi hayazai maua meusi Walituandikia nyaraka ndefu.(Solved)

    Andika kwa umoja. Machaka ya waridi hayazai maua meusi Walituandikia nyaraka ndefu.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Ainisha silabi katika maneno yafuatayo Lugha Muhtasari(Solved)

    Ainisha silabi katika maneno yafuatayo Lugha Muhtasari

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Onyesha matumizi matatu ya kiimbo katika sentensi ifuatayo: Mtoto analia.(Solved)

    Onyesha matumizi matatu ya kiimbo katika sentensi ifuatayo: Mtoto analia

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Weka shadda katika maneno haya. Maharagwe Tupa(Solved)

    Weka shadda katika maneno haya. Maharagwe Tupa

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Taja konsonanti ambazo ni viyeyusho.(Solved)

    Taja konsonanti ambazo ni viyeyusho.

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Eleza sifa za sauti zifuatazo: /o/ /Sh/(Solved)

    Eleza sifa za sauti zifuatazo: /o/ /Sh/

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata: Hapo zamaniza kale palikuwa na mfalme aliyesifika sana. Sifa zake zilienea karibu na mbali. Zilienea kama moto nyikani msimu wa...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata: Hapo zamaniza kale palikuwa na mfalme aliyesifika sana. Sifa zake zilienea karibu na mbali. Zilienea kama moto nyikani msimu wa kiangazi. Mstahiki Salamwana Salamwene, maana hili ndilo lilikuwa jina lake, alikuwa mtu wa ajabu sana. Asili yake yenyewe ilikuwa kitendawili. Inasemekana mamake alibeba mimba iliyopita miezi tisa. Na kila aliposhangaa alisikia sauti tumboni ikisema. “Mama kuwa na subira, bado ninalainisha lugha yangu” Baada ya muda mama alipolalamika alisikia, “Mama ninakaribia, ninamalizia kunoa ubongo wangu.” Halafu siku moja ikanyesha mvua kubwa iliyoandamana na radi. Waliokuwepo wanasema waliona mmweso mkali ulioangaza hata kwenye milima mikubwa. Salamwene akazaliwa. Moja ya sifa zake kubwa ilikuwa hekima na maarifa ya ajabu. Hakuna tatizo la watu wake ambalo alishindwa kulitatua. Watu wakawa wanafunga safari za siku nyingi kutoka mbali kuja kwenye ikulu yake. Wengi walienda kwa shida za dhati lakini wengine walikuja kumjaribu. Siku moja akaja mfanyabiashara tapeli na maua ya aina akamwambia, “Mstahiki mfalme, mtu wako anataka kuniuzia maua haya kwa vipande vingi vya almasi name nina shaka kuwa moja ni la bandia waweza kuniamulia?” Mfalme hakujibu. Naye inasemekana alipenda zaraa na hivyo alikuwa na miti na mimea iliyozaa maua na kutoa harufu anuwai. Basi akaja nyulu na kutua kwenye ua moja. Mfalme Salamwana akamtambulisha ua halisi. Muda ukayoyoma huku wahitaji wakiingia ikulu na kutoka. Siku moja akaja Binti mfalme mmoja kutoka nchi ya mbali na msafara mkubwa. Alipokewa kwa taadhima. Alikaa mwezi mmoja. Kila siku alikaa kwenye baraza akishuhudia mfalme akiyatatua matatizo ya watu. Jioni walikaa na mfalme pamoja wapambe wao akijifunza kutoka kwenye hazina kubwa ya busara ya Mstahiki Salamwana. Usiku uliotangulia kuondoka kwa mgeni, Salamwana alitoa amri za ajabu. Kwanza, aliamuru magudulia yote ya maji kwenye chumba cha kulala mgeni yabadilishwe. Pili, alimwamuru mpishi kupika chakula kilichokolea viungo kutoka Bara Hindi. Tatu, aliwaamuru wapambe kuwa mgeni akiomba chochote wasimpe ila wamfahamishe. Usiku huo, mgeni alihisi kiu kikali lakini aliponyanyua gudulia kumimima maji kwenye bilauri ya dhahabu, halikuwa na maji. Akajaribu la pili, magudulia yote ya shaba yaliyokuwa chumbani hayakuwa na maji. Alijitahidi kuvumilia lakini wapi! Ilibidi atafute msaada kwa wapambe nao wakamweleza walivyoambiwa. Mwanzoni aliona ni kukosa fadhila kumsumbua mwenyeji mwenye staha kama mfalme. Kiu ilipozidi kumkeketa koo alisalimu amri. Mfalme alifahamishwa. Na kama aliyejua alichoitiwa akaja na kigudulia kidogo chenye nakshi ya dhahabu na kifuko cha hariri. Alikuwa radhi kumpa mgeni sharubati ya kukata kiu ila kwa masharti. Anapokunywa maji ameze na zawadi atakayompa ambayo angeitapika afikapo nyumbani. Keshowe mgeni aliagwa kwa mbwewe na taadhima. Akaanza safari iliyochukua takriban mwezi mmoja. Baada ya miezi kumi, Mstahiki Salamwana Salamwene alipata risala kuwa Binti wa Mfalme alikuwa ameitapika zawadi aliyopewa kama alivyokuwa amekula yamini. Hicho kikawa kitendawili kwa watu wengi. Wakabaki wakiulizana jibu la fumbo hilo. Maswali 1. Ipe hadithi hii anwani mwafaka. 2. Kwa nini ilisemekana asili ya Mfalme Salamwana ilikuwa kitendawili? 3. Eleza sifa sita za mfalme zinazojitokeza kwenye kifungu. 4. Ni watu gani walikuja kwa mfalme. 5. Mfalme alitumia hekima gani kutambua ua la bandia. 6. Ni zawadi gani aliyopewa Binti mfalme aliyoitapika alipofika nyumbani? 7. Ni ujumbe upi unaopatikana kutoka na hadithi hii. 8. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika kifungu. i. Maguduli ii. Sharubati iii. Dhati iv. yamini

    Date posted: November 22, 2022.  

  • Andika visawe vya viwakifishi hivi. (i)Nukta- (ii)Koma – (iii)Mkwaju- (iv)Mtajo-(Solved)

    Andika visawe vya viwakifishi hivi. (i)Nukta- (ii)Koma – (iii)Mkwaju- (iv)Mtajo-

    Date posted: November 21, 2022.  

  • Ainisha mofimu na viambishi katika neno Aliyesomewa.(Solved)

    Ainisha mofimu na viambishi katika neno Aliyesomewa.

    Date posted: November 21, 2022.  

  • Bainisha aina za maneno katika sentensi hizi. (i) Mwalimu anaandika . (ii) Mwalimu anaandika ubaoni.(Solved)

    Bainisha aina za maneno katika sentensi hizi. (i) Mwalimu anaandika . (ii) Mwalimu anaandika ubaoni.

    Date posted: November 21, 2022.