Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Keiyo District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Keiyo District Mock - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2006



102/2
KARATASI 2
1. UFAHAMU
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali;
Watu wamesimama nusu mduara chini ya mti mkubwa. Wanafanya kelele na kuinua silaha zao. Mbele
yao kuna viongozi. Hivi ndivyo marnbo yalivyoendelea.
Mkuu wa wilaya: Ningependa kiongozi wenu awasilishe matatizo yenu. Tafadhali ketini
tumsikilize.
Mzee: Wakale hawakuropoka walipolonga kuwa ng'ombe akivunjika guu
malishoni, hujikokota zizini. Sisi Walukenya tumepata dhiki isiyo
kifani. Chanzo cha idhilali yetu ni wanyama pori. Ninasema uongo?
Umati: (Kwa kishindo) HAPANA!
Mzee: Tuvumilie hadi lini? Tumeamua kupiga milundi kuleta malalamiko yetu
kwa serikali. Tatizo letu la kwanza ni usalama. Wiki hii tumezika vijana
watano. Mwezi uliopita, tulipoteza watu watatu. Wote hawa ama
wamevyogwa na ndovu au wamegotwa na vifaru kama sio nyati. Udhia
tuupatao ni kuwa tunapowazika fisi nao huwazikua. Linalotuudhi zaidi
ni kuwa serikali haitoi fidia na mara chache inapotoa, ni shilingi
thelathini elfu tu. Yaani, maisha ya binadamu ni rahisi hivyo?
Wanaonusurika mashambulizi hubidi wagharamie matibabu yao
wenyewe. Walukenya hawa na usalama. Linalotisha mno ni kuwa siku
hizi wanyama mwitu wanatuvamia hata mchana juzi, ndovu
alishambulia matatu barabarani na kujeruhi watu wengi. Shughuli zetu
za kila siku zimekwama. Mbali na hayo makazi, nyua na rasilmali kama
miti na mito inaharibiwa na hawa wanyama, (Akigeukia umma) Kweli
au sio?
Umati: (Kwa sauti) Kweli kabisa!
Mzee: Tatizo la tatu linahusu mifugo. Hakuna aliye salama. Ng’ombe
wanaliwa ovyo na simba. Chatu wanameza kuku, huku nyoka wadogo
wakigubia mayai. Mwezi uliopita, chui waliwaua mbuzi thelathini wa
Mzee Kitainge na kula ini la mmoja tu. Mifugo ni uhai wa WaluKenya.
Watakuwa nini bila mifugo? Isitoshe, wanyama pori wamedidimiza
malisho ya mifugo yetu. Tuingiapo mbugani, tunashtakiwa. Tangu lini
wanyamapori wakawa muhimu kuliko binadamu? Halafu mara kwa
mara mifugo wanaambukizwa maradhi sugu. (anakohoa kidogo na
kuendelea) la nne ni kuwa, tangu jadi, Walukenya wanajilisha lakini
siku hizi wanaomba chakula. Kwa nini Wanyama wameharibu mimea
yetu. Tumekataa kuhangaishwa zaidi. Tumeandaa silaha na kesho
tunaanza kuwaangamiza wanyama pori.(Anaketi huku akishangiliwa
kwa vifijo na nderemo).
Mkuu wa wilaya: Afisa Tarafa, Chifu, Madiwani na Walukenya wote. Hamjambo? Kwa
kweli mali na maisha ya watu wengi yamepotea. Nawashukuru kwa
uvumilivu wenu. Nawahakikishia kuwa penye wazee hapaharibiki neno.
Naahidi kuwa serikali itatatua matatizo yenu. Hakuna haja ya
kushambulia wanyama pori. Hatua hiyo ni kama kuchukua sheria
mikononi mwenu. Serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa wahusika.
Umati: Aaah!
Mkuu wa wilaya: Serikali inashughulikia migogoro baina ya binadamu na wanyamapori
katika nchi nzima. Imeunda jopo kukusanya maoni kuhusu fidia na
suluhisho. Jopo hili litakuwa hapa kesho kutwa. Nawahimiza mje kwa
wingi na mtoe maoni yenu.
Mtu: Maoni na tunateseka?
Mkuu wa wilaya: Tunapongojea matokeo ya jopo, serikali imechukua hatua za dharura.
Hizi ni pamoja na kuanzisha kikosi maalumu cha askari wa kulinda
wanyama na binadamu. Serikali pia itajenga ua wa umeme kuzunguka
mbuga ili wanyama wasitoke. Zaidi ya hayo, serikali itajenga mabwawa
mbugani na kuimarisha Idara ya Tiba kwa mifugo wilayani. Haya
yamefanywa ili kulinda wanyama pori. wanyama pori hawana uwezo wa
kujitetea. Hata hivyo, sote twajua manufaa yao. Ili hatua za serikali
zifaulu na ili muishi na wanyama kama ilivyokuwa tangu jadi, naomba
mfanye mambo fulani. Kwanza, ningependa mjizuie kuwinda wanyama
pori. Hili hutatiza mkufu wao wa utegemezi. Vilevile, msiwachokoze
wanyama.jambo hili huwakasirisha na kuwafanya kuwashambulia. Pili,
tujizuie kuingilia njia za wanyama za kuhama, pamoja na malisho yao.
Mwisho, mchukue hatua za kujilinda kutokana na wanyama pori. Hizi ni
pamoja na kuzungushia makaazi nyua na kupiga ripoti kwa
walindambuga hatari itokeapo. Mungu aliwapa Adamu na Hawa jukumu
la kulinda rasilmali zote ardhini. Kama vizazi vyao, nasi lazima tubebe
jukumu hilo kifuani. Ahsanteni.
Maswali:
1. Kwa kurejelea taarifa, eleza ukweli wa methali "Ng'ombe akivunjika mguu malishoni
hujikikota zizini kusaidiwa". (alama 2)*Kyo*
2. Taja malalamiko manne yaliyowasilishwa na wanakijiji. (alama 2) *Kyo*
3. Kuvamiwa kwa wanakijiji na wanyama pori kuna athari gani kwa mifugo wao?
(alama 2) *Kyo*
4. Ni hatua gani ambazo serikali imechukua ili kutatua migogoro baina ya wanyama na
binadamu? (alama4) *Kyo*
5. Ni kwa nini mzee anatumia balagha katika uzungumzo yake? (alama 1) *Kyo*
6. Eleza maana ya misemo hii kama ilivyotumiwa katika taarifa. (alama 2}*Kyo*
(a) Kupiga milundi
(b) Kuchukua sheria mkononi
7. Eleza maana ya maneno haya jinsi yalivyotumiwa katika taarifa. (alama 2) *Kyo*
(i)Idhilali
(ii) Udhia
(iii) Wakigubia
(iv) Jopo
2 . MUHTASARI
Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali.
Vijana wengi, wake kwa waume, walikuwa ndio tu wakamilishe shughuli ya kusajiliwa chuoni.
Walikuwa bado nadhari zao zimetekwa na ugeni, hawajapata starehe akilini mwao wala kujisikia wamekaribia kama kwao nyumbani.Kwa hakika mazingira yale mapya yalikuwa yanawapa kiwewe kidogo au tuseme hata woga kiasi. Kusema kweli, kwa wakati ule walikuwa hawajui ni maisha ya namna gani yanayo wasubiri mahali pale. Hawakuweza kukadiria kwa uyakinifu wowote iwapo makaazi yao pale ya miaka minne mizima kuanzia wakati ule, yangekuwa na utulivu na raha au pengine yangeondokea kuwa ya roho juu juu na matatizo chungu nzima. Walisubiri.
Walimsubiri mkuu wa Chuo aingie wasikize atakalosema waweze kubashiri vyema mkondo wa
maisha yao utakavyokuwa. Lakini jinsi walivyosubiri Mkuu wa Chuo aingie ukumbini ndivyo wayo wayo lao lilivyozidi kuwacheza shere. Waliwaza: ugeni jamani kweli ni taabu. Mawazo mengi yaliwapitia bongoni mwao. Wakawa kimya ukumbi mzima, kama kwamba wamekuja mazishini
badala ya kuja kusoma. Waliwaza na kuwazua. Waliona au pengine walidhani kuwa hapa kila kitu ni tofauti.
Wanafunzi hawa waliona tofauti nyingi kati ya mambo pale chuoni na yale waliyokuwa wamezoea.
Kwa mfano, mwalimu Mkuu hapa hakuitwa ‘headmaster’' kama kule katika shule za msingi na vile vile shule za upili, bali aliitwa 'vice-chancellor''. Nyumba za kulala hazikuitwa ‘dormitory’ au ‘mabweni’ . kama walivyozoea, bali ziliitwa ‘halls’ kwa sababu sio kumbi za aina yoyote ile bali ni nyumba hasa, zenye vyumba vya kulala, kama nyumba nyingine zozote zile. Shule yenyewe haikuitwa shule au skuli, au hata chuo kikuu kama walivyozoea kuiita walipokuwa shule zao za upili huko, bali hapa wenyewe wenyeji waliita kwa majina mengine kabisa! Mara University, mara Zutafindaki, mara Ndaki kwa ufupi, mara Jamahiriya na kadhalika na kadhalika! Waliwaza: kweli mahali hapa panaweza kumkanganya mtu! Kwa kweli kabisa panaweza kumzubaisha mtu hadi kufikia kiwango cha kuonekana kama zuzu! Hata hivyo hawakuvunjika moyo, bali walipiga moyo konde wakanena kimoyomoyo: potelea mbali Ukiyavulia nguo, yaoge! Walikuwa wamo katika hali hii ya kurandaranda katika ulimwengu wa mawazo pale katika ulimwengu wao mpya, ulimwengu mwingine kabisa usiofanana hata chembe na ule waliouzoea, Mkuu wa Chuo alipoingia.
Kuingia Mkuu wa Chuo, wote walisimama kwa pamoja na kwa mjiko, wamekauka kama askari katika
gwaride. kuona hivyo, Mkuu wa Chuo akawaashiria wakae tu, bila kujisumbua. Kicheko kikawatoka bila kukosa adabu na heshima, kisha wakakaa kwa makini. Ndio mwanzo wakajisikia wamepoa.
Kuona kuwa sasa wametulia na wamestarehe, Mkuu wa chuo akaanza kwa kuwaamkua, kisha
akawajulisha kwa wakuu wa vitivo mbali mbali na idara mbali mbali waliokuwa wamekaa pale
jukwaani alipo yeye upande huu na huu.
Kufikia hapo, alaka ikawa imeungwa baina ya wenyeji na wageni wao. Kila mtu akaona mambo
yamtesibu tena, huo bila shaka ni mwanzo mwema, na kama ilivyosemwa na wenye busara, siku
njema huonekana asubuhi. Hii, kwa wote ndiyo asubuhi: na si asubuhi tu, bali ni asubuhi njema, si haba.
Maswali
a) Ukirejelea aya ya kwanza na ya pili, eleza ni kwa nini wanafunzi walikuwa na wasiwasi.
(Maneno 45 - 50) (alama 6) *Kyo*
b) Ni mambo gani mageni ambayo wanafunzi walikumbana nayo, (Maneno 20 - 25) (alama 3) *Kyo*
c) Bila kupoteza maana, fupisha aya tatu za mwisho kwa kutumia maneno yako mwenyewe.
(Tumia maneno 40 - 45) (alama 6) *Kyo*
3. MATUMIZI YA LUGHA
A. (i) Onyesha kirai katika sentensi hii (alama 1) *Kyo*
Kalamu yake ilipotea
(ii) Bainisha vielezi katika sentensi hizi na utaje ni vya aina gani. (alama 4) *Kyo*
(a) Mpishi hatapika leo jioni
(b) Mwanafunzi ameenda shuleni.
B. Tambulisha viwakilishi katika sentensi hizi na utaje ni vya aina gani. (alama 4) *Kyo*
(i) Wao wanatazama runinga
(ii) Cha mlevi huliwa na mgema
C.. Tumia viashiria visisitizi vya karibu katika sentensi ukitumia nomino zifuatazo
(alama 2) *Kyo*
(i) Mitume …………………………………………………………………………………
(ii) Pahali ……………………………………………………………………………………...
D. Bila kubadilisha maana, andika sentensi zifuatazo ukitumia kirejeleo cha ngeli kifaacho,
(alama 2) *Kyo*
(i) Nyumbu alishinda farasi
(ii) Milango yote ilijijfunga ovyo nenda ukafunge.
E. Andika kisawe cha (alama1) *Kyo*
Dunia …………………………………………………………….
4
F. Andika sentensi zifuatazo kulingana na maagizo. (alama 4) *Kyo*
(i) Barmasai huzungumza kilatini vizuri sana (wakati usiodhihirika)
(ii) Mtoto huyu hula chakula kingi sana. (kanusha katika hali ya ukubwa)
G. Unda majina kutokana na vitenzi hivi. (alama2) *Kyo*
(i) subiri ………………………………………….
(ii) Tazama ……………………………………………
H. Andika sentesi hii katika usemi wa taarifa
1. "Njoo hapa" Askari alimwita Koech. (alama 2) *Kyo*
2. I. Andika kinyume cha neno lililopigwa mstari. (alama 2) *Kyo*
Alipokuwa akienda kulala usiku aliushindika rnlango, na asubuhi allipoamka
………………………………… na akatoka nje.
3. J. Ainisha maneno yote katika sentensi hii (alama 3) *Kyo*
Wanakijiji hawa wote ni wazembe mno,
4. K. Unganisha maneno haya ili kuunda neno moja. (alama 2) *Kyo*
(i) Mwana wetu ………………………………………………………………
(ii) Tawi lake ………………………………………………………………………
L. Kwa kutumia mifano katika sentensi, onyesha matumizi ya alama hizi za. uakifishaji.
(alama 2) *Kyo*
(i) dukuduku
(ii) parandesi
5. M. Tunga sentensi kuonyesha tofauti kati ya (alama 2) *Kyo*
(i) Dagaa
(ii) Tagaa
6. N. Ngeli ya zi katika wingi ina viambishi mbalimbali katika nomino zake. Onyesha mabadiliko
haya na kwa kila moja,toa mifano miwili ya sentensi. (alama 4) *Kyo*
7. O. Eleza maana ya methali ifuatayo. (alama2) *Kyo*
Kipya kinyemi ingawa kidonda.
4. ISIMU JAMII
5. Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali.
B: Matoke
A: Ishirini
C: Chapati nyama
A: Thelathini
D: Chips kuku
A: Mia selasini
B: Ugali ng'ombe
A: Hamsa
Maswali
8. a) Ainisha sajili ya mazungumzo haya. (alama1) *Kyo*
b) Eleza sifa za rejista iliyotumika katika mazungumzo haya. (alama 5) *Kyo*
c) Taja na ueleze mambo yoyote manne yanayoathiri namna watu wanavyotumia lugha.
(alama4) *Kyo*






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers