Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Aliyeumwa na nyokaakiona ung’ong’o hushtuka a) Weka dondoo hili katika muktadha b) Eleza namna mzungumziwa alivyoumwa na nyoka c) Mzungumziwa anaendeleza vipi maudhui ya ushauri na ukosefu wa...

Aliyeumwa na nyokaakiona ung’ong’o hushtuka
a) Weka dondoo hili katika muktadha
b) Eleza namna mzungumziwa alivyoumwa na nyoka
c) Mzungumziwa anaendeleza vipi maudhui ya ushauri na ukosefu wa utu?

Answers


Kavungya
a) Weka dondoo hili katika muktadha
Maelezo ya mwandishi kuhusu Otii pale nyumbani. Otii alirejelea maisha yake ya awali, alipoumia mguu na kupoteza umaarufu wake.
Otii alikuwa amerejeshwa pale nyumbani kwake kwa amri ya daktari angojee kifo.
Otii alipovunjika mguu na kutumia mikongojo miezi sita, alikataa kurejelea kandanda uwanjani

b) Eleza namna mzungumziwa alivyoumwa na nyoka
• Otii alikuwa uwanjani akichezea timu ya bandari FC
• Kutokana na uhodari wake alikuwa mwiba kwenye timu kinzani ya Yanga kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kombe la klabu bingwa Africa Mashariki na kati.
• Alikuwa amewala chenga mabeki wote wa Yanga na kuelekea kufumua kiki kali kwenye eneo hatari, ndipo jibaba moja la miraba mine lilipomkwaa akaanguka.
• Alianguka vibaya kama gunia la chumvi. Picha ya eksirei ilionyesha kuwa amevunjika mfupa wa muundi na nguyoni.
• Baada ya kuumia aliterekezwa kabisa na maafisa wa Bandari FC
• Hata maafisa wa serikalini hawakumjali hata kidogo.
• -Alitupwa kama masimbi na hakuna aliyemkumbuka.

c) Mzungumziwa anaendeleza vipi maudhui ya ushauri na ukosefu wa utu?
a) i) Ukosefu wa utu.
- Mwandishi anaonyesha kuwa utu umepotea na haupo tena katika jamii.
- Otii anatoa mchango mkubwa kwa kuichezea timu ya Bandari FC na hata timu ya taifa Harambee lakini anapovunjika mguu hakuna anayejali kipaji chake.
- Hakuna fidia anayopewa hata baada ya kuacha mchezo huo kwa kuumizwa.
- Chama cha watu wa nyumbani wanaanza kujadili mazishi ya mtu akiwa bado hai.
- Wanachama wa chama cha nyumbani wanakosa utu na kuanza kujadili kusafirisha maiti ya Otii wakati Otii bado yu hai na anawasikiliza.
- Rehema anakosa utu kwa kumwambukiza Otii maradhi.

ii) Umuhimu wa Kuzingatia ushauri
- Otii anaitwa na rafiki yake na kushauriwa dhidi ya kujihusisha na msichana mrembo Rehema Wanjiru.
- Otii anapuuza ushauri huo na kusema kuwa yuko radhi kuwa nzi na kufia kidondani.
- Matokeo ni kuwa rehema anamuambukiza ugonjwa wenye dalili za Ukimwi. Wote wawili wanafariki mtawalia.
- Otii anamshauri mwenyekiti wa chama nyumbani azikwe Mombasa. Wao walikataa ushauri huo.
- Baadaye wanapata ajali mbaya
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 08:08

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions