Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata Kuna sayansi mpya inayoitwa “cloning” kwa lugha ya Kiingereza. Pengine kwa sasa tuite “kutumbisha.” Sayansi hii tayari imeleta mapinduzi makubkwa...

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata
Kuna sayansi mpya inayoitwa “cloning” kwa lugha ya Kiingereza. Pengine kwa sasa tuite
“kutumbisha.” Sayansi hii tayari imeleta mapinduzi makubkwa katika uzalishaji mimea
na uvunani. Imesemekana ya kwamba, ghairi ya wivu na kijicho baina ya jamii
mbalimbali ulimwenguni, aina hii ya sayanzi ina uwezo na kuangamiza kabisa janga la
njaa katika sayari hii yetu. Kivipi? Rahisi kabisa. Ni kwamba mbegu moja tu ya aina
yoyote ya mmea, baada ya kuneemeshwa vyumba vyake vidogo ambavyo ndivyo hasa
msingi wa uhai vinaweza kunyunyiziwa dawa maalum ili vitawanyike mara hata
mamilioni na kuwa mimea kamili…. Mamilioni!

Sayansi hii tarari inatumiwa kukuza viazi na vyakula vingine. Hii ina maana ya kwamba
mashamba makubwa si muhimu siku hizi, yaani vyakula vingi kabisa vinaweza kukuzwa
mahali padogo sana. Kwa hivyo hivi karibuni tu, kutakuwa hakuna haja ya kupigania
mashamba.

Vyema. Hebu sasa tuangalie zilizokwishapigishwa hii sayansi ya “kutumbisha” na mahali
binadamu alipofika kimaendeleo kwa sababu ya hatua hizo. Jambo la kwanza sayansi hii
tayari imeshatumiwa kuzalishia wanyama wengi, wengi sana wadogo wadogo kwa lengo
la kuendeleza mbele utafiti. Kufikia sasa, wanyama hawa waliotengenezwa na binadamu
katika maabara yake bado wanahifadhiwa mumo humo walimotengenezwa. Hii ni hatua
kubwa na binadamu anastakili pongezi kwa jinsi anayotumia akili yake kuvumbua ibura
hizi zote.

Hata hivyo imesemwa kwamba kuchamba kwingi ni kuondoa mavi. Binadamu kama
ijulikanavyo, anajaribu sana jujitakasa kwa kujitenga mbali sana na asili yake ya unyama
ili aufikie ubinadamu mkamilifu. Hapana ubaya hapo. Lakini tukirudi nyuma tunakuta ya
kwamba binadamu sasa aneingia tama kubwa sana kuliko wakati wowote ule. Tamaa hii
imeletwa na ujuzi wake katika sayansi hii ya “kutumbisha.” Sasa binadamu ana jua
vizuri sana kwamba kwa vile ana ujuzi wa kutengeza panya na hata kondoo katika
maabara basi hata ujuzi wa kutengeneza binadamu pia anao! Na hapo ndipo tatizo lilipo.
Swali hi hili: Je, ujuzi huu utatufikisha wapi? Na kikomo chake kitakuwaje?

Binadamu sasa ujuzi wake unamtia wasiwasi. Wataalam wa sayansi hii wamejiuliza mara
nyingi nini kitakachotokea ujuzi huu utakapomilikiwa na mwenda wazimu mweledi.”
Watu kadha wa kadha, miongoni mwao wakiwa wanasiasa wamejiuliza mara
zisizohesabika swali hili: kama Hitler angekuwa na ujuzi huu, angekuwa na lazima gani
ya kuwaulia mbali wayahudi milioni sita wasiokuwa na hitia isipokuwa na nywele
nyeusi na hawakuwa weupe sana kama wazungu? Hitler aliamini ya kwamba “mtu
mzuri” ni mwenye pua ya upanga (kama mzungu), macho ya buluu nywele rangi ya dhahabu na mwenye kimo cha futi sita au zaidi kidogo. Hivyo lengo lake lilikuwa ni
kubuni taifa la watu wazuri pekee ambao mwisho watautawala ulimwengu na kuenea
duniani kote. Katika mpango wake, watu weusi wote wangefaa kuangamizwa tu ili watoe
nafasi kwa watu aliowaona yeye kuwa bora.

Sasa baada ya sayansi hili ya “kutumbisha” kuvumbuliwa, wataalam wametishika sana.
Wamewaza jinsi ambavyo Hitler angeweza kufanya kama angekuwa mjuzi wa taaluma
hiyo.

Kitisho hiki kimezidi kuwatwanga wataalam na wasiokuwa wataalam hivi majuzi tu
ilipogunduliwa maiti ya msichana wa miaka kumi na mine huko milima ya Andes,
Amerika ya kusini. Msichana huyo alikuwa ametolewa kafara miaka karne tano zilizo
pita lakini hakuoza kwa sababu ya baridi kali ya barafu milimani.

Kwa sababu ya dukuduku la uvumbuzi ambalo haliishi dhana za kiajabu ubongo wa
binadamu, wataalamu wa “kuchezea” maumbile walipomwona msichana huyo maiti,
upesi upesi wakampima. Walipofanya hivyo wakagundua ya kwamba mayai yake ni
timamu kabisa wala hayajaharibiwa na mpito wa karne. Papo hapo wengine wakajiwa na
wazo la kuyatoa mayai hayo na kuyahifadhi kwenye mabara. Tamaa ikazidi zaidi ya
zaidi. Baadhi ya wataalamu wakajiwa na wazo la “kuyaneemesha” mayai hayo na mbegu
za uzazui za wanaume. Kwa lengo gani? Kuunda watoto amabo mama yao alikufa
zamani za kale ili waonekane watakuwa watu wa aina gani!

Sasa fikiria mwenyewe! Watoto hawa wa maabara wakiwa weledi zaidi ya binadamu
yeyote yeyote wa kisasa lakini watiifu kama mbwa na paka itakuwaje? Hakuna
atakayefikiria “kutumbisha” ili tuwe na vijitumwa vyetu vipenzi majumbani mwetu
vinavyofanana nasi badala ya paka na mbwa wasiovishwa nguo?

(a) Andika kichwa kifaacho kwa nakala hii
(b) Kutumia sayansi ya “kutumbisha” kunaweza kumsaidia binadamu kuangamiza
mabaa gani mawili yanayomkabili sasa?
(c) Unadhani ni kwa nini wanyama waliozalishwa kwa kutumia sayansi hii bado
wamo maabarani?
(d) Fafanua methali “kuchamba kwingi nikuondoka na mavi” kulingana na muktadha
wa habari hii
(e) Kuna ubaya gani kutumbisha watu?
(f) Mwandishi anaonekana kutishwa sana na uwezekano wa sayansi ya kutumbisha
kuishia mikononi mwa “wendawazimu weledi” kwani kuna hatari gani?
(g) Eleza kwa ukamilifu matatizo yanayoweza kuukumba ulimwengu iwapo mayai ya
msichana wa Andes yatatumbishwa

Answers


Kavungya
a) Kutumbisha
Sayansi ya kutumbisha
Sayansi mpya
Sayansi ya kutumbisha na matokeo yake
Sayansi ya kutumbisha
Sayansi ya ‘Clong’
Tamaa ya kutumbisha
Ajabu katika uzalishaji
Uzalishaji mpya
Tama ya kutumbisha

b) Njaa
-Upungufu wa ardhi
-Kupigania mashamba

c) Wangali wanafanyiwa utafiti
Hawajui ni madhara gani yanayoweza kuletwe nao/kivao
Hawana uhakika kama wanaweza kuishi nje ya maabara
Sheria haiwaruhusu wanasayansi kuwatoa nje “Yoyote

d) Jinsi binadamu anavyoendelea kufanya utafiti ili ajiondolee unyama ndivyo
anavyojijuta katka maafa au utafiti ukikithiri utaleta maafa.
‘Akijieleza sawasawa
Aliyeshughulikia upande mmoja

e) - Aliyetumbishwa aweza kuwa mweledi zaidi ya binadamu wa kawaida na
kuwatatiza
- Aliyetumbishwa aweza kuwa na uwezo mdogo wa kiakili na hivyo kuwa
mzigo kwa wale wa kawaida
- Ni kuharibu msingi wa jamii
- Aliyetumbishwa si binadamu halisi
- NI kuharibu taasisi za maisha-Utamaduni, itikadi, ndoa, lugha na
kadhalika
- Kutakuwa na maumbile sawa ya watu au kutatokea ukosefu wa maumbile
tofauti.

f) Matumizi mabaya ya ujuzi ule
Mweledi atatumbisha watu wasio wa kawaida
Mweledi aweza kuangamiza ulimwengu huu na kuutawala ulimwengu mpya wote
Kitakuwa na msongamano wa watu duniani
Ukosefu wa huduma muhimu za jamii

g) Watoto hao wanaweza kuwa weledi aidi
Wanaweza kuwa na uwezo mdogo kiakili
Wenti wao watakuwa mayatima
Watarithi kasoro za mwili au magonjwa yasiyo na tiba au yanayo ambukiza na
Kuangamiza binadamu wa kawaida.
Kuwepo kwa uhuru wa kutumbisha mayai ya wafu’
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 08:08

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions