Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Akifisha kifungu kifuatacho “Baba Wafua, ona Barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki” “lo” baba watoto akamaka. Hii barua kweli imetoka kwa mwanangu Wafua. “Waniuliza mimi?” Mama akamjibu...

Akifisha kifungu kifuatacho
“Baba Wafua, ona Barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki” “lo” baba
watoto akamaka. Hii barua kweli imetoka kwa mwanangu Wafua. “Waniuliza
mimi?” Mama akamjibu “Tazama maandishi na anwani basi. Shule ya Msingi ya
Barungani S.L.P 128 Vuga.”

Answers


Kavungya
“Baba Wafula, ona barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki” .
Lo! Baba watoto akamaka. Hii kweli imetoka kwa mwanangu wafua?”
waniuliza mimi?” Mama watoto akamjibu. “Tazama maandishi na anwani
basi. Shule ya msingi ya Burungani, S.L.P. 128 Vuga.”
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 06:44

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ili kupiga vita propaganda za wakoloni mambo leo katika vyuo vikuu vyetu, inafaa kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote. Jambo hili ni... (Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Ili kupiga vita propaganda za wakoloni mambo leo katika vyuo vikuu vyetu, inafaa
    kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote. Jambo hili ni la lazima na linawezekana
    kabisa, ingawa lina matatizo yake. Jambo linalotakiwa kufanya ni kuchukua
    wananchi wenye elimu ya juu wakatafsiri fikra za wazalendo katika Kiswahili. Kwa njia
    hiyo, lugha ya wanachuo itakuwa ndiyo lugha ile ile ya umma

    Ni jambo la kuepukwa kuwa na lugha mbili ambazo zinasaidia kuwatenga na umma.
    Wasomi wetu watakuwa wamekaribia umma kwa kutumia lugha iliyozoeleka na umma
    wenyewe. Jambo linalotutinga ni hili: mara nyingi wasomi wengine waliozoea
    kutakadamu lugha ya Kiingereza wanapojaribu kuwaeleza watu wengine jambo la
    kieleimu au kitaalamu, hushindwa kabisa. Wao huchanganya sana maneno ya
    Kiingereza na Kishwahili hata kufikia kiasi ambacho mtu wa kawaida haelewi
    chochote.

    Kwa kuwa wakoloni mamboleo wameelewa kwamba lugha ni kioo cha kuchujia
    utamaduni, miaka ya hivi karibuni wamejifunza kwa dhati kuliko wakati mwingine
    kupigania ufundishaji wa lugha zao, hususa, Kifaransi na Kiingereza. Wakati huo wao
    wanatoa porojo kuwa kugha ya Kiswahili haifai na kwamba ni lugha ya watumwa.
    Kwa mfano, utaona katika maandishi mngi kila wanapoorodhesha lugha kuu za dunia.
    Kiswahili hakionyeshwi katika hizo.

    Badala yake wanakiweka kwenye kiwango sawa na Kiganda, Kikikuyu, Kinyamwezi
    na lugha kadha wa kadha za kikabila. Hiyo ni harakati kubwa ya kudanganya umma
    na kukivua Kiswahili hadhi yake ilhali lugha hii inatumiwa na zaidi ya watu milioni
    mia moja wanaosambaa katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Kwa kutumia hila hii,
    wao wanasadikisha watu wengi ili wachukulie Kiswahili kama lugha nyimgine ya
    kikabila. Ndiposa hawa wakoloni mamboleo wanawashawisha baadhi ya watumiaji wa
    Kiswahili wastawishe lugha za makabila mabalimbali na kuonyesha kwamba
    umaarufu wa lugha hizo ni sawa na Kiswahili. Hayo bila shaka ni mawazo. Ukweli
    ulioko ni kwamba mawazo kama haya yawezi keundeleza ukabila. Hata hivyo sharti
    kueleweka kwamba kusema hivyo si kudhalilisha umuhimu wa kukuza lugha za
    kikabila. Tusemacho ni kuwa ukuzaji wa lugha hizo ungekuwa na kusidi moja kuu
    ambalo ni kustawisha Kiswahili kufika ngazi za kimataifa.

    Swali ambalo ni muhimu kujiuliza ni hili: Wakoloni - mamboleo wanatuonaje
    tunapokazania Kiswahili? Je, wanaona ni faida kwao au kwetu? Jambo muhimu zaidi
    ni kutamba jinsi Kiswahili kinavyotuwezesha kuungana na kuwa kitu kimoja. Ni dhahiri
    kwamba wakoloni mamboleo hawafurahili wanapoona kishahili kikituunganisha.
    Machoni mwao Kiswahili ni ishara mojawapo ya kujikomboa kwetu kutokana na
    minyororo yao. Hivi si kusema kwamba hapupaswi kujifunza kiingereza, Kifaranza au
    Kijerumani, la hasha. Tunachosema ni kwamba tutumie Kiswahili ambacho ni kioo
    cha utamaduni wetu.

    (a) Mwandishi amesema nini kuhusu utengano kati ya umma wa wasomi?
    ( Maneno 30 – 40)
    (b) Eleza pingamizi zilizowekwa na wakoloni- mamboleo ili kudunisha
    Kiswahili (maneno 40 – 50)
    (c) Kulingana na mwandishi ni sababu gani zinazofanya wakoloni mamboleo
    kupinga maendeleo ya Kiswahili?

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Andika kwa udogo ;ndege mkubwa alitua dirishani (Solved)

    Andika kwa udogo ;ndege mkubwa alitua dirishani.

    Date posted: June 15, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana ya kiimbo na onyesha dhima yake (Solved)

    Eleza maana ya kiimbo na onyesha dhima yake.

    Date posted: June 9, 2019 .    Answers (1)

  • Taja aina mbili za ala (Solved)

    Taja aina mbili za ala

    Date posted: June 9, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha matumizi ya hali "ni" katika wing I. (Solved)

    Onyesha matumizi ya hali "ni" katika wing I.

    Date posted: May 14, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana ya upangaji lugha na ufafanue sababu ya shughuli hiyo (Solved)

    Eleza maana ya upangaji lugha na ufafanue sababu ya shughuli hiyo

    Date posted: May 14, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza dhima mbili ya kiimbo (Solved)

    Dhima ya kiimbo

    Date posted: May 14, 2019 .    Answers (1)

  • Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo mpitapo kwake mtampata (Solved)

    Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo mpitapo kwake mtampata.

    Date posted: May 14, 2019 .    Answers (1)

  • Mambo yepi yanayoweza kusababisha kufa kwa lugha? (Solved)

    Mambo yepi yanayoweza kusababisha kufa kwa lugha?

    Date posted: May 14, 2019 .    Answers (1)

  • Taja na ueleze dhima tano ambazo sajili za lugha hutekeleza (Solved)

    Dhima ambazo sajili za lugha hutekeleza

    Date posted: May 14, 2019 .    Answers (1)

  • UFAHAMU Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Ulimwengu unatakiwa kuzua mbinu za kulitatua tatizo la ufukara ambao ni kikwazo kikuu cha juhudi za maendeleo. Ufukara unayakabili mataifa mengi yanayoendelea... (Solved)

    UFAHAMU
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
    Ulimwengu unatakiwa kuzua mbinu za kulitatua tatizo la ufukara ambao ni
    kikwazo kikuu cha juhudi za maendeleo. Ufukara unayakabili mataifa mengi
    yanayoendelea na kuyatosa kwenye shida nyingi huku mataifa ya magharibi
    yakizidi kupiga hatua kubwa za kimaendeleo. Tofauti iliyopo kati ya mataifa
    yanayoendelea na yaliyoendelea inaendeiea kuongezeka kila siku.
    Miongoni mwa sababu zinazochangia katika ufukara huu ni pamoja na ufisadi,
    uongozi mbaya, turathi za kikoloni na uchumi unaotegemea kilimo ambacho
    hutegemea mvua isiyoweza kutabirika. Vilevile, mataifa yanayoendelea yana idadi
    kubwa ya watu inayoupiku uwezo wa mataifa husika. Pamoja na haya, mataifa
    haya hayana uwezo wa kuwakomboa raia wake kutoka katika lindi la umaskini
    huu unaokithiri. Ukosefu wa elimu na nafasi adimu za kazi huchangia pia katika
    tatizo hili. Ni wazi kuwa ufukara una athari hasi kote ulimwenguni. Aghalabu,
    ufukara huchipuza matendo mabaya. Ni rahisi kuwashawishi wananchi maskini
    kushiriki katika uhalifu iii kujinasua kutoka kwenye lindi la kimaskini. Udhaifu huu
    huweza kuzaa mbegu ya kuatika maovu ya kila aina ukiwemo ugaidi. Mataifa
    yaliyoendelea yanatakiwa kuyaburai madeni yanayoyadai mataifa yanayoendelea
    kama njia moja ya kupambana na ufukara. Mataifa haya maskini hutumia asilimia
    kubwa ya mapato ya kitaifa kuyalipia madeni haya. Hali hii imeyafanya mataifa
    haya kushindwa kujikwamua kutoka kwenye minyororo ya ufukara. Njia nyingine
    ya kuyasaidia mataifa haya ni kukubali kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya
    mikopo kwa nchi husika.
    Mataifa yanayoendelea nayo yanatakiwa kuchukua hatua katika kuwanusuru raia
    wake kutoka kwenye dhiki hii.Ni sharti yaibuke na mikakati kabambe ya
    kupambana na ufukara. Itakuwa na faida kubwa iwapo mataifa haya yataunda
    sera zinazotambua ufukara kama tatizo kuu linalozikabili na kuweka mikakati ya
    kuwaokoa raia wake kutoka kwenye tatizo hili. Pamoja na mikakati hii ni kuzalisha
    nafasi za kazi, kuimarisha miundo msingi,kuendeleza elimu inayolenga kutatua
    matatizo maalumu katika jamii na kupanua viwanda. Kuna pia haja ya viongozi
    kuwa waangalifu ili mfumo wa soko huru ambao unaendelezwa na mataifa
    yaliyoendelea usiishie kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia. Maamuzi yote ya
    sera za kiuchumi sharti yauzlngatie uhalisia wa maisha ya raia wa mataifa haya.
    (a) Eleza athari za madeni kwa nchi zinazoendelea.
    (b) Kwa nini umaskini unatawala mataifa yanayoendelea?
    (c) Mwandishi anatoa mapendekezo yapi kwa mataifa yanayoendelea katika
    kutatua tatizo la ufukara?
    (d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa yanayoendelea?
    (e) Taja visawe vya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu.
    (i)Turathi za kikoloni
    (ii) Kuatika
    (iii) Kuyaburai

    Date posted: May 7, 2019 .    Answers (1)

  • MUHTASARI (alama 15) Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima... (Solved)

    MUHTASARI (alama 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa
    kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima sawa. Utaifa hujengwa kwenye
    misingi ya mapenzi kwa nchi, Utambuzi wa cheo, eneo, hadhi, rangi na hata
    makabila wanakotoka raia wa taifa moja si chanzo cha kuwatanganisha. Nchi moja
    huweza kuundwa na watu walio na tofauti chungu nzima zikiwemo tofauti za
    kikabila, kitabaka na kimawazo. Hata hivyo, watu hao huwa na folsafa na imani
    sawa kama taifa inayoashiriwa hasa na wimbo wa taifa. Hata hivyo haya yotc
    hayawezi kuwafikia katika kiwango cha kuunda taifa. Uzalendo ndio mhimili
    mkuu wa utaifa. Uzalendo ni mapenzi aliyo nayo mtu kwa nchi yake. Mapenzi
    haya humwongoza mtu katika mawazo yake, itikadi yake, matendo yake,
    matamanio yake na mkabala wake kuhusu nchi na hatima ya nchi yake.
    Mzalendo hawezi kushiriki katika matendo yanayoweza kuiletea nchi yake
    maangamizo kwa vyovyote vile. Mzalendo huongozwa na mwenge wa wema.
    Mzalendo hawezi kushiriki kwenye shughuli zozote zinazohujumu mshikamano wa
    kitaifa. Yeye hatawaliwi na ubinafsi wa kutaka kufaidi nafsi yake naya jamii
    yake finyu. Matendo yake yote huongozwa na ari ya kuiboresha nchi yake.
    Anayeipenda nchi yake hujiepusha na ulafi wa kujilimbikizia mali. Yuko radhi
    kuhasirika mradi taifa lake linufaike.
    Utaifa ni mche aali unaopaliliwa kwa uzalendo, kuepuka uchu wa nafsi na taasubi
    hasi zikuwepo za kikabila na ubinafsi. Hali hii inapofikiwa, hatima ya taifa na
    mustakabali wa raia wake huwa wenye matumaini makubwa.
    (a) Kwa maneno 40 - 50 dondoa sifa kuu za utaifa.
    (b) Ni nini misingi ya kutathmini mzalendo? (maneno 60 - 70)

    Date posted: May 7, 2019 .    Answers (1)

  • Tumia nomino yoyote katika ngeli ya I-I kutunga sentensi. (Solved)

    Tumia nomino yoyote katika ngeli ya I-I kutunga sentensi.

    Date posted: May 7, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga neno lenye muundo huu wa silabi: Irabu + konsonanti + konsonanti + irabu (Solved)

    Tunga neno lenye muundo huu wa silabi:
    Irabu + konsonanti + konsonanti + irabu

    Date posted: May 7, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi hii upya kwa kufuata maagizo: Wasichana wanaingia darasani kwa haraka (andika kinume chake) (Solved)

    Tunga sentensi hii upya kwa kufuata maagizo: Wasichana wanaingia darasani kwa haraka (andika kinume chake)

    Date posted: May 7, 2019 .    Answers (1)

  • Tambua kiambishi awali na tamati kati neno: Alalaye (Solved)

    Tambua kiambishi awali na tamati kati neno: Alalaye

    Date posted: May 7, 2019 .    Answers (1)

  • Ainisha vivumishi katika sentensi hii: mzee mwenyewe ni mkongwe na amepewa zawadi kwa kuwa shamba lake lilitoa mazao mengi. (Solved)

    Ainisha vivumishi katika sentensi hii: mzee mwenyewe ni mkongwe na amepewa zawadi kwa kuwa shamba lake lilitoa mazao mengi.

    Date posted: May 7, 2019 .    Answers (1)

  • Askari wasipopiga doria wala kushikiana na raia hawatakuwa wametuhakikishia usalama. (yakinisha sentensi hii) (Solved)

    Askari wasipopiga doria wala kushikiana na raia hawatakuwa wametuhakikishia usalama. (yakinisha sentensi hii)

    Date posted: May 7, 2019 .    Answers (1)

  • "Shughuli yetu itakamilika kesho", mama alimwambia mwanaye Juma. (Andika katika usemi wa taarifa). (Solved)

    "Shughuli yetu itakamilika kesho", mama alimwambia mwanaye Juma.
    (Andika katika usemi wa taarifa).

    Date posted: May 7, 2019 .    Answers (1)

  • Dhihirisha matumizi matatu tofauti ya kimaana yatakayotokea ketenzi "ona" kikinyambuliwa katika kirai hiki "ona ndoto". (Solved)

    Dhihirisha matumizi matatu tofauti ya kimaana yatakayotokea ketenzi
    "ona" kikinyambuliwa katika kirai hiki "ona ndoto".

    Date posted: May 7, 2019 .    Answers (1)