Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Jadili matatizo yanayowakumba wakaazi wa Madongo poromoka katika tumbo lisiloshiba

Jadili matatizo yanayowakumba wakaazi wa Madongo poromoka katika tumbo lisiloshiba

Answers


Kavungya
i. Wanamadongoporomoka wanadharauliwa na kutwaliwa ardhi yao
ii. Kuporwa ardhi :ardhi yao imenyanyswa na tabaka la mabwanyenye .
iii. Wanawatoa katika ardhi yon a kuvunja vibanda vyao pasipo hata kuwalipa fidia.
iv. Unyanyasaji huu unafanya kwa wakazi hawa kwa kuwa hawana mtetezi.
v. Haki imenunuliwa na wenye nacho.wanabomolewa vibanda vyao ilhali hawajaonyesha mahali mbadala pa kwenda kuishi.
vi. Ukosefu wa haki :watu wa madongoporomoka hawana haki wenye fedha wanawaona wakazi hawa kama takataka tu.
vii. Ardhi ya madogoporomoka inaponyakuliwa na wenye nacho wanashindwa kupata mtetezi.wanasheria wamenunuliwa na matajiri.ni vigumu kupata mwanasheria mwaminifu.mzee mago anashaurianana wenzake namna ya kuruka viunzi hivi vya kisheria.
viii. Makazi duni:wakazi wa madongoporomoka wanaishi katika makazi yenye mandhari chafu .kulikuwa na mashonde ya vinyesi.
ix. Wanaishi katika vimbanda uchwara vinavyozungukwa na uozona bubujiko la maji machafu.hakuna mamlaka yoyote ya maji taka inayojishughulisha nao.
x. Wakazi wa madongoporomoka wananyimwa fidia inayolingana na thamaka ya makazi yao yaliyopokonywa na mabwanyenye.
xi. Watu wa madongoporomoka wanaachwa njaa baada ya jitu kubwa kula chakula chote .jitu linaingia katika mkahawa mshenzi na kuagiza kila chakula kilichopo kiletwe,jitu linabugia chakula chote huku watu waliokua wamesubiri chakula hicho wakibakia na njaa.
xii. Wakazi wa madongoporomoka wanabaguliwa .sehemu wanaoishi hakuna maendeleo yoyote.kuna uchafu mwingi sana .sehemu hii ilipaswa kusafisha ili walau ifanane na sehemu nyingine za mji huo.
xiii. Wanamdongoporomoka wamekosa usalama.wanaishi kwa wasiwasi sana.wanaamshwa kwa vishindo vya mabuldoza.
xiv. Askari wa baraza la mji wanaangusha vibanda vyao na kuwatimua waliokuwa bado wamelala.jeshi la polisi linawapa ulinzi askari kwa mirau na bunduki .mali zao duni zinaharibiwa.
xv. Wanamdongoporomoka wanalia na kulalamika kwa kukandamizwa na vyombo vya ulinzi.wanakandamizwa kwa sababu ya umaskini wao.matajiri wanawakandamiza
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 08:03

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions