Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Questions and answers: Kiswahili

Ask, answer and revise exam-style questions across Kenyan subjects and professional courses.

Q&A Categories

Exams With Marking Schemes

2200 Questions    View: All Solved Unsolved

Search Results...
  • Kanusha. Mwanafunzi alikuwa akilia alipojikwaa.

    Date posted: October 31, 2019
  • Onyesha aina ya vishazi katika sentensi hii. Isipokuwa ni kulewa kwake angeenda Kitui.

    Date posted: October 31, 2019
  • Kosoa sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti. Ningelima shamba langu kwa wakati ufaao ningalivuna sawasawa.

    Date posted: October 31, 2019
  • Tunga sentensi kutofautisha maana ya majina haya. Nadhari Nathari

    Date posted: October 31, 2019
  • Onyesha shamirisho katika sentensi ifuatayo. Kakubwa alimjengea mama yake nyumba kwa mawe.

    Date posted: October 31, 2019
  • Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika kauli ya kutendwa. Simba mwenda pole alimla swara mnono sana.

    Date posted: October 31, 2019
  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi. Anampenda wake sana lakini alimpiga sana

    Date posted: October 31, 2019
  • Tumia neno msomi kama nomino na kama kivumishi katika sentensi.

    Date posted: October 31, 2019
  • Andika kinyume cha sentensi hii. Mama alienda sokoni jana asubuhi.

    Date posted: October 31, 2019
  • Andika sentensi hii kwa udogo wingi. Mti ulikatwa ukatengeneze kiti.

    Date posted: October 31, 2019
  • Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi cha kuongeza.

    Date posted: October 31, 2019
  • Tumia kiambishi ndi- pamoja na kiwakilishi huru cha nafsi ya kwanza wingi.

    Date posted: October 31, 2019
  • Thibitisha kuwa neno moja linaweza kuwa katika ngeli mbili tofauti.

    Date posted: October 31, 2019
  • Onyesha mofimu mbalimbali katika neno kikikipikia.

    Date posted: October 31, 2019
  • Eleza kanuni ya kutia shadda katika lugha ya Kiswahili.

    Date posted: October 31, 2019
  • Toa mfano wa maneno mawili ambayo yana sauti mwambatano mbili.

    Date posted: October 31, 2019
  • Taja sifa mbili za irabu /e/ na /i/ ambazo zinafanana.

    Date posted: October 31, 2019
  • UHUSIANO WA FASIHI NA HISTORIA Historia na fasihi zina uhusiano wa karibu sana hasa fasihi ya kihistoria. Hata hivyo fasihi sio historia na historia si fasihi kwa sababu hizi ni taaluma mbili ambazo zina uhusiano tu. Hata hivyo, fasihi na historia zina mambo ambayo yanafana na yale ambayo hayafanani. Kati ya mambo ambayo yanafanana ni kwamba fasihi na historia wakati mwingine huweza kuwa na wahusika ambao wanafanana kitabia, kimaumbile na hata wakati mwingine matendo ya kukumbukwa waliyofanywa. Mfano ni katika shairi la “Hongera Rais Moi” katika diwani ya ' Malenga wa ziwa kuu' ambapo mhusika ni rais Moi na mhusika kama yule pia aliishi katika kipindi Fulani katika nchi ya Kenya. Jambo jingine ambalo linapatikana katika fasihi na pia kinaoana na historia ni mandhari. Wakati mwingine, mandhari ambayo ni ya kihistoria yanakaribiana sana na ya kifasihi na hata wakati mwingine kufanana. Mandhari ya shamba la bwana Delamon katika 'kilio cha haki' yanaweza kuwa shamba lolote na mabwanyenye kama hata ni ya Bwana Dalamere. Wakati mwingine matukio katika fasihi huwa karibu sawa na yale ambayo yanapatikana katika historia ya kawaida. Mfano katika shairi la ' wasifu wa baba Kenyatta', mhusika mkuu yasemekana alipigania uhuru wa nchi ambayo aliiongoza. Matukio kama kufungwa jela ambayo mhusika huyu anapitia katika kujaribu kukomboa nchi ni sawa na yale ambayo mhusika wa kihistoria ambaye ni rais wa kwanza wa nchi ya Kenya. Pia, wakati mwingi historia na fasihi huwa na maudhui na dhamira sawa. Tamthilia kama 'Mstahiki Meya' ambayo nia yake ni kuonyesha jinsi waafrika ambao walichuukua uongozi baada ya ukoloni walivyowanyanyasa waafrika wenzao yaweza kuwa sawa na historia ambapo waafrika ambao walichukua uongozi waliwanyanyasa waafrika wenzao. Uhusiano mwingine wa karibu ni kwamba wakati mwingine fasihi huchota kutoka kwa historia na inapofanya hivyo fasihi hiyo inakuwa ya kufanana sana na historia yenyewe.Mfano ni kitabu cha mzalendo kimathi ambapo matukio mengi katika kitabu hicho kinadhihirisha kwamba kimechota kutoka kwa historia. Pia baada ya kipindi Fulani, fasihi husika inakuwa historia. Uhusiano mwingine ni kwamba zote huandikwa kwa lugha na zinapoandikwa fasihi hufufua majina ya wale ambao majina yao hayakuweza kuingia katika vitabu vya historia. Mwisho, historia na fasihi hufanya jukumu la kumjuza mwanadamu kuhusu mazingira yake hasa yale ya zamani na kumuwezesha kuweza aidha kuyarekebisha au kuyakubali. Mfano ni katika tamthilia ya kidagaa, Mtemi Nasaba Bora anawapokonya waafrika wezake mashamba kwa kutumia nguvu. Fasihi hii pia inaoana na jinsi ambavyo historia inafunza ambavyo viongozi wa kwanza walivyojipatia vipande vikubwa vikubwa vya ardhi.Fasihi na historia pia zinakaribiana sana kutokana kwamba mwanahistoria na mwanafasihi ni wanajamii wote. Wale ambao huchunguza matukio ya kihistoria na wale ambao huandika fasihi pia ni wanajamii. Mojawapo wa tofauti ya historia na fasihi ni tofauti ya kiwakati. Historia imefungika kiwakati hivi kwamba upeo wake ni sasa. Mwanahistoria akitaka kujuza kuhusu nchi Fulani anaeleza ilikoanza hadi ilikofika lakini mwanafasihi anaweza kueleza mahali nchi fulani ilikoanza, iliko sasa na itakavyokuwa baada ya miaka mingi baada ya sasa. Mwanafasihi anaweza kuandika kuhusu nchi ya kesho peke yake na fasihi iwe imekamilika. Mfano mwema ni George Orwell ambaye alikiandika kitabu mwaka wa 1978 na akakiita 1984. Pia Riwaya ya 'Walenisi' ni riwaya ambayo inazungumza kuhusu dunia ambayo ni ya kesho jambo ambalo historia haiwezi. Tofauti nyingine ni kwamba historia hutegemea ithibati ili iweze kufahamisha. Kama inazungumzia kuhusu tukio Fulani, lazima iwe na dhibitisho sahihi na hamna nafasi ya ubunifu. Kwa upande mwingine, fasihi ina nafasi ya ubunifu na sio lazima mwanafasihi adhibitishe yale ambayo ameandikia yalifanyika. Hata kama Mstahiki Meya ni jina ambalo ni la kihalisia katika masikio ya Wakenya, mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki hana jukumu la kutoa idhibati za kuonyesha kwamba aliishi na pia cheneo ni mojawapo wa miji ya nchi fulani. Tofauti nyingine ni kwamba kila mwanafasihi huwa na itikadi yake lakini mwanahistoria huweka mambo jinsi yalivyo na kumwachia msomaji awe wa kuamua. Mwandishi kama wa tamthilia ya 'Mstahiki Meya' ana itikadi kwamba viongozi dhalimu wanastahili kuondolewa mamlakani kwa nguvu lakini mwanahistoria hawezi kuwa na msimamo kama huo. Tofauti nyingine ni kwamba fasihi hujikita sana kwa wahusika na maisha yao lakini jambo kuu na ambalo historia huzingatia sana ni matukio na wakati ambao matukio hayo yalitokea. Hili hufanya takriban fasihi zote kuwa na mhusika mkuu lakini kipindi fulani cha historia chaweza kosa hata mhusika mmoja mkuu. Jambo jingine ni kwamba historia na fasihi hutofautiana kiwakati, mahali na mandhari ambamo matukio fulani yanatokea. Tamthilia kama ya ‘Mstahiki Meya’ ina uwezakano kwamba inazungumza kuhusu Kenya na viongozi wa baada ya uhuru lakini mahali ambapo matukio ya tamthilia yanafanyikia ni cheneo ala sio wa mji kama Nakuru au Nairobi. Tofauti nyingine ni kwamba hamna nafasi ya ubunifu katika historia lakini fasihi huwa ni zao la ubunifu. Mambo ambayo wanahistoria huwa wamekosa katika historia yanaweza yakawa wazi kupitia ubunifu wa mwandishi. Fasihi pia inaweza ikaumba wahusika au hata dunia ambayo haiwezi ikapatikana katika ulimwengu wa kawaida. Maswali. a. Fupisha aya tatu za kwanza kwa maneno 20-30. Nakala safi b. Fupisha aya tano za mwisho kwa maneno kati ya 60-70 Matayarisho

    Date posted: October 31, 2019
  • Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Siku ya Alhamisi tarehe 4 Disemba 2014 Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti ukitahadharisha juu ya kuongezeka vitendo vya ghasia na mauaji nchini Kenya. Ripoti hiyo inasema kuwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita watu zaidi ya 300 wameuawa na wengine takribani 220,000 kulazimika kuishi kama wakimbizi kutokana na ghasia hizo. Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja huo amesema kuwa ukame mkubwa na mivutano inayotokana na siasa za kuhamishia madaraka mashinani ni baadhi ya mambo yanayochangia kuongezeka vitendo vya ghasia na mapigano katika maeneo ya kaskazini na ya mbali nchini Kenya. Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa wizi wa mifugo na mauaji ya kulipiza kisasi kati ya jamii hasimu za wafugaji katika maeneo hayo ni jambo la kawaida na kwamba silaha ndogondogo zinapatikana kwa wingi kati ya jamii hizo. Ugomvi wa kuwania ardhi, malisho, vyanzo vya maji na madaraka ya kisiasa mwaka huu umewafanya raia wengi katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya kuwa wakimbizi katika nchi yao wenyewe. Kwa kadiri kwamba idadi ya wakimbizi hao imeongezeka mara nne zaidi ikilinganishwa na ya mwaka uliopita wa 2013. Mbali na matatizo ya ndani yanayotokana na ukame na ugomvi wa kikabila, mashambulio ya kundi la kigaidi la al- Shabaab ni jambo jingine ambalo linahatarisha usalama wa Kenya. Kundi hilo Jumapili iliyopita lilitangaza kuhusika na bomu lililolipuka katika soko moja huko mjini Garissa, mashariki mwa Kenya karibu na mpaka wa nchi hiyo na Somalia. Kundi hilohilo lilihusika na mauaji ya abiria 28 waliokuwa kwenye basi moja la shirika la usafiri la Makka lililokuwa njiani kutoka mjini Mandera kaskazini mwa nchi kuelekea mji mkuu Nairobi. Siku 10 baadaye kundi hilo hilo la kigaidi lilivamia na kuwafyatulia risasi kinyama wafanyakazi 36 wa machimbo ya mawe katika kijiji cha Koromey kilicho nje kidogo ya mji huo wa Mandera. Katika tukio jingine la mashambulio ya kundi la al- Shabaab katika maeneo yanayopakana na Somalia, siku ya Jumatatu iliyopita kundi hilo lilishambulia klabu ya Ngamia mjini Wajir na kuwafatulia risasi kiholela watu waliokuwa katika klabu hiyo ambapo waliua mmoja kati yao na kuwajeruhi wengine 13. Visa hivyo vya machafuko na ukosefu wa usalama vilimpelekea Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Jumanne iliyopita kuwafuta kazi Waziri wa Mambo ya Usalama wa Ndani pamoja na Inspekta Mkuu wa polisi ya nchi hiyo. Kufuatia matukio hayo, vyombo vya usalama vya Kenya vimezidisha hatua za kiusalama nchini ili kuzuia kukaririwa kwa matukio kama hayo ya utovu wa nidhamu na usalama. Mbali na hayo mwaka uliopita kundi la al- Shabaab lilishambulia na kusababisha maafa na hasara kubwa katika jengo la maduka ya kibiashara la West Gate mjini Nairobi. Al- Shabaab linapigana na kikosi cha askari wa kulinda amani cha Umoja wa Afrika kinachohudumu huko Somalia AMISOM na limekuwa likitekeleza mashambulio ya kigaidi nchini Kenya kama alama ya kulalamikia ushiriki wa nchi hiyo katika kikosi hicho, ili hatimaye liilazimishe iondoe askari wake katika radhi ya nchi hiyo. 1. Yape makala haya kichwa mwafaka. 2. Taja matatizo manne ya ndani kwa ndani ambayo yanahatarisha usalama wa Kenya.(alama 2) 3. Taja matukio matatu yaliyomfanya rais awapige kalamu waziri na inspekta mkuu wa polisi (alama 3) 4. Eleza sababu wanayotoa wana al-Shabaab ya kutekeleza ukatili dhidi ya Wakenya. (Alama 2) 5. Eleza dhamira ya kikundi cha al-Shabaab 6. Kwa maoni yako mwenyewe, Eleza mambo matatu ambayo anayevamiwa na kundi la al-shabaab anaweza kufanya ili kujiokoa na kuokoa wengine. 7. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kufungu. a) Radhi b) Wakimbizi

    Date posted: October 31, 2019
  • Fafanua sababu tatu zilizochochea usanifishaji wa lugha ya Kiswahili kabla ya uhuru .

    Date posted: October 29, 2019
  • Eleza mambo manne yaliyochangia kuenea kwa lugha ya Kiswahili kabla ya uhuru wa mataifa ya Afrika mashariki .

    Date posted: October 29, 2019
  • Tambua hali na nyakati katika sentensi ifuatayo Atakuwa ameondoka utakapofika.

    Date posted: October 29, 2019
  • Geuza sentensi ifuatayo kwa kutumia kirejeshi ‘AMBA’ Mti uzaao matunda mengi ulikatwa jana

    Date posted: October 29, 2019
  • Unda sentensi yenye muundo ufuatao. T+E+H+N+T+E

    Date posted: October 29, 2019
  • Ainisha vitenzi vilivyopigiwa mstari Niliwahi kumwona kifaru. Niliwahi gari hilo la asubuhi.

    Date posted: October 29, 2019
  • Toa visawe viwili vya ‘uchochole’

    Date posted: October 29, 2019
  • Kanusha sentensi ifuatayo: Aimbapo vizuri mtuze

    Date posted: October 29, 2019
  • Bainisha maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii Mshikie mtoto.

    Date posted: October 29, 2019
  • Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa Paka huyu aliguguna mfupa wa mtoto huyu.

    Date posted: October 29, 2019
  • Tunga sentensi mbili kudhihirisha matumizi ya virai vifuatavyo na uvipigie mstari a)Kirai Nomino b)Kirai kivumishi

    Date posted: October 29, 2019