Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ili kupiga vita propaganda za wakoloni mambo leo katika vyuo vikuu vyetu, inafaa kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote. Jambo hili ni...

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Ili kupiga vita propaganda za wakoloni mambo leo katika vyuo vikuu vyetu, inafaa
kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote. Jambo hili ni la lazima na linawezekana
kabisa, ingawa lina matatizo yake. Jambo linalotakiwa kufanya ni kuchukua
wananchi wenye elimu ya juu wakatafsiri fikra za wazalendo katika Kiswahili. Kwa njia
hiyo, lugha ya wanachuo itakuwa ndiyo lugha ile ile ya umma

Ni jambo la kuepukwa kuwa na lugha mbili ambazo zinasaidia kuwatenga na umma.
Wasomi wetu watakuwa wamekaribia umma kwa kutumia lugha iliyozoeleka na umma
wenyewe. Jambo linalotutinga ni hili: mara nyingi wasomi wengine waliozoea
kutakadamu lugha ya Kiingereza wanapojaribu kuwaeleza watu wengine jambo la
kieleimu au kitaalamu, hushindwa kabisa. Wao huchanganya sana maneno ya
Kiingereza na Kishwahili hata kufikia kiasi ambacho mtu wa kawaida haelewi
chochote.

Kwa kuwa wakoloni mamboleo wameelewa kwamba lugha ni kioo cha kuchujia
utamaduni, miaka ya hivi karibuni wamejifunza kwa dhati kuliko wakati mwingine
kupigania ufundishaji wa lugha zao, hususa, Kifaransi na Kiingereza. Wakati huo wao
wanatoa porojo kuwa kugha ya Kiswahili haifai na kwamba ni lugha ya watumwa.
Kwa mfano, utaona katika maandishi mngi kila wanapoorodhesha lugha kuu za dunia.
Kiswahili hakionyeshwi katika hizo.

Badala yake wanakiweka kwenye kiwango sawa na Kiganda, Kikikuyu, Kinyamwezi
na lugha kadha wa kadha za kikabila. Hiyo ni harakati kubwa ya kudanganya umma
na kukivua Kiswahili hadhi yake ilhali lugha hii inatumiwa na zaidi ya watu milioni
mia moja wanaosambaa katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Kwa kutumia hila hii,
wao wanasadikisha watu wengi ili wachukulie Kiswahili kama lugha nyimgine ya
kikabila. Ndiposa hawa wakoloni mamboleo wanawashawisha baadhi ya watumiaji wa
Kiswahili wastawishe lugha za makabila mabalimbali na kuonyesha kwamba
umaarufu wa lugha hizo ni sawa na Kiswahili. Hayo bila shaka ni mawazo. Ukweli
ulioko ni kwamba mawazo kama haya yawezi keundeleza ukabila. Hata hivyo sharti
kueleweka kwamba kusema hivyo si kudhalilisha umuhimu wa kukuza lugha za
kikabila. Tusemacho ni kuwa ukuzaji wa lugha hizo ungekuwa na kusidi moja kuu
ambalo ni kustawisha Kiswahili kufika ngazi za kimataifa.

Swali ambalo ni muhimu kujiuliza ni hili: Wakoloni - mamboleo wanatuonaje
tunapokazania Kiswahili? Je, wanaona ni faida kwao au kwetu? Jambo muhimu zaidi
ni kutamba jinsi Kiswahili kinavyotuwezesha kuungana na kuwa kitu kimoja. Ni dhahiri
kwamba wakoloni mamboleo hawafurahili wanapoona kishahili kikituunganisha.
Machoni mwao Kiswahili ni ishara mojawapo ya kujikomboa kwetu kutokana na
minyororo yao. Hivi si kusema kwamba hapupaswi kujifunza kiingereza, Kifaranza au
Kijerumani, la hasha. Tunachosema ni kwamba tutumie Kiswahili ambacho ni kioo
cha utamaduni wetu.

(a) Mwandishi amesema nini kuhusu utengano kati ya umma wa wasomi?
( Maneno 30 – 40)
(b) Eleza pingamizi zilizowekwa na wakoloni- mamboleo ili kudunisha
Kiswahili (maneno 40 – 50)
(c) Kulingana na mwandishi ni sababu gani zinazofanya wakoloni mamboleo
kupinga maendeleo ya Kiswahili?

Answers


Kavungya
a)i) Wasomi kutafsiri fikra za wazalendo kwa Kiswahili ili kufika/kukaribiana
na umma.
ii) Wasomi wanapojaribu kueleza umma jambo la kielimu ama kitaalamu
hushindwa kabisa kulieleza kwa lugha ya Kiswahili.
II a) Eleza maana ya methali ifuatayo kwa kifupi: Uji ukiwa moto haupozwi
kwa ulimi
b) Eleza maana ya misemo ifuatayo:
i) Kukunjua jamvi
ii) Kula mate
c) Maana moja ya ‘andika’ ni kuchora maandishi ubaoni, kitabuni n.k
Toa maana nyingine ya neno hilo.
iii) Badala yake wanachanganya Kiswahili na Kiingereza kiasi kwamba
wanaosikiliza hawaeleqi hata kidogo lugha mbili zinatenga wasomi na
umma-tuepuke kutumia lugha mbili
b) i) Wanapigania ufundishaji wa lugha zao kama kiingereza na kifaraansa.
ii) Wanatoa porojo kuwa lugha ya Kiswahili haifai na kwamba ni lugha ya
watumwa
iii) Wanaaishia lugha kuu za dunia kwa upendeleao na wanaweka Kiswahili
katika kiwango sawa na lungha za Kikabila.
iv) Kuwashawishi watu kustawisha lugha za kikabila na lugha za mababa zao.
c) i) Kuunganisha wenyewe- kutuunganisha
ii) Kujenga utamaduni/kuukwasisha utamaduni au kioo cha utamaduni wetu.
iii) Kukomboa wenyewe.
iv) Kinashindania hadhi na lugha zao.
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 06:42

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions