Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno. Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote...

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno.
Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote mawili
yaliyopita; wanawake makamu ya nyanyake na mamaake-kuu.

Yeye hatarajii kuzaliwa, kukua, kuolewa, kuwa mke wa bwana, kumzalia watoto, na
daima dawamu kuwa ‘mwendani wa jikoni’ akawapikia watoto na bwanake chakula; na
akitoka jikoni aelekee shambani kulima, kichakani kuchanja kuni, mtoni kufua nguo na
kuteka maji ya kutumia nyumbani. Mwanamke wa kisasa huandamana na mwanamume.
Akanyangapo mume naye papo huutia wayo wake.

Mwanamke wa kisasa huenda shule na kujifunza yote yafunzwayo huko. Hushindana na
wanawake kwa wanaume na kuibuka mshindi si mara haba. Huibuka mshindi katika
masomo ya lugha, historia, jiografia, hesabu, sayansi na mengineyo, sawa na
mwanamume.

Mwanamke wa kisasa hutaka kufanya kazi za kibega, akazifanya. Akataka kuwa
mwalimu, akawa. Akataka kuwa daktari, akafanikiwa. Almuradi, siku hizi mwanamke
hufanya kazi yoyote ile afanyayo mwanamume. Kuna wanawake marubani wa ndege,
masonara, waashi, wahandishi, madereva wa magari, mawakili, mahakimu, mawaziri
wakuu na hata marais wa nchi. Hakuna kazi isiyofanywa na mwanamke siku hizi.

Mwanamke wa kisasa hateswi akafyata ulimi. Anapohiniwa yeye hupigania haki yake
kwa dhati na hamasa. Katu hakubali ‘mahali pake’ katika jamii alipotengewa na
wanaume wenye mawazo ya kihafidhina yaliyopitwa na wakati.

Siku hizi mwanamke huolewa tu wakati amepata kazi ya kumwezesha kujikimu maishani
au pale anapokuwa na hakika kwamba biashara yake, iwapo ni mfanyi biashara, imepiga
hatua ya kutomrudisha ukutani.

Mwanamke wa kisasa haamuliwi katika jambo lolote, bali hufanya maamuzi yake
mwenyewe. Kwa upande mwingine, mwanamume wa ‘kisasa’, ambaye bado amefungwa
pingu na taasubi za kiume, hapendezwi na mwanamke huyu. Huuma kidole akatamani ya
kale, lakini wapi! Analazimika kumkubali mwanamke huyu kama mshirika sawa
maishani, na kuishi naye, apende asipende. Shingo upande analazimika kukubali kwamba
mabadiliko haya sio mithili ya kiwingu kipitacho, bali ni ya aushi.

a) Msemo ‘mwendani wa vijungu jiko’ unadhihirisha hali gani ya
mwanamke katika jamii?
b) Jamii imemfanya mwanamke kuwa hayawani wa mizigo. Fafanua
c) Eleza maana ya ‘akanyagapo mume papo huutia wayo wake.’
d) Zungumzia maswala ya ndoa na elimu huku ukilinganisha mwanamke wa
kiasili na wa kisasa.
e) Mwanamume wa kisasa anamwonaje mwanamke wa kisasa?
f) Taja mifano minne ya ‘mawazo ya kihafidhina.
g) Eleza maana ya:
(i) Akafyata ulimu……………………………………………
(ii) Ukatani…………………………………………………….
(iii) Taasubi za kiume………………………………………….
(iv) Aushi…………………….………………………………..

Answers


Kavungya
(a) Mahali pa mwanamke ni jikoni
Kazi yake ni kuitumikia jamii
(b) Anafanyishwa kazi nyingi
(c) Afanyayo mwanamume mwanamke pia hulifanya
fig227620191149.png
(e) Hapendezwi naye. Ni mkaidi, mshindani, mzushi ( 2)
(f) Mahali pake ni jikoni
Akiteswa alipaswa kunyamaza/ kufyata ulimi
Lazima aolewe amzalie mume watoto
Hapaswi kupelekwa shuleni
Anapaswa kufanyiwa uamuzi
Hapaswi kujitetea
Anakazi maalum
(g) (i) Akafyata ulimi – akanyamaza
(ii) Ukatani – umaskini
(iii) Taasubi za kiume fikra/ wazo la kibaguzi/ uchoyo
Mwanamme kuona bora kuliko mke
(iv) Aushi Maisha/ kudumu/ milele/ daima/ alfulela
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 08:51

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions