Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Badilisha katika udogo kasha uukanushe udogo huo (i) Guu lake limepona baada ya kuumwa na jibwa la jijini (ii) Nyumba yenyewe ilijengwa bondeni karibu na mto

Badilisha katika udogo kasha uukanushe udogo huo
(i) Guu lake limepona baada ya kuumwa na jibwa la jijini
(ii) Nyumba yenyewe ilijengwa bondeni karibu na mto

Answers


Kavungya
i) Kiguu chake hakijapona baada ya kuumwa na kijibwa cha kijijini
ii) Kijumba chenyewe hakikujengwa kibondeni karibu na kijito
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 07:46

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Eleza matumizi ya ‘Po’ katika sentensi hii Nilipofika nilimwona pale alipokuwa amesimama (Solved)

    Eleza matumizi ya ‘Po’ katika sentensi hii
    Nilipofika nilimwona pale alipokuwa amesimama

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Kutokana na vitenzi tunaweza kuunda majina na pia kutokana na majina tunaweza kuunda vitenzi. Mfano Jina ... (Solved)

    Kutokana na vitenzi tunaweza kuunda majina na pia kutokana na majina
    tunaweza kuunda vitenzi. Mfano
    Jina Kitendo
    Mwuzaji Uza
    Mauzo Uza
    Wimbo Imba

    Sasa kamilisha:
    Jina Kitenzi
    (i) Mnanda
    (ii) Kikomo
    (iii) Ruhusa
    (iv) ashiki
    (v) husudu

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Tunasema: Mtoto huyu mzuri anapendeza Ukitumia majina yafuatayo kamilisha sentensi ukifuata mfano ulio hapo juu (i) Ngome (ii) Mitume (iii) Heshima (iv) Ng’ombe (v) Vilema (Solved)

    Tunasema: Mtoto huyu mzuri anapendeza
    Ukitumia majina yafuatayo kamilisha sentensi ukifuata mfano ulio hapo juu
    (i) Ngome
    (ii) Mitume
    (iii) Heshima
    (iv) Ng’ombe
    (v) Vilema

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza kazi ifanywayo na (i) Mhariri (ii) Jasusi (Solved)

    Eleza kazi ifanywayo na
    (i) Mhariri
    (ii) Jasusi

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Fafanua maana za misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi (i) Kula uyundo (ii) Kula uhondo (Solved)

    Fafanua maana za misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi
    (i) Kula uyundo
    (ii) Kula uhondo

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Andika sentensi zifuatazo ukitumia kinyume cha neno lililoandikwa kwa herufi za Mlazo (i) Usijaribu kupaaza sauti unapoimba (ii) Huyu ni mtu mwenye busara (iii) Binadamu hawezi kumuumbua mwenzake (Solved)

    Andika sentensi zifuatazo ukitumia kinyume cha neno lililoandikwa kwa herufi za
    Mlazo
    (i) Usijaribu kupaaza sauti unapoimba
    (ii) Huyu ni mtu mwenye busara
    (iii) Binadamu hawezi kumuumbua mwenzake

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana ya sentensi hizi (i) Mikono yao imeshikana (ii) Mikono yao imeshikamana (Solved)

    Eleza maana ya sentensi hizi
    (i) Mikono yao imeshikana
    (ii) Mikono yao imeshikamana

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Sahihisha makosa yaliyomo katika sentensi mbili zifuatazo (i) Bei za vitu zimepanda juu sana siku hizi (ii) Weka mizigo kwa gari (Solved)

    Sahihisha makosa yaliyomo katika sentensi mbili zifuatazo
    (i) Bei za vitu zimepanda juu sana siku hizi
    (ii) Weka mizigo kwa gari

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Mababu walituachia msemo maarufu kuwa “ Kuzaa sio kazi. Kazi kubwa ni kulea.” Busara iliyomo katika methali hii inatupambazukia peupe pindi... (Solved)

    Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali
    Mababu walituachia msemo maarufu kuwa “ Kuzaa sio kazi. Kazi kubwa ni kulea.”
    Busara iliyomo katika methali hii inatupambazukia peupe pindi tukianza kuchunguza
    maisha ya vijana wa siku hizi katika jamii zote, hasa zile za Afrika. Kwa upande
    mmoja, maisha ya vijana hawa yanaonyesha cheche ya matumaini kwa maisha ya siku
    za usoni kwa sifa zao za mori na kupenda kujaribu na kushika mambo upesi kama
    sumaku. Lakini kwa upande wa pili, tunashuhudia upotevu wa kimawazo na hulka
    ambayo ndiyo kipingamizi cha kuendelea kwao kama raia wa kutegemewa.

    Kuwanyeshea vijana lawama na kashifa za kila aina hakufai wala hakufui dafu katika
    juhudi za kuwaongoza na kuwalea. Kwa hili hatuna budi kusadiki, “mtoto umleavyo
    ndivyo akuavyo.” Basi hivyo badala ya kuwashambulia vijana wenyewe. Tutafanya
    hivyo kwa imani kuwa “mwiba uchomeako ndiko utokeako.” Kiini cha matatizo ya
    vijana wa leo ni namna ya mwongozo na vielezo wanavyopokea kutoka kwa wazazi,
    waalimu, viongozi wa kijamii wakiwemo pia wale wa medhehebu tofauti na hasa kutokana na vyombo tofauti vya habari: vitabu majarida, filamu, magazeti na
    kadhalika.

    Jamii ina haki gani kuwashtumu vijana iwapo mzazi, tangu utotoni mwao
    amewahubiria maji na huku mwenyewe anakunywa mvinyo? Kama fasihi na
    maandishi mengine wanayoyabugia vijana yamejazwa amali, picha, jazanda na taswira
    zinazohimidi ugeni na kutweza Uafrika, tutashangazwa na nini pale vijana
    watakapoanza kupania zile zile amali za ugenini? Iwapo jamii na mazingira
    wanamokulia vijana yanatukuza kitu kuliko utu. Hatupaswi kupepesa macho na
    kukonyeza tunapowaona vijana wakihalifu sheria zote kwa tamaa ya kujinufaisha binafsi.

    Ni hoja isiyopingika kuwa kulea sio tu kulisha na kuvisha au kumpeleka mtoto
    shuleni sharti itambulike wazi wazi kuwa sehemu kubwa ya elimu na mwongozo
    unaoathiri mienendo ya jijana na watoto haitokani na yale waambiwayo bali hasa yote
    wanaoyashuhudia kwa macho na hisia zao.

    (a) Katika aya ya kwanza, maisha ya vijana wa kisasa yameelezwaje?
    (b) Kwa nini vijana hawapaswi kulaumiwa kulingana na mwandishi
    Maneno 30 – 35
    (c) Eleza sifa za malezi bora
    (Maneno 20 – 25)

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Akifisha kifungu kifuatacho “Baba Wafua, ona Barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki” “lo” baba watoto akamaka. Hii barua kweli imetoka kwa mwanangu Wafua. “Waniuliza mimi?” Mama akamjibu... (Solved)

    Akifisha kifungu kifuatacho
    “Baba Wafua, ona Barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki” “lo” baba
    watoto akamaka. Hii barua kweli imetoka kwa mwanangu Wafua. “Waniuliza
    mimi?” Mama akamjibu “Tazama maandishi na anwani basi. Shule ya Msingi ya
    Barungani S.L.P 128 Vuga.”

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ili kupiga vita propaganda za wakoloni mambo leo katika vyuo vikuu vyetu, inafaa kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote. Jambo hili ni... (Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Ili kupiga vita propaganda za wakoloni mambo leo katika vyuo vikuu vyetu, inafaa
    kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote. Jambo hili ni la lazima na linawezekana
    kabisa, ingawa lina matatizo yake. Jambo linalotakiwa kufanya ni kuchukua
    wananchi wenye elimu ya juu wakatafsiri fikra za wazalendo katika Kiswahili. Kwa njia
    hiyo, lugha ya wanachuo itakuwa ndiyo lugha ile ile ya umma

    Ni jambo la kuepukwa kuwa na lugha mbili ambazo zinasaidia kuwatenga na umma.
    Wasomi wetu watakuwa wamekaribia umma kwa kutumia lugha iliyozoeleka na umma
    wenyewe. Jambo linalotutinga ni hili: mara nyingi wasomi wengine waliozoea
    kutakadamu lugha ya Kiingereza wanapojaribu kuwaeleza watu wengine jambo la
    kieleimu au kitaalamu, hushindwa kabisa. Wao huchanganya sana maneno ya
    Kiingereza na Kishwahili hata kufikia kiasi ambacho mtu wa kawaida haelewi
    chochote.

    Kwa kuwa wakoloni mamboleo wameelewa kwamba lugha ni kioo cha kuchujia
    utamaduni, miaka ya hivi karibuni wamejifunza kwa dhati kuliko wakati mwingine
    kupigania ufundishaji wa lugha zao, hususa, Kifaransi na Kiingereza. Wakati huo wao
    wanatoa porojo kuwa kugha ya Kiswahili haifai na kwamba ni lugha ya watumwa.
    Kwa mfano, utaona katika maandishi mngi kila wanapoorodhesha lugha kuu za dunia.
    Kiswahili hakionyeshwi katika hizo.

    Badala yake wanakiweka kwenye kiwango sawa na Kiganda, Kikikuyu, Kinyamwezi
    na lugha kadha wa kadha za kikabila. Hiyo ni harakati kubwa ya kudanganya umma
    na kukivua Kiswahili hadhi yake ilhali lugha hii inatumiwa na zaidi ya watu milioni
    mia moja wanaosambaa katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Kwa kutumia hila hii,
    wao wanasadikisha watu wengi ili wachukulie Kiswahili kama lugha nyimgine ya
    kikabila. Ndiposa hawa wakoloni mamboleo wanawashawisha baadhi ya watumiaji wa
    Kiswahili wastawishe lugha za makabila mabalimbali na kuonyesha kwamba
    umaarufu wa lugha hizo ni sawa na Kiswahili. Hayo bila shaka ni mawazo. Ukweli
    ulioko ni kwamba mawazo kama haya yawezi keundeleza ukabila. Hata hivyo sharti
    kueleweka kwamba kusema hivyo si kudhalilisha umuhimu wa kukuza lugha za
    kikabila. Tusemacho ni kuwa ukuzaji wa lugha hizo ungekuwa na kusidi moja kuu
    ambalo ni kustawisha Kiswahili kufika ngazi za kimataifa.

    Swali ambalo ni muhimu kujiuliza ni hili: Wakoloni - mamboleo wanatuonaje
    tunapokazania Kiswahili? Je, wanaona ni faida kwao au kwetu? Jambo muhimu zaidi
    ni kutamba jinsi Kiswahili kinavyotuwezesha kuungana na kuwa kitu kimoja. Ni dhahiri
    kwamba wakoloni mamboleo hawafurahili wanapoona kishahili kikituunganisha.
    Machoni mwao Kiswahili ni ishara mojawapo ya kujikomboa kwetu kutokana na
    minyororo yao. Hivi si kusema kwamba hapupaswi kujifunza kiingereza, Kifaranza au
    Kijerumani, la hasha. Tunachosema ni kwamba tutumie Kiswahili ambacho ni kioo
    cha utamaduni wetu.

    (a) Mwandishi amesema nini kuhusu utengano kati ya umma wa wasomi?
    ( Maneno 30 – 40)
    (b) Eleza pingamizi zilizowekwa na wakoloni- mamboleo ili kudunisha
    Kiswahili (maneno 40 – 50)
    (c) Kulingana na mwandishi ni sababu gani zinazofanya wakoloni mamboleo
    kupinga maendeleo ya Kiswahili?

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Andika kwa udogo ;ndege mkubwa alitua dirishani (Solved)

    Andika kwa udogo ;ndege mkubwa alitua dirishani.

    Date posted: June 15, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana ya kiimbo na onyesha dhima yake (Solved)

    Eleza maana ya kiimbo na onyesha dhima yake.

    Date posted: June 9, 2019 .    Answers (1)

  • Taja aina mbili za ala (Solved)

    Taja aina mbili za ala

    Date posted: June 9, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha matumizi ya hali "ni" katika wing I. (Solved)

    Onyesha matumizi ya hali "ni" katika wing I.

    Date posted: May 14, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana ya upangaji lugha na ufafanue sababu ya shughuli hiyo (Solved)

    Eleza maana ya upangaji lugha na ufafanue sababu ya shughuli hiyo

    Date posted: May 14, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza dhima mbili ya kiimbo (Solved)

    Dhima ya kiimbo

    Date posted: May 14, 2019 .    Answers (1)

  • Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo mpitapo kwake mtampata (Solved)

    Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo mpitapo kwake mtampata.

    Date posted: May 14, 2019 .    Answers (1)

  • Mambo yepi yanayoweza kusababisha kufa kwa lugha? (Solved)

    Mambo yepi yanayoweza kusababisha kufa kwa lugha?

    Date posted: May 14, 2019 .    Answers (1)

  • Taja na ueleze dhima tano ambazo sajili za lugha hutekeleza (Solved)

    Dhima ambazo sajili za lugha hutekeleza

    Date posted: May 14, 2019 .    Answers (1)