Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Jadili mbinu ya kinaya katika kigogo

Jadili mbinu ya kinaya katika kigogo

Answers


Noah
Kinaya(irony)-ni hali ya mambo katika riwaya ama hadithi kuwa kinyume na matarajio.
(i)Habari zinazotolewa na mjumbe katika rununu ni za kinaya,kuwa wanasagamoyo wasirudishe maendeleo nyuma bali wafurahie ufanisi ambao umepatikana katika kipindi cha miaka tisini baada ya uhuru.Ujumbe huu ni kinaya kwa vile Sagamoyo hakuna maendeleo wala ufanisi.
(ii)Boza anadai kuwa kulipa kodi na kujenga nchi ni kujitegemea,kauli hii ni kinaya kwa vile kodi wanayolipa wanasagamoyo haitumiki kujenga nchi kwa vyovyote vile.
(iii)Sudi anasema kuwa katika kipindi cha mwezi mzima wa uhuru wale mali walizochuna kwa miaka sitini.Ni kinaya kwa kuwa hakuna walichovuna,Viongozi hujilimbikizia mali.
(iv)Boza anamwambia Sudi kuwa wanatia doa kwa kila jambo nzuri.Ni kinaya kwa vile hakuna mambo Mazuri ambayo Majoka amefanya Sagamoyo.
(v)Wanasagamoyo kusheherekea miaka sitini ya uhuru ni kinaya kwani hakuna cha muhimu kusheherekewa.
Boza anadai kuwa Kinyango chake chapendeza na kufanana na shujaa Marara Bin Ngao,ni kinaya kwani kinyango hicho hakifanani na shujaa huyo.
(vi)Mzee Majoka kudai kuwa anamheshimu Sudi ni Kinaya kwani Majoka hana heshima kwa raia wake,nia yake ni kutaka Sudi amchongee kinyango.


Kibet Koina answered the question on January 5, 2019 at 18:35

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions