Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Eleza dhima ya fasihi simulizi

Eleza dhima ya fasihi simulizi.

Answers


Mitch
1. Huburudisha, huliwaza na kufurahisha Jamii Kama vile nyimbo Za kazi huimbwa kuwaondolea watu uchovu wakati wa kazi.
2. Huhifadhi historia ya Jamii kwa vile hupokezwa kwa mdomo kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
3. Hukuza uwezo wa kufikiri na kudadisi hasa katika tanzu Kama mafumbo,vitendawili na methali.
4. Hukuza lugha kupitia vipera Kama vile ulumbi,malumbano ya utani na misimu na utambaji wa hadithi.
5. Fasihi simulizi huadilisha kwa vile katika hadithi matendo mabaya hukashifiwa.
6. Hutambulisha jamii na utamaduni wake kupitia tanzu Kama vile visasili, miviga na nyimbo.
7. Fasihi simulizi ni nguzo ya kuunganisha watu kwa vile uwasilishaji wa fasihi simulizi huhitaji uhusika wa watu hivyo umoja hujengeka.
8. Hukuza uzalendo kwa vile watu wanaposhiriki katika miviga ya jando, harusi na matambiko,wao hujitambulisha na kuionea fahari jamii yao .
Mitch_254 answered the question on April 12, 2018 at 07:20

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions