Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Fafanua sifa kumi za mzee Mago katika hadithi ya tumbo lisiloshiba.

Fafanua sifa kumi za mzee Mago katika hadithi ya tumbo lisiloshiba.

Answers


Kavungya
i) Mwenye bidii – anajitahidi kupigania haki za wanamadongoporomoka.
Ana mkahawa madongoporomoka.
ii) Mtetezi/mpenda haki – Anatafuta wakili ambaye hajahongwa ili kutetea haki ya wanyonge.
Hapuuzi uvumi kuhusu uwezekano wa vipande vyao vya ardhi kuchukuliwa.
Iii) Mwenye hekima/busara – Anafahamu vyema matokeo ya wingu linalotarajiwa kupigania haki zao.
iv) Amepevuka/mwerevu – Anafahamu uzito wa kesi unaotokana na ardhi.
- Anafahamu haki haipatikani kwa urahisi.
v) Mzinduzi – Aliwazindua wenzake na kuwapa nasaha kuhusu maendeleo.
- Aliwatahadharisha kwamba wachunguze ni maendeleo gani yatakayonufaisha.
vi) Jasiri – Analijibu jiyu kwa kuliambia wanamadongoporomoka hawataondoka.
vii) Mshawishi – Aliwashawishi wanyonge wenzake watafute wanasheria waaminifu ili wasaidie kufafanua vipengele vigumu vya sheria kama njia ya kuwavukisha vikwazo ili wapate suluhisho.
ix) Mpenda ushirikiano – Anashirikiana na wanyonge wenzake katika kutafuta uvumbuzi wa kunyakuliwa kwa ardhi yao.
x) Mwenye matumaini – Aliamini ardhi ya wanamadongoporomoka itabaki mikononi mwao. Hata baada ya vibanda kubomolewa
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 07:21

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions